Makhirikhiri:Ni mfano wa kuigwa

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Hawa jamaa wa makhirikhiri ni mafano wa kuigwa, tunahitaji tuwe na vikundi vya sanaa za asili ambavyo vimejitangaza kimataifa ili waweze kupata mialiko ya nje kuutangaza utamaduni wetu kama hawa jamaa na utamaduni wao wa kibotswana. Wako wapi wakima Mwanzalima ambao wanaweza kuutangaza utamaduni wetu?. Serikali kupitia wizara ya elimu na utamaduni wana kazi kubwa ya kuhakikisha ngoma zetu za asili zinatumika kuutangaza utamaduni wetu pamoja na vivutio vya utalii wetu wa hapa nchini kimataifa.
 
Attachments

  • makhirikhiri-3.jpg
    makhirikhiri-3.jpg
    36.4 KB · Views: 54
  • makhirikhiri-4.jpg
    makhirikhiri-4.jpg
    27.3 KB · Views: 60
  • makhirikhiri-2.jpg
    makhirikhiri-2.jpg
    34.7 KB · Views: 60
Hawa jamaa wa makhirikhiri ni mafano wa kuigwa, tunahitaji tuwe na vikundi vya sanaa za asili ambavyo vimejitangaza kimataifa ili waweze kupata mialiko ya nje kuutangaza utamaduni wetu kama hawa jamaa na utamaduni wao wa kibotswana. Wako wapi wakima Mwanzalima ambao wanaweza kuutangaza utamaduni wetu?. Serikali kupitia wizara ya elimu na utamaduni wana kazi kubwa ya kuhakikisha ngoma zetu za asili zinatumika kuutangaza utamaduni wetu pamoja na vivutio vya utalii wetu wa hapa nchini kimataifa.

Hapo penye bold and coloured ndipo watanzania na baadhi ya waafrika tulipokosea na kupoteza mwelekeo. Utasikia kila kitu serikali itufanyie (Kuchimba choo, kuzoa takataka, au kuondoa jalala mahali fulani, n.k), rais njoo utusaidie, waziri mkuu sikia kilio chetu n.k, wakati mambo yakiendelea kuharibika na hata kuachwa nyuma wakati wenzetu wakipiga hatua. Hii kasumba imeenea mpaka hata kwa viongozi wa ngazi za juu wa nchi nyingi za kiafrika utasikia World bank tusaidie, G8 tekelezeni ahadi zenu za kutusaidia n.k.

Sasa kuanzisha kikundi cha ngoma ambacho kinajua kinataka nini, kinakwenda wapi, kiko well structured, kina dedication, kunahitaji serikali au wizara husika kuwakusanya watu na kuwapa hayo. Je Makhirikhiri walisaidiwa na serikali yao kufikia hapo?

Tafakari chukua hatua!
 
Back
Top Bottom