Yussuf Makamba amwinda Reginald Mengi, yeye awataja mafisadi Papa rasmi!

ameshaanza ndio anataja .kataja wachache kidogo

yumo

YUSSUF MANJI

ROSTAM AZIZ

SUBHASH PATEL

RMESH PATEL NA WENGINE WENGI......AKATAJA KUAN MAFISADI PAPA WANA DFEDHA NYINGI SANASANA NA WENGINE WAMEANZA KUTUMIA MAGAZETI HAO NI

RICHMOND

DOWANS

KIWIRA

NSSF

PPF

EPA
 
Imeanza saa 3. Kawataja watano -- Rostam, Jeetu Patel, Yusauf Manji, Tanil Somaiya na Subhash Patel., na amewaambia waende mahakamani hata kesho kama watapenda, ushahidi anao. Asema wamehamisha mabilioni nje ya nchi.
 
Hao wanweza kukua ama wako tanzania ama wako nje ya nchi;nchi ina hela watu wengi hawah=jui watalala nwapi wanaamkaje madawati hakuna watu wamekuw hawana aibu unasaliti vijiji madawati;kweny issue za barabara ujue siku yamwisho unarudi ukoi uko kuzkikwa je utazikwa na watu ambao hawajala hawana dawa ...hawana nguvu hata ya kubeba jeneza...lohhhh
 
Mahakama nayo iwe makini kushuhulikia mafisadi papa.....hata kama wana hela wawe makini sana na hili;mfano katibu mkuu wa wizara anaondolewa kwa kula rushwa tunamwondoa tunabadilisha tena mwingine anakula rushwa anatoka;uwezi maliz sarakani ya rushwa kwa wanaopokea rushwa tu
 
list ya mafisadi papa km ilivotajwa na be. Mengi;
rostam aziz, subsh patel, jeetu patel, tanil somaiya na yusuf manji..
 
Sio kila mlarushwa anaaomba rushwa wengine wanashawishiwa kupokea rushwa...lazima tudili na vishawashi na kuviondoa na jinsi gani ya kufanya ni kudeal na mafisadi papa..vinginevyo utabaki mchezo wa kuigiza
 
Lazima tufike muda tuseme jamani hawa mafisadi papa enough is enough;siku moja wakaamua kuondoka hapa nchini kwa kweli kitaniuma sana mi napenda wanedelee kukaa hapa hapa nchini tutumie pesa zetu
 
Duh namsikiliza mzee kaamua kweli kweli! Mwaka huu atakufa mtu walai, mpaka mafisadi papa wakomeshwe!!
 
Huna jamaa mmoja wa India Kenya yaani nae wanasema ni fisadi angalia KTV u tube ana miliki vituo vya mafuta..na yupo implicated ktk deal nyingi kenya! wanasema alifanya birthday Mombasa iligharimu zaidi ya Tshs 1 billion na sasa anaishi hotelini India analipia USD 1,000 chumba kwa siku!

Mafisadi ni phenomen mbaya!
 
Jamani he has opened doors for all of us to join in and condemn these imbeciles. Lets unity and fight these Mafisadi. It can be doe we just need unity and reform our country and condemn corruption at all level and make sure those people responsible for embezzlement are brought to justice. God bless mengi and others.
Ciao
 
..sasa CCM na Kikwete wamefadhiliwa na hao mafisadi kwa muda mrefu sana. mahusiano ya Rostam na Kikwete ya kuvuruga siasa za CCM na Tanzania kwa kutumia pesa na vyombo vya habari ni ya zaidi ya miaka 10.

..huu ufisadi ukiufuatilia[money trail] kwa jinsi ambavyo wenzetu wa magharibi wanaufuatilia unaweza kufikia conclusion kwamba CCM na Jakaya Kikwete walikiuka sheria za Jamhuri ktk harakati zao za kutafuta madaraka.

..CCM na Raisi Kikwete wanapaswa kuueleza umma kwamba katika uhai wa chama chao wamepokea fedha kiasi gani toka kwa mafisadi waliotajwa na wengine wanaohisiwa kwa ufisadi.

..nakumbuka Barack Obama alirudisha fedha alizochangiwa na yule rafiki yake mtuhumiwa wa ufisadi. ingekuwa vizuri kama Raisi Kikwete na CCM watarudisha fedha zote walizochangiwa na hawa mafisadi. huo ndio uungwana.


Hapo umesema kweli Jokakuu, ufisadi hauwezi kwisha Tanzania kama watu wanafiki kama akina Mengi hawatakwisha. Unawezaje kumsifia Kikwete kuwa anapambana na ufisadi wakati marafiki zake na yeye mwenyewe waliingia madarakani kwa ufisadi. Unawezaje kusifia mahakama kuwa zinafanya kazi vizuri kila wakati kuna watanzania kibao ambao ni maskini wameshalalamika kuwa hawapewi haki zao. Mengi anajua maana ya ufisadi kweli?? Ufisadi ni ukosefu wa maadili kwa hiyo yeye mwenyewe kwa kujipendekeza kwa Kikwete pia anakuwa fisadi papa kama wale wazee wa CCM waliosema JK hastahili kupingwa.
 
Kitu muhimu hapa ni ushahidi wa kuwatupa ndani, hii kuwasemasema tu hawa tayari walishakomaa. maana ni majina yaleyale sijaona jina jipya hapa
 
Hivi huyu Mengi na mshikaji wake Idd Simba hawakuwemo kwenye ule uuzaji wa hisa za NICO wakati kampuni ilikuwa haijaanza rasmi uzalishaji?? Huo pia ni ufisadi kwenda kuwauzia hisa walimu wa shule za msingi kwa kuwadanganya kuwa watapata gawiowakati kampuni haioperate. Mengi kama unataka ufisadi utokomee kuweni na nyie ni wasafi na pia acheni tabia ya kujikombakomba kwa JK. JK ni fisadi na hata wewe Mengi ukijifanya kumpamba haitasaidia. JK ametumia magazeti kwa muda wa miaka 10 kuwachafua wenzie ili aingie ikulu na hiyo dhambi mpaka leo inawaandama akina Jenerali Ulimwengu na Salva Rweyemamu. Wewe leo unakuja unasema JK shujaa!!! Kama huna jipya kaa kimya, ukikaa kimya hawatakuchinja kama kondoo kama ulivyosema mwenyewe. Maana utakuwa huwatishi, ila kwa kitabia chako cha kupambana na ufisadi selectively unabore stiff
 
laiti kama wangekuwa wanafanyiwa kazi ipasavyo wala tusingekuwa na nyimbo za kila siku, hivi kwa nini sheria ya kukata viungo isingebadilika na watu wote hawa wakakatwa wao? at least lingekuwa fundisho
 
kwikwikwi mengi hana jipya......ati anampa shavu jk......hao aliowataja jk ndio anawatumia kuchota mijihela.....

.....nani mshika mihuri? mwenye dhamana hao ni wafanya biashara tu wamepata baraka zoote toka kwa jk.......
 
Mengi nae ni fisadi tu ,ila anataka kuwahi na mapema ili ionekane nae ni katika anaochukia mafisadi ,matajiri wote tulio nao ni mafisadi kwa njia moja au nyingine maana ni watu wanaosapoti Utawala wa Sultani CCM kwa hali na mali zaidi waswahili tunasema hivi ni vita vya Mengi na wengine katika kugombania maslahi linganisha na ile ya Mwakiembe na Rostam

Kwamba wanaompa shida kwa sasa ni hawa hivyo ni lazima atumie mbinu za kuwagandamiza na kuwaangusha ili abaki yeye ndio maana yake,ile kesi ya mzee wa vijisenti imeishia wapi ?
 
kwikwikwi mengi hana jipya......ati anampa shavu jk......hao aliowataja jk ndio anawatumia kuchota mijihela.....

.....nani mshika mihuri? mwenye dhamana hao ni wafanya biashara tu wamepata baraka zoote toka kwa jk.......

I agree totally...you cant bite the hand that feeds you, labda Mengi afanye hizi bidii kujulisha wananchi lakini sio kutegemea kwamba chochote kitafanyika juu ya hawa jamaa.
 
kwikwikwi mengi hana jipya......ati anampa shavu jk......hao aliowataja jk ndio anawatumia kuchota mijihela.....

.....nani mshika mihuri? mwenye dhamana hao ni wafanya biashara tu wamepata baraka zoote toka kwa jk.......

si wajitokeze kina Rostam na Manji na wenyewe walaani yaliyotokea Benki Kuu angalau tujue wanakerwa? Mbona hadi leo Lowassa na kina Patel na kina Don Ande hawajajitokeza kusema hata jambo moja dhidi ya EPA, na wizi wa mamilioni yetu Benki Kuu?

Wote hawa wana matatizo yao, lakini kumuweka Mengi kwenye kundi la wezi wa Benki Kuu ni kukosa kuwa wakweli.

Leo hii Mkapa aliyekuwa Rais wakati wizi mkubwa unatokea nchini hadi leo hajajitokeza kulaani yaliyotokea na badala yake amejikunyata kimya! Kina Makamba badala ya kulaani yaliyotokea wanataka kina Mengi wanyamaze! Kina Kaboyonga badala ya kulaani wizi wa fedha zetu wanataka kina Slaa wanyamazishwe! tukisema tumelaaniwa au tumerogwa watu wanasema tunajitukana!

Sasa hapa wanajitokeza wengine kujaribu kuneutralize alichosema Mengi ili tusipime madai dhidi ya wezi wa utajiri wetu! Kama kina Manji, Patel, Rostam na wenzao wanaona wameonewa na kuwa wanasingiziwa waende mahakamani! Kama wanashindwa basi na wao angalau wajitokeze na kulaani ufisadi nchini! Hawawezi; ufalme hauwezi ukajipinga wenyewe halafu ukasimama!

Kama na wenyewe wanajua Mengi ana mambo yake ya kifisadi wajitokeze basi wayaseme na kuonekana ni watetezi wa taifa basi..
 
Jamani, hebu mnihabarishe -- ufisadi wa Mengi ni upi? Nimerejea list ya EPA hayumo. Radar pia hayumo. kadhalika hayumo katika Deep Green, Meremeta, Mchuchuma, Tanpower, BoT Twin Towers, Mwanachi Gold, Ubungo NSSF Godowns, Richmond, Dowans, Ndege ya Rais na nyinginezo zinazotajwa na kuandikwa kila mara kwenye magazeti (mainstream newspapers).

Huenda ufisadi wake ni ule wa kulazimisha tu na huandikwa kwenye magazeti uchwara. Hiyo mnasema ya NICO na Idi Simba mbona haitajwi, ila tu hutajwa na wale wanaohangaika kuutafuta "ufisadi" wa Mengi na kuandikwa kwenye magazeti hayo uchwara? Kwa nini Watanzania tunakuwa hivi? Huyu mtu amejitolea mhanga kupambana na mafisadi waliokubuhu na wanaojulikana, vipi tena naye aambiwa fisadi?

Niliwahi kusema katika thread moja ya nyuma kuhusu Rostam kwamba ni bora nchi hii ikawa na akina Mengi watano tu, kuliko kuwa na kina Rostam elfu moja. Tofauti na Mengi, michango yao mikubwa ni kwa CCM tu, na madhumuni yake yanajulikana.

Hebu tuambieni, mnaompinga Mengi, mbinu zenu ni zipi za kumaliza ufisadi?
 
Back
Top Bottom