Makamba: Waislamu, nafasi za kazi hazigawanywi kama Njugu, someni!!

Status
Not open for further replies.

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Katibu mkuu mstaafu wa CCM Yusuph Makamba amewaasa waislamu kusomesha watoto elimu akhera na Dunia, ili waweze kuajiriwa na serikali ktk nafasi mbalimbali.

Amesema kuwa anashangaa Waislamu wakidai kuwa Serikali inawapendelea Wakristo huku wao (Waislamu) wengi wakiwa hawana elimu na kwamba nafasi za kazi haziwezi kugawanywa kama njugu hivyo ni lazima sasa waislamu wahakikishe wanasomesha watoto wao ili waweze kuwa na elimu ya kuweza kuajiriwa.

Source; Radio Free Afrika tuzungumze magazeti.
 
Katibu mkuu mstaafu wa Ccm Yusuph Makamba amewaasa waislamu kusomesha watoto elimu akhera na Dunia,ili waweze kuajiriwa na serikali ktk nafasi mbalimbali.
Amesema kuwa anashangaa Waislamu wakidai kuwa Serikali inawapendelea Wakristo huku wao (Waislamu)wengi wakiwa hawana elimu na kwamba nafasi za kazi haziwezi kugawanywa kama njugu hivyo ni lazima sasa waislamu wahakikishe wanasomesha watoto wao ili waweze kuwa na elimu ya kuweza kuajiriwa.

Source; Radio Free Afrika tuzungumze magazeti.

Watakataa tu kusema na yeye nikibaraka ilhali anawapa chanjo ya gonjwa lao!
 
Taja vyuo vinavyomilikiwa na wakristo au waislamu?

Ataje ili iweje? Wewe si umesoma kuwa Makamba anasema kuwa Waislamu waache kudai serikali inawapendelea Wakristo ili na badala yake wasomeshe watoto elimu dunia na sio elimu ahera pekee! Sasa swala la vyiuo hapa linatoka wapi?
 
Tulikuwa tunaelekea kusahau hizi mada za waislamu/wakristo, lakini wakereketwa wa udini mnaanza kuzileta tena. Mods, plz fanyeni kazi yenu hima, toeni uchafu huu
 
Ukweli mtupu,hakuna miujiza katika hilo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
At least huu sio uchochezi. Ni kitu ambacho kinaweza kutusaidia sote. Tusisistize elimu kwa watoto badala ya kupandikiza chuki na dhana kuwa wanaonewa. Kila mtu anavuna alichopanda.
Tulikuwa tunaelekea kusahau hizi mada za waislamu/wakristo, lakini wakereketwa wa udini mnaanza kuzileta tena. Mods, plz fanyeni kazi yenu hima, toeni uchafu huu
 
Wasome wasisome linakuhusu nini..Acheni mada za udini kwa mitandao ya kijamii..magazeti ni yanatafuta njia ya kutokea kimauzo
 
Tulikuwa tunaelekea kusahau hizi mada za waislamu/wakristo, lakini wakereketwa wa udini mnaanza kuzileta tena. Mods, plz fanyeni kazi yenu hima, toeni uchafu huu

Zinedine,

Acha uvivu wa kufikri bana!
Hakuna swala la udini au ukabila. Hapa Makamba wa Chama cha Magamba amewapa 'makavu live' Waislamu.
Alichosema Makamba ni ukweli mtupu na lazima Waislamu wote wasikie na waelewe hivo. Kwamba ni upuuzi kukaa na kulalamika ati Wakristo wanapendelewa kwenye nafasi za uongozi serikalini ilhali huna sifa(Qualifications) za kuomba na kuipewa hiyo nafasi!!!

Someni kwa bidii kwenye shule zinazofundisha Elimu Dunia! Lakini kama mtaendelea kung'ang'ania shule za MADRAS na kushinda misikitini hamuwezi kupata Nafasi za uongozi ngazi yoyote kwa vile Vyeo/Nafasi serikalini hazigawiwi kama SADAKA!!!

Saafi sana Makamba wa Magamba.
 
Tulikuwa tunaelekea kusahau hizi mada za waislamu/wakristo, lakini wakereketwa wa udini mnaanza kuzileta tena. Mods, plz fanyeni kazi yenu hima, toeni uchafu huu

Wewe sasa ndio unaeleta Udini! Kama huna cha kukoment kaa kimya sio lazima utafute watu wakubaliane na mtazamo wako.
Kwani wapi umeona Uislamu au Ukristo umekashifiwa!? Makamba kawaeleza Waislamu ukweli na kuwashauri kuwasomesha watoto shule wapate elimu Akhera na Dunia,ili waweze kuajiriwa na serikali pale inapo tokea Fursa na wasibaki tu kulalamika kuwa Wakristo wanapendelewa kitu ambacho sio kweli!
 
Makamba aseme waislam hawakusoma kipindi kipi?
Pia ataje ratio ya hao waislam wachache ambao wamesoma ndio ratio ya waislam kwenye ajira?
Yusuf makamba ndo mana waislam wanamwita joseph makamba kutokana na huu ujinga wake wa kuwakebehi waislam.
Hii takwimu makamba kaitoa wapi?
Mbona waislam walivyotaka kuweka hiki kipengele katika sensa wakristo na serikali yao walipinga.
Makamba acha kuwakebehi waislam, hii dunia tunapita tu!
kumbuka ipo siku utakufa na utahukumiwa kutokana na huu upuuzi unaofanya.
Makamba mbona hajasema kuwa NECTA ndio machinjio makuu ya waislam!
 
Ndio maana tunaomba mahakama ya kadhi ili nasisi tupate ajira ya kutandika viboko, kuwapiga mawe na kunyonga watu. Hii itatusaidia kuongeza obwe la ajira hapa Tanzania.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Wasome wasisome linakuhusu nini..Acheni mada za udini kwa mitandao ya kijamii..magazeti ni yanatafuta njia ya kutokea kimauzo

Kamuambie baba yako Makamba haya unayoyasema! Mimi nimeandika tu nilichokisikia. Ikiwa unaona kuna kosa ktk Ushauri huu wa Makamba basi ni vema ukaeleza kuwa kosa ni lipi na sio kulalamika.

Binafsi naona kuwa Ushauri wa Makamba ni wa Msingi na ni changamoto ikiwa Waislamu wanataka kupata ajira Serikalini na ktk taasisi za mashirika na watu binafsi. Duniani kote sasa ajira hupatikana kwa Profesianal na sio kwa uzoefu,.Hatusemi watu waache kusoma elimu ya Akhera hapana! Ila wasome elimu akhera na dunia. Makamba yupo sahihi kwa waelewa ila kwa wasioelewa kama wewe Kaaazi kwelikweli!!
 
Ndio maana tunaomba mahakama ya kadhi ili nasisi tupate ajira ya kutandika viboko, kuwapiga mawe na kunyonga watu. Hii itatusaidia kuongeza obwe la ajira hapa Tanzania.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Ironic statement? au kutoka moyoni?
 
Nadhani makamba ameenza kuchanganyikiwa akili.

Hujuma ziko wazi! Na hata akina Ndalichako walikili! huyo makamba anaongea kwa ushahidi upi?
Mara ngapi misaada mikubwa imepelekwa Kwenye mashule na vyuo vinavyomilikiwa na kanisa KUPITIA makubaliano Haramu ya MOU? Hii ni kwa faida ya nani? na maslahi ya nani? watu wakihoji mnasema udini na uchochezi! acheni mambo yenu bwana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom