Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 525
- 1,816
Kuanzia TSMC, SAMSUNG, PANASONIC, HONDA na LG wameonyeshwa kutoridhishwa na sera za Marekani za uwekezaji.
Tuanze na makampuni ya kutoka nje yaliyoonyesha nia kuwekeza katika sekta ya utengenezaji chips (semiconductors)
●TSMC
Hii ni kampuni ya kutengeneza chips (semiconductor) ambayo makao yake makuu ni Taiwan, ilianza kujenga kiwanda Arizona Marekani. Ila ujenzi unasuasua sana kutokana changamoto mbalimbali mojawapo ni serikali ya Marekani kutolipa ruzuku.
●SAMSUNG
Samsung walijenga kiwanda cha kutengeneza chips kilichopo Texas, ambacho kingeanza uzalishaji mwaka 2024. Hata hivyo wamesimamisha mpango wa kuanza kutengeneza chips. Moja ya changamoto ni ucheleweshwaji wa ruzuku kutoka serikali ya Marekani na vibali kutoka kwa wenye mamlaka.
Kwenye sekta ya magari ya umeme, mojawapo ya hitaji muhimu ni betri za magari hayo. Hivi karibuni serikali ya Marekani ilipunguza ruzuku kwenye sekta ya magari ya umeme.
Mabadiliko ya sera hiyo imefanya makampuni ya Honda, Panasonic na LG kusitisha uwekezaji wa kutengeneza betri za magari ya umeme nchini Marekani.
●HONDA
Kampuni ya Honda kutoka Japan walikuwa waingie ubia na kampuni ya kutengeneza magari ya Marekani ya GM kutengeneza betri za magari ya umeme. Mwezi Oktoba mwaka huu walitangaza kujitoa kwenye mradi huo.
●PANASONIC
Kampuni hii ya Japan wamesitisha mpango wa kujenga kiwanda cha betri walichopanga kujenga mjini Oklahoma, Marekani.
●LG
Hii ni kampuni ya Korea Kusini nayo imefuata hatua zilichokuliwa na Panasonic na Honda, imesimamisha mpango wake wa kushirikiana na kampuni kubwa ya utengenezaji magari ya Marekani ya Ford kujenga kiwanda cha betri za magari ya umeme mjini Kentucky, Marekani.
Mwanadiplomasia nguli na maarufu Mmarekani Henry Kissinger ambaye aliwahi pia kuwa Waziri wa Mambo ya nje ya Marekani aliyekufa Nov 29, 2023, aliwahi kunukuliwa akisema: "To be an enemy of the US is dangerous, but to be a friend is fatal."