Makato kodi ya miamala haya hapa, kuanza kesho

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015

Makato kodi ya miamala haya hapa, kuanza kesho​

WEDNESDAY JULY 14 2021​

kodimiamalapic

Summary

  • Ni kodi ya uzalendo inayokusudia kufanikisha ujenzi wa barabara vijijini na uboreshaji wa huduma nyingine za jamii.

New Content Item (1)

By Julius Mnganga
More by this Author

Dar es Salaam. Licha ya Serikali kusisitiza utekelezaji wa tozo mpya ya miamala ya kwenye simu inayoanza kutozwa kuanzia kesho, wananchi wameonyesha wasiwasi kutokana na gharama mpya za kutuma au kutoa fedha.

Kuanzia kesho Alhamisi Julai 14, 2021, wanaotuma au kutoa fedha kwa wakala wa simu ya mkononi wataanza kulipia kodi ya uzalendo ambayo ni kati ya Sh10 na Sh10,000 kulingana na ukubwa wa muamala.

Kutokana na kodi hiyo mpya, wadau wana wasiwasi kwamba itapunguza matumizi ya huduma hiyo hivyo kushusha mchango wake kwenye uchumi.

Kwa gharama mpya zilizopo, wapo wanaoamini hakuna atakayeenda kwa wakala kufanya muamala.

Kabla ya kodi ya uzalendo, wateja wa Airtel Money walikuwa wanakatwa Sh350 tu ndani ya mtandao kutuma Sh15,000 lakini sasa watalipa Sh960 na walikuwa wanakatwa Sh550 kwenda mtandao mwingine lakini imepanda mpaka Sh1,160. Watakapotaka kutoa, watalipia Sh2,010 badala ya Sh1,400 ya mwanzo.

kodiairteli

Kwa wateja wa Mpesa, kutuma Sh15,000 kwenda kwa mteja asiyesajiliwa, makato yatakuwa Sh970 kutoka Sh360 wakati ikigharimu Sh2,820 kwa mteja asiyesajiliwa kutoka Sh2,210. Kwenda mitandao mingine, kiasi hicho kitalipiwa Sh1,160 kutoka Sh550 iliyokuwapo na watakaopelekwa kwenye akaunti zao za benki watakatwa Sh1,810 badala ya Sh1,200 iliyokuwapo. Kutoa kiasi hicho iwe kwa wakala au ATM, watakatwa Sh2,060 kutoka Sh1,450.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuendeleza Huduma za Fedha Tanzania (FSDT), Sosthenes Kewe anasema kwa kuwa miundombinu ya huduma hizi imeshawekwa na matumizi ya simu yamekuwa sehemu ya maisha ya wananchi, mabadiliko ya tabia za wateja ndio yatakayoamua uendelevu wa kodi hii mpya.

“Wapo wanaokopa au kuweka akiba kwenye simu zao. Wapo wanaolipia usafiri mfano Uber kwa simu zao. Adhima ya kuwa na uchumi wa kidijitali unataka watu wengi zaidi kutumia huduma za fedha. Ongezeko la gharama linaweza kuwarudisha watu kulipa kwa fedha taslimu,” anasema.

Kwa mabadiliko haya mapya, mteja wa miamala kwa simu ya mkononi atakuwa analipa kodi tatu. Kwanza ni ushuru wa forodha ambao ni asilimia mbili na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Hizi mbili zilikuwepo kabla ya mabadiliko yanayoanza leo.

kodimpyapicc

Kwenye makato ya Sh360 yalikuwapo kutuma Sh15,000 kwa mteja asiyesajiliwa, Vodacom ilikuwa inapata Sh289.1 na Serikali kukusanya Sh65 VAT na Sh5.9 ya ushuru wa forodha lakini kuanzia kesho Serikali itakuwa inaondoka na Sh680.9 ilhali Vodacom ikibakiwa na ileile.

Akizungumza kwenye kipindi cha 360 cha kituo cha runinga chaa Clouds, Julai 12, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alisema “hii sio tu ni kodi bali tunatunisha mfuko wa mshikamano. Tutachangia kupitia makato ya simu.”

kodipicctigo

Waziri huyo alisema itakuwa aibu kwa miradi ya maendeleo kukwama kwa kuwa tu Serikali imeshindwa kukusanya kodi hivyo akavitaka vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kodi kwa maendeleo yao.

“Kuna mambo hayapaswi kuwepo. Haitakiwi kuona kijiji hakina barabara inayopitika muda wote na tunabeba wagonjwa juujuu. Mbona tunaweza miito ya simu na kukatwa hela nyingi tu kwa nini isiwe kutunisha mfuko wa mshikamano?” alihoji Waziri Mwigulu.

Kutokana na vipeperushi vya makato mapya yatakayoanza usiku wa kumkia kesho, Boniface Mekuru amesema “Naenda kutoa salio lote nililonalo kabla ya kesho. Haya makato hayavumiliki. Nikikatwa Sh8,000 tu huwa naumia sasa haya mapya, siwezi kuyavumilia.”
 
Huu ni msumali wa moto kwenye vidonda vya waTanzania....

Hii ni dharau na kejeli kwa waTanzania........

Hii inaonyesha namna gani taifa hili linahitaji katiba mpya haraka iwezekanavyo........

Hii ni alama kuwa tuna watawala badala ya viongozi....

Mungu pamoja nasi waTanzania.......
 
Wamekosea sana, kodi mbili kwenye muamala mmoja haiwezekani, sio sawa hiki serikali walichofanya, hata kama wanataka kuboresha huduma za barabara lakini sio kwa kumkata mwananchi masikini anayehangaikia mahitaji yake mengi tofauti na wabunge na mawaziri.

Ule msemo wa tuma na salio la kutolea sasa naona unaenda kufa rasmi, kwasababu hicho kiasi cha kutolea pekee naweza mtumia mtu mwingine afanyie mambo yake, makampuni ya simu na serikali yenyewe wajiandae kupoteza wateja kwa hayo makato.
 
Na mkome!

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya kuongeza kodi pale bungeni mambo yalikuwa hivi hapa jf

Uzi wa bajeti ulikuwa na replays 90

Uzi wa Sabaya ulikuwa na replays elfu 1 na zaidi

Uzi wa kusaini petition ya kumtoa Mondi kwenye tuzo za bet ulikuwa na replays 800 na zaidi.

Kuleni upumbavu wenu. Najua hata hili mtapiga kelele siku 2 hizi alafu mnarudi kwenye ujinga wenu kama kawaida.
 
Hapa ndipo tulipofika
Kibaya ni WaTz kuona sawa tu
** Nini kifanyike
Vyama vya Upinzani huu ni wakati wa kutoa matamko
Kuwatetea wananchi maskini
*** Itisheni vyombo vya habari mlizungumze kwa SAUTI KUBWA NA KALI KUKEMEA UJAMBAZI HUU
Hawa watunga sheria hawana cha kupoteza mishahara yao mikubwa
Ni vipi mkulima mfanyabiashara atajikimu kwa wizi huu
Wenye biashara za miamala wanapoteza kazi mitaji etc
Endeleeni kuzalisha majambazi

Hii nchi ipo kwenye machela kuelekea makaburini

Hii sheria imepitishwa na nani kwa faida ya nani
Someone will pay the price siku moja
This is beyond unyama
 
Huu ni msumali wa moto kwenye vidonda vya waTanzania....

Hii ni dharau na kejeli kwa waTanzania........

Hii inaonyesha namna gani taifa hili linahitaji katiba mpya haraka iwezekanavyo........

Hii ni alama kuwa tuna watawala badala ya viongozi....

Mungu pamoja nasi waTanzania.......
ccm imekosa muelekeo kabisa
 
i cant beleive what i am reading, yaani hii serikali inajua vile maisha yamekuwa mangumu
 
Hapa ndipo tulipofika
Kibaya ni WaTz kuona sawa tu
** Nini kifanyike
Vyama vya Upinzani huu ni wakati wa kutoa matamko
Kuwatetea wananchi maskini
*** Itisheni vyombo vya habari mlizungumze kwa SAUTI KUBWA NA KALI KUKEMEA UJAMBAZI HUU
Hawa watunga sheria hawana cha kupoteza mishahara yao mikubwa
Ni vipi mkulima mfanyabiashara atajikimu kwa wizi huu
Wenye biashara za miamala wanapoteza kazi mitaji etc
Endeleeni kuzalisha majambazi

Hii nchi ipo kwenye machela kuelekea makaburini

Hii sheria imepitishwa na nani kwa faida ya nani
Someone will pay the price siku moja
This is beyond unyama
Hii sheria Imepitishwa na bunge lako tena kwa 100%. Pia hii ndio faida ya kuwepo chama kimoja bungeni kwasababu walisema wapinzani wanachelewesha maendeleo, hawana hoja, wanapinga kila kitu nk. Hivyo binfsi kwa hiki kinachoendelea me nimefurahi ili hapo mbeleni wananchi tuijue thamani ya uwepo wa upinzani bungeni na nchini kwa ujumla.

MITANO TENA KWA CCM.
 
Hizi mambo huwa sana announce wapi ili watz tuvote?
Ulipomvote in Bi Mkubwa, tambua ulivote package ya mambo mengi, likiwemo hili la makato. Mlisema mnamwelewa sana Bi Mkubwa, eti tuwaachie ndoa yenu. Au mlimaanisha yuleeeee ^Angelimako^ wa ^Ujeremani^!???
 
Na mkome!

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya kuongeza kodi pale bungeni mambo yalikuwa hivi hapa jf

Uzi wa bajeti ulikuwa na replays 90

Uzi wa Sabaya ulikuwa na replays elfu 1 na zaidi

Uzi wa kusaini petition ya kumtoa Mondi kwenye tuzo za bet ulikuwa na replays 800 na zaidi.

Kuleni upumbavu wenu. Najua hata hili mtapiga kelele siku 2 hizi alafu mnarudi kwenye ujinga wenu kama kawaida.
Kumbe Jeiefu ndio walipewa kazi ya kubalansi makato yetu, wao wakawa wamejikita kwenye mambo yao!??? Sasa nimewaelewa vizuri wabaya wetu. Dah!!!
 
Huu ni msumali wa moto kwenye vidonda vya waTanzania....

Hii ni dharau na kejeli kwa waTanzania........

Hii inaonyesha namna gani taifa hili linahitaji katiba mpya haraka iwezekanavyo........

Hii ni alama kuwa tuna watawala badala ya viongozi....

Mungu pamoja nasi waTanzania.......
Kwahiyo katiba mpya ndiyo itakuja kukulipia hii miamala?

Acha kufuata mkumbo kila kitu katiba mpya
 
Lengo la serikali ya Bi Mkubwa ni kuwalinda wafanyabiashara wakubwa; ndiyo hata mantiki ya kuwatimua hovyo machinga.
Heheheh kuwalinda in expense ya wafanyabiashara wadogo ndio ambacho nakiona! Anyways ni sawa tu sababu si mlimtukana sana jembe ooh anachukia matajiri ila msijue kuwa hao wafanyabiashara matajiri ndio wanakuwa favored sana kwenye kodi!

Wao kutokulipa kodi ni kama tusi kwa serikali ila mlimuona mzee yule ni mwehu! Ila alikuwa na mantiki sana ntakupa mfano mdogo tu, tajiri kama Mo kuingiza malori 5 mapya anasamehewa kodi ya kuingiza ila mjasiriamali anaenunua moja atalipishwa kodi which is not fair, tulitegemea tajiri alipishwe kodi sababu ana uwezo ila mwenye mtaji mdogo ndio analipishwa kodi!

Tuendelee na bibie sasa, kazi ndio kwanza imeanza! Anafungua nchi sasa
 
Back
Top Bottom