Makalio ya watu wa CCM yana Misumeno?

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Wana Bodi
Jumanne jioni 19/6/2012 katika mjadala wa bajeti, Mbunge wa Viti Maalum, Chadema aitwaye Conchesta Rwamlaza amenivunja mbavu. Katika hali ya kujiamini sana, alidai kuwa serikali hii kila mwaka inaleta bajeti ya mamilioni ya kununua viti vipya. Akaendelea kusema kuwa, amekuwa bungeni akikalia kiti kile kile na wala hakijaharibika. Ndipo akahoji, "KWANI HAWA WATU WA SERIKALI, MAKALIO YAO YANA MISUMENO?"

Piga picha mwanabodi, ufikirie makalio (masaburi) yenye msumeno, ambayo kila yakikalia kiti kinachanwa na huo msumeno!

Pamoja na kwamba hii ni lugha ya picha, lakini kimsingi, watu wa serikali yetu wana misumeno vinywani mwao na mifukoni mwao kwa sababu kasi ya kutafuna fedha ya serikali sawa na kasi ya msumeno unaokata mbao.

Ahsante sana kamanda Rwamlaza.
 
Yule mama wakati anaanza niliona kama atachemsha.Lakini mpaka anamaliza alikuwa na hoja za nguvu sana. Kumbe uteuzi wa viti maalumu CDM haukuwa wa kubabaisha kama watu wanavyotaka kututanabaisha.Dr Kitila na timu yake kumbe walifanya kazi ya uhakika. Kama sijasahau huyu mama ndiye aliyewapa ile nukuu ya Mwl kwa nini vyama vya upinzani vilianzishwa,ili kuitoa serikali legelege(dhaifu) ya CCM madarakani au kuirekebisha madudu yake
 
Kwanza kabisa makalio ya wakuu wa CHADEMA yanasemaje?
Hebu jiridhishe mwenyewe na utujuze.
 
Hiyo ni bajeti tu ya makaratasini, huwa wanaipanga then wanaila na haitumiki katika ukarabati
 
Yule mama wakati anaanza niliona kama atachemsha.Lakini mpaka anamaliza alikuwa na hoja za nguvu sana. Kumbe uteuzi wa viti maalumu CDM haukuwa wa kubabaisha kama watu wanavyotaka kututanabaisha.Dr Kitila na timu yake kumbe walifanya kazi ya uhakika. Kama sijasahau huyu mama ndiye aliyewapa ile nukuu ya Mwl kwa nini vyama vya upinzani vilianzishwa,ili kuitoa serikali legelege(dhaifu) ya CCM madarakani au kuirekebisha madudu yake

Aliyenukuu ile nukuu ya hayati baba wa taifa anaitwa Naomi Kaihula aligombea ubunge jimbo la Ilala lakini kura hazikutosha ndipo akachaguliwa kuwa mbunge wa viti maalum,yule mama ni bonge la jembe.
 
Haya mambo ya makalio tumuulize Meya Masaburi na wabunge wa Dar kwa watumishi wa umma hapo Duh! labda yana Magamba
 
Kwa nini uchakachue heading, kasema watu wa serikali na si wa CCM. Serikalini kuna watu wa vyama vyote na si ajabu hata wewe uko serikalini na ndo mnaomba fenicha kila mwaka.

Ustarabu wa kuanzisha habari ni kuileta kama ilivyo watu wenyewe ndo wachambue kuliko kuanza na uongo kwenye heading.
Shame on you!
 
Back
Top Bottom