Makamba atoa zawadi ya Nguruwe

Status
Not open for further replies.
Kashfa ipo wapi hapo jamani kwa yeye kutoa Zawadi ya Kitimoto.

Kwanza zawadi ni zawadi, Pili Makamba amesoma shule za Mission na vile vile mkewe ni Mkristu sasa kwa yeye kutoa zawadi ya Kitimoto si jambo la kushangaza.

Mbona huwa hamshangai kweli hutuba zake huwa anapenda sana kukopi vifungu nya Biblia kuliko vya Quraan Tukufu.

Acheni mambo ya kumshimanga huyu mzee wa watu
 
jamani mbona wengine wanavila sana tuuu na hawasemi ni dhambi embuse aliyemtoa mzima anapumua, waislam acheni unafiki asilimia kubwa siku hizi wanakula kitimoto tena wao ndio wanaongoza kuvila. Hakuna nyama tamu kama kiti moto hata hao wanaoisakama wanajua.
 
Bado haijawa dhambi yeye kutoa Nguruwe hata kuwaambia watoto wa kiislamu kujiunga na shule hiyo,kosa lingekuwa kama mheshimiwa amewalazimisha waislam kula nguruwe,kwani ni waislam wangapi wanakula kitimoto?au mmemuona makamba tuu ndio mtata?
 
Mnalalamika nini kuzagaa maduka ya vyakula? Nyie dhambi ni kula Nguruwe tu? Mbona dhambi nyingine mnazifumbia macho tu au mnawaonea wivu wanaofaidi kitimoto?

By the way kutafuna kitimoto sio dhambi ndo maana akatoa zawadi ya chakula kwa shule, hii ni zawadi nzuri tu na haina tatizo lolote.

Najua wengine wenu mtakua mmepata kisingizio cha kutokuwapeleka watoto wenu shule kwa sababu navyoona ndicho mnachotafuta hapa, miaka ijayo muanze kulalamika kama kawaida yenu....Acheni hiyo tabia haitawasaidia.

Poleni sana wandugu kama mnaona mwenzenu kawasaliti, Nafikiri mkimsomea ile nanihii, labda itasaidia asirudie tena.

Kula au kutokula nguruwe hakuwezi kunfanya binadamu awe mkosefu kwa Mungu na hata kwa tohara ni hivyo hivyo. Mtu atakuwa mnyofu kwa Mungu kwa matendo na uadilifu wake kwa Mwenyezi Mungu. Baba wa Imani hapa Duniani ni Abraham ambaye hakuna mfano wake katika maandiko matakatifu. Lakini Abraham hakuwa na dini yoyote na wakati wake alikula vyakula vyote na hakuwa ametahiriwa mpaka Mwenyezi Mungu alipotaka afanye tohara kama ishara ya agano lake kwa Mungu.

Tunatakiwa tutahiri mioyo yetu sio mwili ili tupate kuwa karibu na Muumba wetu. Ukisoma vizuri agano la kale baadhi ya mambo ya sheria (Walawi) alizowapa Mwenyezi Mungu Waisraeli wakiwa jangwani kuelekea Canaan zilishapitwa na wakati by the time wanaingia Israel. Mwenyezi Mungu uwaweka hatiani waja wake kwa mioyo na matendo yao sio kwa vitu kama mavazi, vyakula na ishara za nje kama tohara. Kuna haja gani ya kutimiza hayo wakati unauwa albino, unatoa tambiko kwa miungu mlingotini, unadhulumu na huishi vizuri na jirani yako? Tumwache Makamba na Mungu wake.
 
13693_whole_roasted_suckling_pig_600.jpg


Nguruwe wa kuokwa sasa wataanza kupatikana Dar kuanzia December. Nadhani kiongozi bora wa kualikwa siku ya ufunguzi atakuwa ni Bw.Makamba
 
Kwani Makamba kutoa zawadi ya Nguruwe kwa shule ni kosa???

Hakuna kosa lolote. Nguruwe ni nyama safi na tamu kabisa. Tatizo liko kwa hawa wenye dini ya kuosha kikombe kwa nje wakati ndani kichafu na kinanuka. MUNGU awasadie kuujua ukweli.

Saaaaaaaaaaaaafi sana Makamba keep it up.
 
jamani mbona wengine wanavila sana tuuu na hawasemi ni dhambi embuse aliyemtoa mzima anapumua, waislam acheni unafiki asilimia kubwa siku hizi wanakula kitimoto tena wao ndio wanaongoza kuvila. Hakuna nyama tamu kama kiti moto hata hao wanaoisakama wanajua.

Ni kweli kabisa waislamu wanakula sana nguruwe na ndo maana kwenye mfungo wa ramadhani biashara ya kitimoto huwa inadorora.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom