Makinda akacha mdahalo wa Posho

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Nyongeza posho za wabunge kaa la moto
Monday, 12 December 2011 20:48
0diggsdigg

SPIKA MAKINDA AKIMBIA MDAHALO,WENGI WAZIDI KUPONDA
Waandishi wetu
Mwananchi

SAKATA la posho za wabunge limezidi kuingia katika sura mpya, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kukwepa mdahalo uliohusu mada hiyo, huku Katibu wake, Dk Thomas Kashilillah, akitua mzigo kwa kutotaka ahusishwe tena kwenye mjadala huo.Wakati viongozi hao wa juu wa Bunge wakikwepa kuzungumzia suala hilo, wasomi, wanaharakati na viongozi wa dini kutoka kona mbalimbali za nchi, wamekuja juu wakipinga nyongeza hiyo.

Makinda akacha mdahalo

Jana, Makinda alikwepa kipindi cha luninga cha Channel Ten cha Asubuhi Njema ambacho mada yake ilikuwa kuzungumzia nyongeza ya posho za wabunge akisema "iwapo mjadala wenu ni kuhusu posho, sitashiriki kipindi hicho."

Mtangazaji wa kipindi hicho, David Ramadhan alisema awali, aliwasiliana na Spika Makinda kwamba angekuwa mgeni katika kipindi hicho, lakini dakika za mwisho, aligeuka na kusema asingeweza kushiriki mjadala huo iwapo mada ni nyongeza ya posho za wabunge.

“Jamani ilikuwa tuwe na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ambaye hata hivyo amesema hataweza kushiriki kipindi iwapo mjadala wenyewe ni huo unaohusiana na ongezeko la posho za wabunge,”alisema mtangazaji huyo akiwajulisha watazamaji.

Kutokana na hali hiyo, Ramadhani aliwasiliana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ili atoe ufafanuzi kuhusu msimamo wa CCM juu ya nyongeza hiyo ya posho. Nape alikazia msimamo wa chama hicho kuwa wanapinga ongezeko hilo kwa nguvu zote.

Jitihada za gazeti hili kumpata Spika Makinda jana ili azungumzia msimamo wake huo wa kukimbia mjadala wa posho hazikuzaa matunda kutokana na simu yake ya mkononi mara kadhaa kuita bila kupokelewa na wakati mwingine, inakatwa.Taarifa zilizopatikana baadaye ofisini kwake zilieleza kuwa muda mwingi jana, Spika Makinda alikuwa na kikao.

Dk Kashililah

Kwa upande wake, Dk Kashililah jana aliamua kutua mzigo baada ya kukataa kuhusishwa tena na mjadala wa posho za wabunge unaoendelea nchini.

Dk Kashililah aliliambia gazeti hili kuwa kauli ya CCM kutaka nyongeza ya posho iondolewa kwa sababu maisha magumu, haimuhusu na yeye hana jipya kwenye mjadala huo.

“Hayo ya CCM hayanihusu… Unanionea tu ndugu yangu,” alisema Dk Kashililah alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu ushauri wa CCM uliotolewa juzi na Nape.

Kuhusu mgongano wa kauli yake na ile ya Spika Makinda kuhusu posho za wabunge, Dk Kashililah alisema" “Wewe ndio unasema (tulitofautiana).”

Wasomi, viongozi dini, wanaharakati

Wakati huo huo wasomi nchini wamesema suala la ongezeko la posho hizo kwa wabunge halijazingatia haki na usawa katika jamii hali itakayoweza kusababisha madhara makubwa katika ustawi wa uchumi na maendeleo ya jamii.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema wabunge waliopitisha kupanda kwa malipo ya posho zao katika vikao vyao, hawana machungu na maendeleo ya taifa, kwani wanachukua pesa nyingi kuliko wafanyakazi wa idara nyingine.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, (UDSM) Dk Benson Bana, alisema wabunge wote wanaotaka pesa zipande, hawana budi kuachia madaraka kwani wanalinyonya taifa.

Alisema wabunge wanatakiwa kufahamu kwamba Serikali ni masikini hivyo wanavyopitisha suala la kupata posho kubwa ni sawa na kuitia nchi umasikini.

“Hawa jamaa mimi siwaelewi kabisa unajua kitendo cha kupandishiwa posho kutoka Sh70,000 mpaka Sh200,000 ni sawa na kulitia umaskini taifa letu,”alisema Bana.
Dk Honest Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema sababu iliyotolewa kwamba posho hizo zimepanda kutokana na hali ngumu ya maisha, haina mashiko kwani ugumu wa maisha hauko mkoani Dodoma pekee.

“Kitendo cha kujiongezea posho kwa wabunge hao kimekuja baada ya kikundi cha watu wachache ambao ni watunga sera na sheria kukaa na kujadili namna ya kujipatia ahueni ya maisha na kuamua kujipandishia hizo posho bila kuangalia mwananchi wa kawaida ambaye ni mlipa kodi atakuwa anaishi katika hali gani,”alisema Dk Ngowi.

Profesa Robert Mabele wa Chuo Kikuu cha Dar e s Salaam, alisema kupanda kwa posho hizo kunamkandamiza mwananchi wa kawaida akiwamo mwalimu.
Alisema Bunge linatakiwa kuhakikisha kwamba mapato ya Mtanzania yanatakiwa kuwa na uwiano sawa na haya mabadikilo yanatakiwa kufanyika kwa watu wote sio kwa wabunge tu.Mhadhiri mwingine wa UDSM, Bashiru Ally alisema kupanda kwa posho za wabunge ni kukomaza utabaka kati ya walionacho na wasio nacho.

Msimamo wa Tucta
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi mkoa wa Mwanza (Tucta), Ramadhani Mwenda aliishutumu ofisi ya Bunge kwa kile alichoeleza kuwa imeonyesha dharau kwa Rais kwa kuongeza posho hizo bila idhini yake.

Alisema dharau ilionyeshwa na ofisi ya Bunge kwa Rais imekiuka misingi na sheria za nchi na kuonyesha kuwa kazi za Rais zinaweza kufanywa na mtu yeyote bila hata idhini yake.Mwenda alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Mkuu wa kitivo cha sheria kutoka Chuo Kikuu cha Makumira,Elfuraha Laltaika alipinga vikali ongezeko hilo kwa madai kuwa sababu zilizotolewa na Bunge hazikuwa na tija yoyote.

Laltaika, alisema ongezeko hilo ni kubwa, lakini sababu za kupanda gharama za maisha linawagusa watanzania wote na sio wabunge peke yao huku akisistiza kuwa kitendo hicho ni ubadhirifu mkubwa serikalini usiovumilika.


 
.....Huyu mama eti naye alipata nishani ya msanii JK!!!! Sijui kwa lipi la maana alilofanya kama spika wa Bunge.
 
Makinda alikiuka sheria kwa kuwalipa wabunge kabla sheria kusainiwa na Rais. Hana mamlaka ya kuzungumzia suala la posho kwa sasa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
.....Huyu mama eti naye alipata nishani ya msanii JK!!!! Sijui kwa lipi la maana alilofanya kama spika wa Bunge.

mkuu wangu inabidi tuombe Mungu hii miaka minne iishe haraka huyu mtu na watu wake waondoke
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mkuu wangu inabidi tuombe Mungu hii miaka minne iishe haraka huyu mtu na watu wake waondoke

Mkuu SI mimi naomba hiyo miaka minne isiishe maana kuna uwezekano mkubwa sana akaiacha nchi katika hali mbaya sana kwenye kila kitu.
 
Makinda alikiuka sheria kwa kuwalipa wabunge kabla sheria kusainiwa na Rais. Hana mamlaka ya kuzungumzia suala la posho kwa sasa

Mkuu G ndio utaona jinsi Serikali hii ilivyokuwa kichekesho maana maamuzi yanafanyika kienyejienyeji tu bila hata kufuata taratibu zilizowekwa. Je, atawajibishwa? Yule Jairo, Utoh, Ngeleja, Malima na Luhanjo hadi hii leo hawajawajibishwa na Mkuu wao wa kazi.
 
Mkuu G ndio utaona jinsi Serikali hii ilivyokuwa kichekesho maana maamuzi yanafanyika kienyejienyeji tu bila hata kufuata taratibu zilizowekwa. Je, atawajibishwa? Yule Jairo, Utoh, Ngeleja, Malima na Luhanjo hadi hii leo hawajawajibishwa na Mkuu wao wa kazi.

Wanajua Watanzania tunasahau mara moja. Sasa limezuka la posho la kina Jairo halizungumzwi. Sisi si wazima
 
Wanajua Watanzania tunasahau mara moja. Sasa limezuka la posho la kina Jairo halizungumzwi. Sisi si wazima

.....Ni kweli kabisa uyasemayo G. Rais anakwepa hata kukutana na waandishi wa habari ili kujibu maswali, anawaita "Wazee wa Dar" na kuwatuhubia kisaniisanii kwisha!!!! Ukimwambia akutane na waandishi wa habari wamuulize maswali anaingia mitini!!!!
 
Mlitegemea ahudhurie na aseme nini wakati kazi yake ni kulinda mafisadi waliomsimika hapo? Angesema nini kihiyo kama huyu ambaye anatumika kirahisi kusafisha nepi za mafisadi? Shame on you Makinda and your masters or mabwana waliokusimika hapo.
 
Back
Top Bottom