Makapuku Forum

"Kifo chake [hayati Bernard Membe] kimeacha pengo kubwa sio tu katika familia yake, bali kwa taifa la Tanzania na mataifa aliyoyafanyia kazi katika kulinda utu na heshima ya mtu." - Rais Samia Suluhu Hassan
Screenshot_20230514_150852.jpg
 
Happy Mother's Day to all those mothers who are here. Channel change after working on my English a bit, in the words of hekima za mfalme Seleman na jaji kanjanja Azdak juu ya hukumu ya yaya ambaye alikuja kuwa ni mama bora kwa mtoto kumzidi mama wa kibaiolojia tajiri.

Point hapa: Mama sio lazima uwe umenizaa bali mama ni matendo ambayo unayafanya na kukustahilisha kuwa mama.

Kama unaye anayekuita mama bila kujali jua leo ni siku nzuri kwako na Happy Mother's Day kwa wote mliopo kwenye jukwaa hili adhimu.

Note: Jaji kanjanja anapatikana kwenye kitabu cha The Caucasian Chalk Circle kimeandikwa na Bretch B.
Nimekifanyia mtihani miaka 20 iliyopita (bragging mode activated)
 
Happy Mother's Day to all those mothers who are here. Channel change after working on my English a bit, in the words of hekima za mfalme Seleman na jaji kanjanja Azdak juu ya hukumu ya yaya ambaye alikuja kuwa ni mama bora kwa mtoto kumzidi mama wa kibaiolojia tajiri.

Point hapa: Mama sio lazima uwe umenizaa bali mama ni matendo ambayo unayafanya na kukustahilisha kuwa mama.

Kama unaye anayekuita mama bila kujali jua leo ni siku nzuri kwako na Happy Mother's Day kwa wote mliopo kwenye jukwaa hili adhimu.

Note: Jaji kanjanja anapatikana kwenye kitabu cha The Caucasian Chalk Circle kimeandikwa na Bretch B.
Nimekifanyia mtihani miaka 20 iliyopita (bragging mode activated)
Asante sana binamu
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu ametoa taarifa kuhusu tetesi za uwepo wa mlipuko mpya wa Covid 19 Tanzania ambapo amewaomba Wananchi waondoe hofu na kusema Wizara ya Afya inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii kisha watatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au lah!

Ummy amesema “Kwa taarifa za Wagonjwa waliopimwa virusi vya Covid-19 wiki ya kuanzia May 6 - 12, 2023, Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya April 29 hadi May 05,2023, hakuna kifo chochote kilichothibitishwa kusababishwa na Covid-19”

“Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili, nawaomba Wananchi muendelee kuzingatia kanuni za afya na usafi”
Screenshot_20230515_044805.jpg
 
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tayari ameuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, Karimjee Dar es salaam.

Kwenye swipe kuna picha za Viongozi wengine wakiwa kwenye kuuaga mwili wa Membe akiwemo Waziri Nape, Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe na aliyekuwa RC wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Screenshot_20230515_044944.jpg
Screenshot_20230515_045005.jpg
 
Muuguzi wa Hospital ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Wilson Fungameza ameibuka mshindi wa tano kati ya washiriki 52,000 katika shindano la wauguzi bora wa dunia lililoratibiwa na Aster Guardian Global Nursing Award jijini London.

Shindano hilo lilihusisha washiriki kutoka nchi 202.
Screenshot_20230515_045209.jpg
 
Rais wa Kenya, William Ruto na kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga wamekutana leo kwa mara ya pili ndani ya wiki moja na kupeana mikono licha ya kuwepo kwa mvutano wa kisiasa nchini humo unaosababisha maandamano yanayoongozwa na Odinga ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha.

Jana walikutana kwenye hafla ya kuaga mwili wa mpigania uhuru wa Kenya, Mukami Kimathi na leo wamekutana katika uwanja wa Nyayo wakati wa mechi ya ‘Mashemeji Derby’ inayokutanisha timu za Gor Mahia na AFC Leopards.

Katika mechi hiyo AFC Leopards ambayo pia mlezi wake ni Rais William Ruto iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Screenshot_20230515_045508.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi (mwenye ushungi wa njano), Zainabu Telack akipata maelezo kutoka kwa wajenzi wa kaburi atakalozikwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe katika makaburi ya Kanisa Katoliki Kijiji cha Rondo Kata ya Chiponda.

Mwili wa Membe utazikwa Jumanne Mei 16, 2023 kijijini hapo.

Membe alifikwa na mauti asubuhi ya Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua ghafla.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari mbalimbali kutoka Rondo mkoani Lindi.

Screenshot_20230515_045728.jpg
 
UKIMUELEWA DI CANIO HUWEZI KUMUELEWA CHAMA, UKIMUELEWA ZIDANE UTAMUELEWA CHAMA
.
Euro 2020 pale Romania kwenye dimba la National Arena, Bucharest beki wa Ujerumani Antonio Ruddiger alimnyata mgongo kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, lakini mpira ulivyoisha alienda kumuomba radhi!! Yes ulikuwa ni uungwana tu, Pogba akuumia kiasi cha kushindwa kuendelea kucheza ila Ruddiger aliamua kukumbuka FOOTBALL IS FAIR PLAY.
.
Uefa Champions League 2015 kule Uholanzi, dunia ilishuhudia rafu mbaya kwenye soka baada ya Hector Moreno wa PSV kupiga brashi kali mpaka mguu wa beki wa Utd Luke Shaw ukavunjika!! Lakini alimfuata palepale uwanjani na kumpa pole ila inasemekana pia alifika mpaka hospitali kumtembelea mchezaji mwenzake!! Yes ni uungwana tu.
.
Msimu huu pia tulishuhudia FAIR PLAY nyingine baada ya beki wa Southampton Kyle Walker Peters kumuumiza kinda Allejandro Garnacho, alimtumia ujumbe wa pole na kumtaka radhi lakini hii FAIR PLAY sio sheria ni ubinadamu tu ambao mtu anakuwa nao.
.
Mwaka 2006 kwenye fainali ya World Cup kule Ujerumani Zinadine Zidane alimpiga kichwa Marco Matterazi wa Italia ila wanadai wakati mchezo unaendelea Zizzou alimwambia Marco asiivutevute jezi yake mpira ukiisha atampatia, kwa jeuri Matterazi akamjibu hataki hio jezi bali anamtaka dadaake Zidane kilipigwa kichwa kizito na sikumbuki kama kuna FAIR PLAY iliyotolewa.
Screenshot_20230515_050028.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom