Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mwanakijiji kwa nini uchore mipaka kati ya JK na kundi linalomwingiza?
Mimi tena? angalia mada yangu ya "Kikwete si safi; yes I said it!" yawezekana ilikuwa ya kwanza kumhusisha Kikwete na ufisadi miaka karibu miwili iliyopita. Mpaka ninauchora ni strategic in nature.
Au ndiyo strategy ya Mengi ili mwishowe yeye ndiyo aanze kucall the shots. Kama unakubali kwamba kundi lililomwingiza ni chafu kwa nini yeye awe msafi?
angalia jibu langu la awali..
Leo hii mwanakijiji unakuja na kusema kwamba JK atofautishwe na kundi lake kwi kwi kwi kwi.
Ndiyo na hili siliombei radhi; kosa walilolifanya Marekani kule Iraq ilikuwa ni kuihusisha Baath yote na ufisadi na kuwatimua watu wote waliokuwa kwenye baath (hasa viongozi wa juu) kutoka kwenye utumishi jeshini; matokeo yake waliyaona. Ni lazima katika mapambano ujue mipaka yako na upange vizuri.
Nimesema, siku JK atakaposimama kuwatetea mafisadi au kuwatafutia kinga na hapo yeye naye nitamuita fisadi. Na hilo mimi sina haya nalo na hata Mengi akigeuka na kuwatetea wezi wa nchi yetu na yeye ataitwa fisadi na atakuwa amechagua upande wa dhulma.
Au kwa sababu bosi wako Mengi kamsifia na wewe unaanza kuimba sifa za JK.
Sasa na wewe bosi wako Rostam kuguswa ndiyo imekuwa vurugu sasa?
Mwanakijiji sikuchagulii nani umpigie kampeni, lakini tambua kuwa ukimpigia kampeni fisadi ukija kuniambia unapambana na ufisadi nitakuuliza hata wewe?? Au unafanya usanii
Usanii wa kwangu au wa kwako; huwezi kunichagulia kitu chochote ambacho mwenyewe sijakichagua. Huna nguvu hiyo wala nafasi hiyo. Na mimi sina kwa upande wako. Chukua msimamo unaouona unafaa na uusimamie; si lazima wote tuone jambo moja sawasawa kama maroboti.
In this case, nakubaliana na Mengi kuhusu mafisadi nchini na juu ya nafasi ya JK katika mapambano haya. Kwa hili hakuna utata.