Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

Ulimsikia mwakyembe alivosema kuwa " mtu muhimu aliesaidia kupambana na madawa kwa % zaidi ya 90, aliishia kufungwa jela mpka leo! Bila kumtaja huyo mtu, pia alieleza kuwa jitihada zake zote za kumtoa huyo mtu zilishindikana!

"Labda kwanza ayakate majina mengine ndo amkabizi"

Mwakyembe anaonyesha Jinsi gani Vita ya Madawa ya kulevya ilivyongumu na haiwezi kutatuliwa kwa Mihemko au sifa binafsi.
 
Ulimsikia mwakyembe alivosema kuwa " mtu muhimu aliesaidia kupambana na madawa kwa % zaidi ya 90, aliishia kufungwa jela mpka leo! Bila kumtaja huyo mtu, pia alieleza kuwa jitihada zake zote za kumtoa huyo mtu zilishindikana!

"Labda kwanza ayakate majina mengine ndo amkabizi"


Kwahiyo bado anazunguka nayo mfukoni
 
Rais anayeondoka Madarakani hukabidhi kila kitu kwa Rais mpya.Sina shaka kabisa kwamba Kikwete alikabidhi Orodha ya Wahusika wa Dawa za kulevya.
Kwa hiyo orodha hiyo Dr Kikwete alimkabidhi Dr Magufuli ya wauzaji wa madawa ya kulevya ndiyo unataka kusema hivyo??
 
Mwakyembe anaonyesha Jinsi gani Vita ya Madawa ya kulevya ilivyongumu na haiwezi kutatuliwa kwa Mihemko au sifa binafsi.
Huyo Dr Mwakyembe atoe hata mwongozo wa namna ya kupigana hii vita na si kulalamika.

Watanzania tuache mzaha ktk hii vita ninajua vijana wanavyoangamia kwa madawa ya kulevya.

Lazima tupigane tu aidha ni vita ya angani,nchi kavu au majini maadui lazima waangamie wote.

Na Serikali kushirikiana na NGOs na Taasisi za kitaifa na kimataifa hebu angaliane namna ya kuwasaidia vijana waliingia ktk hili janga ili warudi ktk maisha yao ya kawaida.

Na kuanzia program za Harm Reduction pia nchi mzima yaani Upunguzaji Madhara kwa watumishi wa msaada ya kulevya kama alivyosisitiza Kamishina Jenerali Singa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kudhibiti Madawa ya kulevya.
 
Vigogo dawa za kulevya watajwa

Written by Mwananchi
Monday, 18 September 2006

*Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
*Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
*Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
*Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani

WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biasharahiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili niwafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.

Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya
viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na
marobota ya mitumba.

Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa
Dar es Salaam na Zanzibar.

Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.

Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito
zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

Ufukwe wa Pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji inaelezwa kuwa linatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za
kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.

Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi
watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.

Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya
nchini, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa vijana wanaotumika kuingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.

Vile vile, katika kundi hili mwanamke mmoja anayefanya kazi katika taasisi moja ya fedha anatajwa kuwa anashiriki katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa
kusafirisha kwenda nje fedha nyingi za kigeni akitumiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya nchini.

Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia
mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.

Barua hiyo ya kurasa 10, pia inamtaja mwanamke mmoja ambaye anatumika kupitisha dawa za kulevya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuwa ni sugu; aliwahi
kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, lakini hivi sasa yupo mitaani kifungo chake akitumikia mtu mwingine.

Alipoulizwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alisema hajapata barua hiyo na kwamba atalizungumzia
baada ya kuipata.

Naye Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema hana taarifa za kuwako kwa barua hiyo. Hata hivyo, alisema kuna tume ya dawa za kulevya iliyopo
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia zaidi suala hilo.

Alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi za kukamata watu wanaojihusisha na dawa hizo na kwamba mikakati mingine ya kupambana na watumiaji inafanywa na tume
hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Polisi liongezewe uwezo wa kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha vituo vya kazi askari
waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu.

Pia alilitaka Jeshi hilo lijisafishwe lenyewe kutokana na madai kwamba polisi wanahusika na baadhi ya matukio ya uhalifu nchini.

Rais alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu, na wanaojua waliko majambazi wazipeleke taarifa hizo kwake kama wanaogopa kuzipeleka polisi.


Katika kuitikia wito huo, wananchi kadhaa waliandika barua iliyooroshesha majina ya polisi 20, wakiwamo baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na kuikabidhi kwa Waziri wa Usalama wa Rais, Bakari Mwapachu.

Tangu wakati huo, mabadiliko makubwa yameshuhudiwa yakifanywa kwenye jeshi hilo, hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa watu kujitolea kuandika barua yenye
majina na maelezo ya kina kama hii kuhusu biashara ya kulevya na kuipeleka kwa Rais.
Noted
 
Mzee Es
Hili ndilo tatizo la watanzania, ni wazuri kusema au kuteta lakini kwa matendo ni zero kabisa.

Kumbuka RA ni mwanahisa wa Mwananchi Communication kwa hiyo itakuwa ni ndoto kutaja majina ya wahusika hasa kama kuna majina ya baadhi ya wanamtandao.
Mimi nataka kuona JK akitoa hizo list za majina anayopelekewa na aliyokiri kuwa anafahamu mwenyewe. hata kama hana uhakika na kama kweli wanahusika basi itakuwa ni wakati mwafaka kwa wahusika kujitokeza kukataa au kukubali shutuma.

tuna safari ndefu.
True
 
Majina ya vigogo ninayo-JK

03 Oct 2006
By Mwandishi Wetu


Rais Jakaya Kikwete, amekiri kupokea majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kwamba majina hayo yanafanyiwa kazi na watendaji wake.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alikuwa akijibu swali kutoka mmoja wa wahariri aliyetaka kujua iwapo amepokea waraka wenye majina ya vigogo wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Bila kufafanua, Rais Kikwete alijibu, “waraka nimeupata na nimewapa wahusika na wanaufanyia kazi.” Inadaiwa kwamba, katika waraka huo ulioandikwa na kikundi kimoja cha wananchi, kimetaja majina ya vigogo zaidi ya 100 wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ama kuingiza nchini dawa za kulevya au kuwa mawakala wa dawa hizo au wauzaji.

Kwa mujibu wa waraka huo, baadhi ya wafanyabiashara waliotajwa ni wa kutoka mikoa ya Tanga, Mbeya, Dodoma, Kigoma, Arusha, Iringa, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar wamedaiwa kuhusika na biashara hiyo.

Aidha, katika waraka huo, umetaja baadhi ya hoteli Jijini Dar es Salaam, kutumiwa kama vituo maalum vya kukutanisha wafanyabiashara wa dawa hizo, kwa ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Kazi ya kuandaa taarifa hiyo yenye kurasa 12, ilifanywa na Shirika moja linalopigania haki na Usawa na Mazingira katika Jamii la Jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kwamba, taarifa hiyo ya siri, ilikabidhiwa kwa Rais Kikwete kupitia kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bw. Bakari Mwapachu.

Katika taarifa hiyo, yamo baadhi ya majina ya wabunge, wafanyabiashara maarufu, maofisa wa idara nyeti za serikali kama vile Mamlaka ya Mapato Nchini, Benki Kuu (BoT) na maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi, pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini.

Viwanja vilivyotajwa kwenye waraka huo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro (KIA), Zanzibar (Karume Aiport), Tanga, Arusha na Mbeya.

Mbali na viwanja vya ndege, waraka huo umetaja wafanyabiashara hao kuzitumia Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar na fukwe za Bagamoyo kuingiza shehena kubwa za dawa hizo.

Taarifa hiyo pia imetaja majina na namba za magari ya watu yanayotumika kusafirisha dawa hizo na kusambaza kwa walengwa jijini Dar es Salaam.

Pia majina ya kampuni za ndege zinazotumiwa na watuhumiwa hao kuingiza dawa, huku wengine wakitumia mikataba ya usafirishaji wa vifaa vya hospitali pamoja na matairi ya magari.


* SOURCE: Nipashe
Hiyo list ya majina iliyotajwa Ikulu ya Magufuli ianze nayo kuifanyia kazi
 
Back
Top Bottom