Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
any body can be a vice president so long is hailing from tannzania island. this is not a big issue so long there are more than one million in isles he/she can be picked easily.
Yaleyale ya ku-simplify serious issues na kuzifanys sio big issued. Anybody anaweza kuwa vice-president maana yake nini? Watanzania wanahitaji kupata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri Kiongozi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa watakaoweza kuleta mbadiliko na kuiletea nchi yetu maendeleo. Tukisema it is not a big issue yoyote tu anaweza kuwa picked ni kutoitakia mema Tanzania. Hivi tutaendelea mpaka lini kuchagua watu maradi wanajitokeza kugombea uongozi badala ya kutafuta ama kuchagua watu makini wenye uwezo wa kuinyanya nchi hii na kuirejesha pale ilipostahili kuwa?
Kila siku watu wamekuwa wakirudiarudia kulitaja jina la Salim katika safu ya uongozi wa ngazi ya juu wa Taifa letu kwa sababu alionyesha uwezo mkubwa wa uongozi na angaliweza kuliongoza taifa hili kwa ufanisi mkubwa. Watu kama marehemu Mwalimu Nyerere , Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine wataendelea kutajwa hadi na vizazi vijavyo kwa sababu ya uongozi wao bora. Siamini kwamba watu kama hawa tunaowachagua kwa kuangalia sura zao ama kwa kuona kwamba it is not a big issue kuwachagua wataweza kukumbukwa na yoyote zaidi ya marafiki zao pale watakapomaliza uongozi wao. Ni pale tu watakapojirekebisha na kuiga yaliyokuwa yakiwaletea sifa viongozi niliowataja hapo ndio hukumu ya wananchi inaweza ikabadilika kwao na wakaweza kukumbukwa siku za usoni.