Majina ya mawaziri wanaopaswa kujiuzuru yatua mezani kwa JK

Status
Not open for further replies.
Hivi Haji Mponda hajioni kuwa yeye hafai tangu enzi za MGOMO WA MADAKTARI?
HATMA ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Ni nani? Mkulo ndiye aliwanyima posho au Pinda hao Mawaziri wa5 ni sahihi kabisa tuache hasira na Pinda
 
HATMA ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

kwan hajui kama ni MZGO?hadi aambiwe,?huyo anayepelekewa nae pia tatzo
 
Thubutuu,Usitegemee jipya chini ya serikali ya magamba. Mbona tangu mkuu wa nci alipoingia madarakani alituambia ana list ya majambazi na hakuwashughurikia na aliwaambia wajirekebishe, ile lists ya wauza unga, ile lists ya EPA, lists ya kwao ya CCM ya kujivua magambayaani troika(vijisenti,mamvi na rost amu)!!! Hapa ni kiinimacho tu ninachokiona.

Yaani ndo taabu ya kumpa ikulu msanii,kazi ipo. Huwa nikifikiria kidogo tu juu ya serikali yetu na hatma ya nchi hii nashkwa na hasira sana.KAZI TUNAYO
 
Hao panya hawatakiwi wajiuzulu, hawana hadhi ya kujiuzulu!
Wanatakiwa wafukuzwe kazi Panya buku hao!
Nitamshangaa sana kikwete kama atakubali kujiuzulu kwao! Kinachotakiwa rais kama atapenda kulinda heshima yake ambayo imepungua sana ni kukataa kujiuzulu kwa mawaziri, na Kuwafukuza kazi. hii at least itamsaidia kulinda kaheshima kadogo alikonako kwa jeshi la polisi na tume ya uchaguzi!
 
Serikali yote ni mbovu,bora uchaguzi uitishwe kila siku wanakula mabilioni ya Watanzania hakuna anaewajibishwa pesa zimeota manyoya na zimepeperuka.
 
Atalikuta kwenye soft copy

Nahisi virus watakuwa wamelitafuna lote au hard disk itaoa error message.
Unleess kama Computer yake ina antivurus ya M4C halafu yeye ndo kirusi wa kwanza sijui itakuwaje? Atayala hayo mafaili mwenyewe au atakubali anti virus ifanye kazi? Kazi ni kwake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom