Majina ya mawaziri wanaopaswa kujiuzuru yatua mezani kwa JK

Status
Not open for further replies.

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
HATMA ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

eeh bana freedom is comming tommorrow
Thubutuu,Usitegemee jipya chini ya serikali ya magamba. Mbona tangu mkuu wa nci alipoingia madarakani alituambia ana list ya majambazi na hakuwashughurikia na aliwaambia wajirekebishe, ile lists ya wauza unga, ile lists ya EPA, lists ya kwao ya CCM ya kujivua magambayaani troika(vijisenti,mamvi na rost amu)!!! Hapa ni kiinimacho tu ninachokiona.
 
HATMA ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

mbona kwenye list hiyo wapo 6?
 
Kama atawafukuza hao mawaziri sita, ina maana tayari rais anamaanisha serikali yake sio makini hivo basi avunje bunge zima na ajiuzuru tufanye uchaguzi upya, na asigombee kabisa aende kuishi ughaibuni!
 
Pinda naye awe kwenye list ya kujiuzulu.Anawatetea wezi.Pia amekula hela ya MFUKO wa MAAFA .Mpaka leo waathirika wa MABOMU YA GONGOLAMBOTO hawajalipwa wakati pesa nyingi ilichangwa na TAASI MBALIMBALI.
 
alishindwa kuwatoa kina Mponda na Nkya leo hii awatoe hao sita!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom