Makanisa yafanye ibada siku ya Jumamosi tarehe 24 Oktoba badala ya 25 Oktoba

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Kutokana na uchaguzi mkuu wa Rais, Ubunge na Madiwani kutarajiwa kufanyika siku ya tarehe 25/10/2015 ambayo ni siku ya jumapili .

Ni busara makanisa kama inawezekana wakubaliane kufanya ibada siku ya Jumamosi ya tarehe 24/10/2015 ili kuwapa waumini wao nafasi ya kupiga kura kwa ufasaha siku ya Jumapili ya tarehe 25/10/2015.

Kwa Mungu nadhani siku zote ni sawa mbele zake kufanya ibada.

Ni mtazamo wangu tu.
 
Uchaguzi hauwezi kubadilisha ratiba ya siku ya Ibada, labda wabadilisha saa au wafanye Ibada fupi.
 
Haitawezekana ya Mungu mpeni Mungu ya kaisari apewe kaisari watu watapiga kura usijali kuna misa za asubui na mchana usijali
 
yaani kubadili siku ya bwana kisa uchaguzi thubutu.uchaguzi wenyewe hauna lolote maana wagombea wote ni mafisadi si lowasa wala magufuri wote wanatafuta kura ili wale tu
 
sisi hatufungwi na wakati tunaweza fanya tu ibada jumamosi na hata ijumaa
 
Kwan tume ingepanga siku ya katkati ya wiki ingepata hasara gani? Elewa kuwa wakristo ulalamika kwann tume inapenda kuvuruga ibada zao
 
uzi wako hauna mashiko..mfano sisi wakatoliki tuna MISA kila siku jumatatu mpaka jumatatu ila jumapili ni DOMINICA....haiwezi kuwa siku tofauti....ila baraka ni zile zile.... kwani ukienda misa ya kwanza saa moja asubuhi ukatoka saa3 asubuhi.....kinazuia nini kwenda kupiga kura!!!!!!! nimepiga kura chaguzi 4 na sijaona shida.....
 
kwani umeambiwa watu watashindwa kupiga kura sababu ya kwenda kanisani
 
Umeambiwa makanisa yanafuata muandamo wa mwezi? Makanisa yanafuata maandiko, c mpango wa binadamu
 

150908090236_catholic_church_512x288_getty.jpg

Kanisa katoliki limeruhusu viongozi kutekeleza ibada jumamosi

Wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa kwa Tanzania kufanya uchaguzi mkuu, baadhi ya makanisa nchini Tanzania yametoa ruhusa maalum kwa viongozi

wa kanisa kuendesha ibada zao Jumamosi tarehe 24 ya mwezi huu wa Oktoba 24 2015 badala ya Jumapili tarehe 25 ili kutoa nafasi kwa waumini wao kushiriki shughuli kubwa ya upigaji kura.

Makamu wa rais wa Baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amesema kuwa ibada haipaswi kuzuia haki ya kimsingi na kikatiba ya waumini .

"Si utaratibu wa kawaida kwa sababu kama baraza hatujakaa, lakini kila askofu anawajibika ndani ya

jimbo lake, hivyo anaweza kutoa fursa hiyo.
"Hata mimi katika jimbo langu la Rulenge Ngara, nimetoa kibali hicho kwa makanisa yote'' amenukuliwa akisema Askofu Severin.
150706095821_china_bible_512x288_afp_nocredit.jpg


Severin Niwemugizi, amesema kuwa ibada haipaswi kuzuia haki ya kimsingi na kikatiba ya wauminiHadi sasa tangu nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1961 imeongozwa na marais wanne wa kwanza akiwa

baba wa taifa hilo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akafuatiwa na Al Haji Hassan Mwinyi, baadaye Benjamin William Mkapa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anayeelekea kukamilisha muhula wake wa pili atatoa nafasi kwa rais wa tano kuchukua madaraka mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.

Makanisa kufanya ibada jumamosi tarehe 24 - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom