MAKAMBA vs SHY-ROSE UVCCM Dodoma, Kulikoni?

1st Shyrose is no more kijana she's 42yrs old so the topic bogus

2nd CCM doesnot hold the future of this country, the future is withing the heart and hand of every Tanzanian. Those are old, stupid and dirty political slogans.
 
Kwani hakuna ukomo wa ujana maana me sielewielewi vile maana shyrose bado tuu ni kijana???????????? Me naona mniache niendelee kula ugali hapa na kuku
 
Kwani hakuna ukomo wa ujana maana me sielewielewi vile maana shyrose bado tuu ni kijana???????????? Me naona mniache niendelee kula ugali hapa na kuku

Kwa taarifa ni kwamba Makamba, Shy-Rose na DC wa Bunda Francis Isaac, wote wamepita umri wa kuwa wanachama wa UVCCM lakini ni wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM kutoka UWT (Shy-Rose), Wazazi (Francis) na Makamba anaingia kama Katibu Mkuu katika baraza kuu la UVCCM, UWT na Wazazi.

Kwa Shy-Rose kumkosoa Makamba hakuwa peke yake hata Ridhiwani Kikwete naye alimkosoa, lakini Makamba akaona mnyonge wake ni Shy-Rose aambaye alimtukana bila sababu na alipotakiwa kuacha jazba, alijitetea na kusema, "I am human being" akiwa na maana kwamba na yeye ana roho na hivyo ameumia. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni, Shy-Rose katika hili amesema kweli na kila siku humu JF munajadili na kusema Makamba aondoke maana amechoka na wana CCM wakiwamo Vijana wamesema huyu mzee ni mzigo kwa CCM naamini hata yeye anajua ila anasubiri astaafu na si kujiuzulu.
 
lakini huyo bi mkubwa kazidi nae! anajifanya kazaliwa kuwa kiongooozi! ukitaka kuamini hilo akaona ajiingize CHANETA kwa sababu hakuna ushindani wa kutosha! amekutana na mwehu mwenzie acha watiane adabu!
 
Kweli tupu EL ako nyuma ya pazia mkuu.

Magige anafanya kwa niaba ya controller wa CCM mkoa wa arusha EL coz yeye ndo anapanga safu za uongozi na ukiwa mtiifu kwake utakula mema ya nchi, na magige anatimiza wajibu.

EL ndo alifanikisha Batilda kupita kura za maoni, James Milya kuwa m/kit wa UV ccm mkoa ars, Nembrisi kimbele kuwa kiongozi UWT na hata ubunge wa viti maalum wa Namalek Sokoine kataftiwa na EL ili asipeleke ushindani monduli na wale wabishi kwa matakwa ya EL huwajibishwa mfano ni ktk uchaguzi wa CCM ktk nafasi ya m/kiti CCM mkoa na jumuiya ya wazazi lekule laizer na elisa mollel walitoswa live kwa msaada wa takukuru, so since hapo uongozi wa CCM Arusha ni watiifu kwa ELna sio hao tu hata viongozi wa dini ka askofu Laizer so lolote utakalo sikia toka kwa uongozi wa CCM Arusha ni kwa amri ya EL na wako kumlinda yeye na ni sababu ya njaa zao na uchu wa madaraka.

Hence hili la Magige ni EL at work am sure asilimia mia moja
 
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Dar es Salaam katika kikao chake kilichofanyika jijini leo April 2, 2011, wamemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kujiuzulu kwenye nafasi hiyo kwa kuwa mzigo kwa chama tawala.

Kikao hicho kimefanyika kwenye ofisi kuu ya CCMn ya wilaya ya Kinondoni.

Wajumbe hao wa UVCCM Dar es Salaam wamemkataa Makamba na kusema kuwa utendaji kazi wake ni mbovu ndani ya chama.

Hatua hiyo inafuatia tathmini ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo CCM ilifanya vibaya na kupoteza kura nyingi za Urais na majimbo mengi ya Ubunge kwa vyama vya upinzani.

Pia, wajumbe hao wa UVCCM walirejea hotuba ya Mwenyekiti wao wa taifa, Jakaya Kikwete, kuwa CCM inahitaji mabadiliko na kuvua gamba, na kusema kuwa mabadiliko yaanze kwa Makamba kung'oka kwenye nafasi yake ya uongozi.

Katika kikao cha leo, wajumbe wengi waliochangia walimnyooshea kidole Makamba kutokana na utendaji usioridhisha.

Mjumbe wa UVCCM, Shy-Rose Bhanji, alisimama tena kama alivyofanya hivi karibuni Dodoma mbele ya Makamba mwenyewe na kuendelea kumchana kiongozi huyo.

Bhanji alisisitiza kuwa muda umefika sasa kwa Makamba kuachia ngazi kwa vile hatoshi kwenye nafasi ya katibu Mkuu wa CCM.

Nao wajumbe wengine wa UVCCM walisimama na kuunga mkono moto uliowashwa na Bhanji na kusema kuwa Makamba amekuwa mzigo kwa chama na sasa ni muda muafaka kwake kupisha damu mpya ili kuleta uhai kwenye chama.

(Source: Wajumbe wa UVCCM Dar es Salaam)
 
Uongozi wa UVCCM taifa ndiyo umekamatwa na mafisadi na wamekuwa wanawatetea kina Makamba, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge wasitimuliwe kwenye chama licha ya viongozi hawa kuendelea kukichafua chama kutokana na kashfa za ufisadi dhidi yao.
Ndani ya UVCCM kuna vijana ambao hawakubaliani na viongozi mafisadi na wanataka watimuliwe.

ShyRose na vijana wenzake wa UVCCM wanaonesha ujasiri mkubwa kutaka mafisadi watimuliwe kwenye CCM. Wakishindwa kwenye vita hii kali nawashauri wahamie CHADEMA 2015 walete mabadiliko ya kweli Tanzania.
 
Hahaaa!!!! Banji Vs Makamba?????

Hahaaa....hii movie tamu sana

Lilianza kundi against Sitta & Co

Likaja kundi against Sumaye

Sasa kundi against Makamba.....

Ni suala la makindi tu na litaendelea mpaka watafika kwa Mwenyekiti wa chama

Yangekuwa na maana na kuonesha UVCCM haitumiwi kama haya matamko yangetolewa kwa pamoja kwa wale wanaowapinga.....

Vioja zaidi tunavisubiri enyi UVCCM....Keep it up ili na nyie muanze kula, haiwezekani wale wao tuu
 
Subirini Makamba atakavyomjibu huyo Shyrose wenu, last time alimwambia anavaa nguo fupi sana na ana hawara CHADEMA!!. Tusubiri safari hii atatoka vipi huyu mgosi. Makamba bwana!!!
 
Mimi nafikiri UVCCM wangeanza na reform kwa kuwataka viongozi wao wa kitaifa kuondoka madarakani then wakishasafisha uongozi wao ambao ni chaguo la wachache kwa faida ya wachache. Wakishasafisha uozo wao na kudeki chumba chao then waingie kudeki nje ya chumba kwa kuelekea chumbani kwa baba yao. Bila kuundosha uongozi wa UVCCM hawajafanya kitu.
 
hawa vijana ni wapiga debe wa mafisadi..iacheni ccm ichanike.
 
hivi shyrose nae ni kijana? sijui katiba ya ccm inavyoprovide kuhusu umri wa kuwa uvccm.

nisaidieni wadau isije ikawa wanachakachua kila kitu
 
Umoja wa Vichaa Cha Changamkia Mafisadi (UVCCM) una kaaaaazi kwelikweli, Makamba kakambika, Pinda kapindika, Kikwete kafisadika. Wote Vilaza ni Bora hilo Genge la Wahuni likafutwa kabisa hapa Tanzania kila nikilisikia hilo Jina la Mafisadi CCM nashikwa na hasira. Rais na Mawaziri wake wanashangashangaa tu hawajui la kufanya kwenye nchi hii.
 
Back
Top Bottom