Majina ya Vijiji vya Wilaya ya Masasi ni 'Kiboko yao'

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,040
Lupaso, Lukuledi, Lulindi, Luchelewa, Lukwika, Luatala, Lusonje. Chiungutwa, Chikundi, Chikukwe, Chilimba, Chiroro, Chipango, Chipembe, Chiwata(ilipo Chidya Sec. Sch.). Chiwale, Chivirikiti. Mkolopola, Mkarango, Mpeta, Mkumbaru, Mkwapa. Nanjota, Nanganga, Nangoo, Namajani, Nakalola. Nanjisa, Nangaramo, Nakachindu, Namikunda, Nairombo, Navai, Nangose... KARIBUNI WAKUU!!
 
Mwena (ilipo Ndanda na nimesoma hapa) mtaa maarufu hapa ni mkorosho haramu, hapa utapata kila aina ya nyama za pori, chaguo lako, Liputu, Ndoro,
 
Mi nimekaa masasi kota za TRM(tanzania road maintenence) cku hizi tanroad 90-94, hivi bado zipo au ndio vile, kuna sehemu ilikuwa inaitwa "wapi wapi", "msimbazi" hospita ya ndanda na nyangao bado zipo? Long time kipindi hicho nasoma chekecheka duu. Tumetoka mbali
 
Mkuu kila ulichoulizia hapo kipo! Ila kuna vitongoji vimezuka ndani ya mitaa ile uliyoijua kabla. Mfano kuna barabara imepita kuanzia hapo Wapiwapi mpaka maeneo ya Madeco kupitia Kisiwani hadi uwanja wa Sabasaba.
 
Nasikia eti Masasi ndio wilaya tajiri kupita zote Tanzania?
 
madeco, uwanja wa 7,7 bado upo? Kuna shule ya primary nilisome std one, ni mchanganyiko, wasio ona, viziwi na wazima ipo kule mliman karibu na kanisa, unaikumba jina? Mi nimelisahau nikumbushe mkuu
 
madeco, uwanja wa 7,7 bado upo? Kuna shule ya primary nilisome std one, ni mchanganyiko, wasio ona, viziwi na wazima ipo kule mliman karibu na kanisa, unaikumba jina? Mi nimelisahau nikumbushe mkuu

Uwanja wa Sabasaba upo Mkuu na Shule uliyoitaja ipo Mtandi na hapo ni sehemu ya kihistoria, kwani kanisa lililopo lilijengwa karne ya 18 na wamisionari wa Anglican na ni moja ya mahali pa mwanzo kuasisiwa na Wakoloni ktk ukanda wa kusini mwa nchi yetu. Baada ya hapo walisambaa sehemu nyingi kama vile Chiwata, Kanyimbi, Utimbe nk. Karibu tena Masasi Mkuu!
 
Vp shida ya maji bado ipo au imeisha?

Bado ipo shida Mkuu! Japo bomba la kutoka Ndanda hadi Masasi limeshafika siku nyingi. Ajabu mvua zikinyesha ndo maji yanapatikana ktk mabomba. Zaidi muulize Dogo Nape kwani nafasi yake haijakaimiwa hata virago hajabeba pale nanihii.
 
Daah chikundi kuna maembe gongo pale balaa daah mate yamenijaa

Kweli Mkuu Chikundi pana neema ya ardhi nzuri hasa kwa kilimo cha Mpunga, Mahindi, Mbogamboga na Matunda aina kwa aina. Lakini wakulima bado wamebaki wapweke hawana ushauri wa kitaalam kama upo si wa karibu. Achilia mbali suala la pembejeo.
 
Nasikia eti Masasi ndio wilaya tajiri kupita zote Tanzania?

Mkuu sina hakika kuhusu hilo. Ila ktk maeneo yaliyojaaliwa raslimali nyingi Masasi imo. Ardhi yenye rutuba, Misitu, Mito(Ruvuma, Mbangara, Miesi, Lukuledi, Mwiti, Mto Ndanda nk.)kuna madini na sehemu za kihistoria.
 
Mtandi pr. School, yap nimekumbuka, ndio lile kanisa na long sana, ila limekaa pazur mlimani, ila du kipindi kile kulikuwa na nyani. Unakumbuka mafuriko ya ndanda 92? Ming'oko, ndanda spring water, makopa,... Long time sana.
 
oya daktari bingwa wa mifupa ( Mwambe yupo?aliwakunitibu ulva bone daa jamaa noma )ndanda.
 
Lupaso, Lukuledi, Lulindi, Luchelewa, Lukwika, Luatala, Lusonje. Chiungutwa, Chikundi, Chikukwe, Chilimba, Chiroro, Chipango, Chipembe, Chiwata(ilipo Chidya Sec. Sch.). Chiwale, Chivirikiti. Mkolopola, Mkarango, Mpeta, Mkumbaru, Mkwapa. Nanjota, Nanganga, Nangoo, Namajani, Nakalola. Nanjisa, Nangaramo, Nakachindu, Namikunda, Nairombo, Navai, Nangose... KARIBUNI WAKUU!!
Vingi ya hivi navifahamu, niliwahi kuishi Chigugu kwa muda wa kama wiki mbili na pia pale Ndanda kwa wamisionari. Kwa kweli Masasi ni kuzuri na watu wa kule ni wakarimu, natamani kurudi tena.....
 
Mtandi pr. School, yap nimekumbuka, ndio lile kanisa na long sana, ila limekaa pazur mlimani, ila du kipindi kile kulikuwa na nyani. Unakumbuka mafuriko ya ndanda 92? Ming'oko, ndanda spring water, makopa,... Long time sana.

Ndanda spring water ipo Mkuu ukiwa Dar ukipita maeneo ya Temeke Sudan huwezi kukosa maji yao pale ktk kituo cha mabasi ya kwenda Masasi, Nachingwea nk. Makopa na Ming'oko ipo tunakandamiza. Kuhusu nyani wa kule mlimani Mtandi bado wanaonekana kwa nadra kutokana na kupanuka kwa mji wa Masasi wanaelekea kutoweka. Mafuriko ya Ndanda ilikuwa Mwaka 90 kama sijakosea. Nilikuwa ktk kambi ya wauguzi Ndanda hosp. Nikiuguza Dadangu!
 
oya daktari bingwa wa mifupa ( Mwambe yupo?aliwakunitibu ulva bone daa jamaa noma )ndanda.

Dkt. Mwambe ameshafariki miaka yapata mitatu au zaidi. R.I.P Alikuwa ni zaidi ya daktari huyu Bwana. Alikuwa ni mtu wa watu.
 
Back
Top Bottom