Makampuni ya Kenya yanavyokwepa kodi Tanzania

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
1,948
1,237
Salamu wakuu,

Nimeona niandike huu uzi leo kwa manufaa ya serikali mpya, mamlaka mpya ya TRA na wananchi wa Tanzania kwa ujumla. Nitahadharishe kwamba ninachokiandika ninakifahamu vema na si mambo ya kusikia sikia.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa asilimia 70 ya makampuni ya Kenya yenye makampuni toto (subsidiaries) nchini Tanzania yanakwepa kodi mbali mbali zikiongozwa na kodi inayotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi wake waliojiriwa Kenya lakini wakiwa wanafanya kazi nchini Tanzania.

Ukwepaji huu hufanyika kwa njia ya mishahara ya wafanyakazi hawa ambao wengi ni wa nafasi za juu (executives) kulipiwa huko Kenya na hivyo kutolipa kodi ya mapato huku Tanzania. Kinachoshangaza ni kwamba jambo hili limeruhusiwa na TRA kuendelea kutokea kwa miaka zaidi ya 9 ya uchunguzi wangu hadi sasa.

Ninamshauri Kamishna mkuu kufuatilia kampuni hizi. Mpaka sasa kampuni ninazozifahamu zenye wafanyakazi hawa wasiolipa kodi ziko kwenye sekta za mafuta, usafirishaji mafuta, kilimo, usambazaji bidhaa zilizozalishwa Kenya n.k. Kama nilivyotangulia kusema ninafahamu vyema ninalolisema kwa sababu nimehusika moja kwa moja makampuni haya kwa ukaribu ulioniwezesha kuyaona haya kwa undani.

Wakati umefika kwa hawa jirani zetu kuacha kutucheza shere na sisi tuijenge nchi yetu kwa kukusanya kodi stahiki kutoka kwa kila mmoja anayestahili kulipa.

Nawasilisha,

Prisoner 46664.

ukweli kuwa kampuni karibu zote zinakwepa kodi,hata ambazo zinalipa kodi na hazilipi ipaswavyo,magufuli ana kazi kubwa sana kwa sababu nyuma yake hakuna wenye nia kama yake,
wapiga dili wa serikali ya kikwete bado wameshikilia nafasi zile zile za kupigia dili,wanachofanya ni style tu ya kupiga inabadilika
 
Salamu wakuu,

Nimeona niandike huu uzi leo kwa manufaa ya serikali mpya, mamlaka mpya ya TRA na wananchi wa Tanzania kwa ujumla. Nitahadharishe kwamba ninachokiandika ninakifahamu vema na si mambo ya kusikia sikia.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa asilimia 70 ya makampuni ya Kenya yenye makampuni toto (subsidiaries) nchini Tanzania yanakwepa kodi mbali mbali zikiongozwa na kodi inayotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi wake waliojiriwa Kenya lakini wakiwa wanafanya kazi nchini Tanzania.

Ukwepaji huu hufanyika kwa njia ya mishahara ya wafanyakazi hawa ambao wengi ni wa nafasi za juu (executives) kulipiwa huko Kenya na hivyo kutolipa kodi ya mapato huku Tanzania. Kinachoshangaza ni kwamba jambo hili limeruhusiwa na TRA kuendelea kutokea kwa miaka zaidi ya 9 ya uchunguzi wangu hadi sasa.

Ninamshauri Kamishna mkuu kufuatilia kampuni hizi. Mpaka sasa kampuni ninazozifahamu zenye wafanyakazi hawa wasiolipa kodi ziko kwenye sekta za mafuta, usafirishaji mafuta, kilimo, usambazaji bidhaa zilizozalishwa Kenya n.k. Kama nilivyotangulia kusema ninafahamu vyema ninalolisema kwa sababu nimehusika moja kwa moja makampuni haya kwa ukaribu ulioniwezesha kuyaona haya kwa undani.

Wakati umefika kwa hawa jirani zetu kuacha kutucheza shere na sisi tuijenge nchi yetu kwa kukusanya kodi stahiki kutoka kwa kila mmoja anayestahili kulipa.

Nawasilisha,

Prisoner 46664.

Sio hao tu mkuu. Ata nduguzetu wa bara Asia wanahili jipu
 
kuna faida gani mtu akijiiita muwekezaji lakini anakwepa kodi, sisi tunafaidika nini sasa? kama hili alilosema mdau sio visa na vitina tu, naomba TRA wafuatilie mara moja na watu watolewe mfano kwa kutumbuliwa majipu. mambo mengine ambayo hata huwezi kuyafanya nchi nyingine hapa tz unaweza kufanya tu kwasababu serikali zetu zilikuwa zimelala sana.shamba la bibi.
 
kampun nying zilijiingiza ktk mkumbo wa kukwepa kodi kwa sababu ilikua ndio ada kila mtu ana kwepa kodi, nadhan ile nidham na structure ziwekwe kurudisha iman kila mtu alipe kodi wakisema wafuatiliwe utakuta almost kampun zote hazilip
 
Hivi mtu kama mshahara wake unatoka huko kenya unamkataje huku kwetu kodi? inamaana kule kenya anakuwa nako hajalipia kodi au ikoje hii
 
Mkuu,

Mtu mwenye mkataba wa kufanya kazi Tanzania anao wajibu wa kulipa kodi Tanzania. Mtanzania akifanya kazi Kenya vivyo hivyo.
 
Hivi mtu kama mshahara wake unatoka huko kenya unamkataje huku kwetu kodi? inamaana kule kenya anakuwa nako hajalipia kodi au ikoje hii

Usemacho ni kweli mkuu,

Kuna kampuni moja kati ya hizo zilizotajwa hapo - niliiona ilipoanza biashara hapa Dar mwaka 2012 na wakaanza moja kwa moja na huu ukwepaji kodi as if ni kitu ambacho tayari wamejifunza kwa kampuni nyingine
 
kwani humu ndani huwa hakuna wafanyakazi wa serikali wanaoweza kutupatia majibu, au wanafuatilia halafu wanaenda kushughulikia kutumbua majipu kimya kimya?jf ni kitu kilicholeta mabadiliko makubwa sana katika siasa za tz.
 
Uko sahihi mkuu..kuna haja ya TRA kutuhabarisha kuhusu kinachoendelea hapa.
 
kwani humu ndani huwa hakuna wafanyakazi wa serikali wanaoweza kutupatia majibu, au wanafuatilia halafu wanaenda kushughulikia kutumbua majipu kimya kimya?jf ni kitu kilicholeta mabadiliko makubwa sana katika siasa za tz.

Nadhani uongozi wa JF unaweza kuchukua maswali nyeti yanayohitaji majibu na kuyawasilisha sehemu husika ili mrejesho au ufafanuzi utolewe.
 
Hichi ni kichaka. ..Hata kampuni za Aviation, Tour Companies etc. ...

Magu atakapogusa viongozi wa mikoani hakika kutakuwa na dalili njema ya majipu kutumbuka. ..
Hizi ngazi za chini zinakwamisha kasi ya Magu. ..
 
Dah! Hata sielewi.Sasa mtu ni mkenya.Familia yake ipo kenya,kila kitu ni kenya hiyo hela itarudije huku ili iweze kukatwa kodi na kurudishwa kenya?
 
Hichi ni kichaka. ..Hata kampuni za Aviation, Tour Companies etc. ...

Magu atakapogusa viongozi wa mikoani hakika kutakuwa na dalili njema ya majipu kutumbuka. ..
Hizi ngazi za chini zinakwamisha kasi ya Magu. ..

Kibaya kuliko vyote hawa mabwana wamefanya hii kuwa ni kawaida kwao..kwa hivyo kila kampuni mpya inayotokea Kenya inakuja na kuanza huu ukwepaji kodi mara moja
 
Back
Top Bottom