Makabila mengi yenye wanawake wazuri kama Wapare wanapewa sifa ya kuwa malaya kwasababu ya wivu wa kijinga

Wanaonekana malaya kwa sababu rate ya kutongozwa ni kubwa kuliko kwa wale wa kawaida.
 
Kwema Wakuu!

Acheni wivu! Yaani mkiona Watu wamebarikiwa jambo fulani roho mbaya zenu mbaya hazitulii. Wivu na maumivu moyoni yanawachoma. Mnaanza kuropoka mashudu yenu.

Mkiona mdada mzuri tuu mnaanza kumpa majina Mabaya. Kisa anatongozwa na Wanaume wengi. Utajiri wa mvuto wa kisura na kimaumbile haihusiani na tabia ya umalaya.

Makabila yenye wanawake wazuri hapa Tanzania imekuwa kawaida kuwahusisha na Umalaya lakini ukichunguza vizuri unakuja kugundua ni Wivu tuu. Kwa mfano Makabila kama Wambulu(Wairaq), Wanyaturu na ndugu zao Wanyiramba, Warangi wote hao ni makabila yènye wanawake wazuri na wanahusishwa na Umalaya jambo ambalo sio Kweli.

Wanawake wa Wapare wapo top five ya wanawake wazuri hapa Bongo, na Kwa wanaume wao wapo top 3 ya wanaume wazuri hapa Tanzania. Hiyo ukubali au ukatae. Upareni kukutana na Handsome boy sio jambo la kushangaza kwa sababu wapo wengi. Kukutana na Wanawake wazuri sio suala la ajabu.

Tabia hiyo pia ya roho mbaya imehamishwa kwenye mambo ya kiuchumi. Makabila yenye Mafanikio ya kiuchumi kama Wachagga, Wakinga, au Wapemba hupewa majina Mabaya kama wizi, ujambazi, ufisadi na uchawi. Acheni wivu.

Huwezi kuoa mke mzuri asitongozwe na wanaume. Kwa sababu wanaume wanapenda wanawake wazuri. Wewe kama kipimo cha kutotongozwa kwa mkeo ndio kutokuwa malaya basi elewa kuwa mkeo hana mvuto, sio mzuri na hana la maana.

Upande wa pili, huwezi kuwa na Mwanaume Handsome boy au mwenye uchumi alafu wanawake wenzako wasimsarandie. Haipo hivyo. Ukiona mumeo yupoyupo tuu na hakuna Mwanamke hata mmoja anayemtaka ujue hapo hakuna kitu. Umepoteza.

Wanawake wa kipare wanajiamini, hawataki kuonewa, hawataki unyanyasaji wa kijinsia kwa Jina la Mfumo dume, wapo radhi wabadilishe wanaume hata elfu moja ikiwa tuu wanapata Wanaume Mabwege wasiojitambua.

Wanawake wa kipare au kichaga, kama unapenda kwenu lazima upende na Kwao. Kuhusu ufupi nyundo ni sifa yao pia, lakini pia wapo Warefu hasa wanaôtokea Upareni kaskazini maeneo ya Mwanga.

Wapare kwa ujumla sio Watu wa kusikiliza maneno ya Watu Wajinga na watu wasiojiamini au wenye roho za chuki kisa tumewazidi mambo nyeti ambayo hayanunuliwi kwa pesa.

Povu Rukhsa!
Huna haja ya kutetea, chochote kizuri kitatafutwa na wengi. Uzuri wa mwanamke ni nini? Hapo kuna majibu mengi - lakini kwa wanaume wengi ni msichana mwenye heshima, mvuto wa kijinsia ya kike, mwili usiokuwa na dosari kubwa , uso usiokuwa na alama kubwa, msichana anayevutiwa na wanaume. Sasa kama ni msichana anayevutiwa na wanaume, na hapo hapo wanaume wengi wanafuata na kutoa ahadi kede kede. Mimi sioni kosa la mwanamke kwa kuwa dunia inaendeshwa kwa misingi ya "supply" na "demand ". Hakuna malaya hapo ni hali ya kibinadamu mtu kutumia vipawa alivyopewa na Muumbaji wake.
 
Back
Top Bottom