Majina ya Viwanja Gezaulole : Aliyefanikiwa kupata ile list ya mgawo wa viwanja atuwekee hapa

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
15,287
10,842
Wakuu ninaomba kama kuna member alifanikiwa ku-save ile orodha ya mgawo wa Viwanja Gezaulole atubandikie hapa. Nimepita website ya Municipal naona wameshaiondoa maana mgawo wenyewe ulikuwa ni wa kujiuliza maswali!!!

Asanteni sana.
 
Angalia katika orodha hii.
 

Attachments

  • MAJINA YA WALIOPATA VIWANJA.pdf
    315.8 KB · Views: 1,059
Watayatoa tu tuendelee kusubiri inasemekana wamechelewa kidogo kwasababu viongozi wengi wapo Bungeni maana inatakiwa wachague viwanja wavitakavyo baada ya hapo sasa vigawiwe kama vitabaki.
 
hui mradi wa kigamboni hauna manufaa....
Wananchi mnaliwa elfu 30 zenu,viwanja wanapeana wabunge, mawaziri na watoto wa vigogo....

Upuuzi mtupu....
Wizi mtupu....
 
he he he he he he he hii noma ss viongozi wasipojipa viwanja wapewe nani??hii ndo inchi yetu bana kila kitu lazima kwanza familia za viongozi wajigawie zeni masalia ndo yanabaki kwa wanainchi
 
Halafu naomba kuuliza ina maana asilimia kubwa ya majina ya walioomba ni dhehebu aina moja? au macho yangu
Pili kama kuna mkakati wa kujenga mji mpya nadhani priority wangepewa wakazi wa huko Kigamboni achana na Mheshimiwa no 218.
 
Angalia katika orodha hii.

Asante sana mkuu. Ila naona watu wanasema hii ni orodha ya awamu ile ya kwanza. Kuna rafiki yangu amewasiliana na mtu wa huko ardhi Temeke na wanasema bado. Ila tu nitashaangaa kama hawa viongozi walipewa vile vya awamu ya kwanza na sasa wapewe tena. Huo nitasema ni uroho na ubinafsi.
 
Back
Top Bottom