Makadirio fyongo ya viongozi kila mara katika kukamilika miradi ya serikali ni ishara mbaya sana

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,641
46,298
Hii tabia ya viongozi wa serikali au wasimamizi wa mashirika ya umma katika miradi ya serikali kutoa tarehe za kuanza au kukamilika kwa miradi zisizo na uhalisia hata kidogo ni kiashiria kikubwa cha uwezo mdogo wa kiutendaji kusimamia miradi hiyo, uongo uliopitiliza wa watawala na watumishi wa umma au yote mawili.

Mradi kama ya SGR zimetangazwa tarehe za kujaa gunia kuhusu kukamilika kwake lakini kila mara tarehe hizo zinapofikiwa hakuna chochote, Bwawa la umeme la Nyerere nalo hali ni hiyo, Miradi mingi ya barabara kuanzia huko Kigoma na kwingine kwingi hali ni hiyo pia na miradi mingine mingi pia.

Kwa hakika ni sehemu chache sana duniani kwenye mataifa yaliyo na utendaji wa hali ya juu kama China, Japan, Korea Kusini, Singapore na baadhi ya Ulaya ambapo miradi hukamilika kwa wakati kwenye dot, lakini hata huko kwingine kote duniani ambapo miaradi huwa inachelewa huwa haichelewi miaka bila sababu za msingi sana na pia viongozi huwa makini sana kutoa ahadi za ukamilikaji wa miradi yenyewe, sisi inawezekana tumekithiri na kuvunja rekodi.
 
Back
Top Bottom