Majibu yangu kwa Bodaboda wa Mbeya aliyetaka kusikia maoni yangu kuhusu Mh. Rais Magufuli

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Leo tarehe 1/6/2018 nikiwa katika Jiji la Mbeya nimekutana na kijana aliyenitajia jina moja la David ambaye anafanya biashara ya usafirishaji maarufu kwa jina la Bodaboda.

Alinisafirisha kutoka eneo la Soko Matola mpaka Sangu.

Tukiwa njiani tulifanya mazungumzo mbalimbali,David akataka kusikia maoni yangu kuhusu Rais MAGUFULI,nikamuambia Rais MAGUFULI anafanya kazi ngumu ya kung'oa kupe wanaomnyonya Ng'ombe.

Rais MAGUFULI ana taka Ng'ombe asiwe na kupe ili atoe maziwa yatakayotutesheleza watu wote tunywe mpaka tusaze.

Hata hivyo kazi ya kung'oa kupe hao sio rahisi, tuzidi kumuombea. Ni kiongozi mwenye maono anayetaka wote tunufaike na raslimali zilizopo ataifikisha nchi hii pazuri.

Akakaa kimya akatikisa kichwa, kisha akanitwika swali jingine, "mbona Mbunge wetu walimfunga"

Nikamjibu Mbunge wenu alifungwa kutokana na kutoa matamshi ya matusi, nikazidi kumuambia kwamba Mbunge wenu hatimizi majukumu yake hivyo anafanya vurugu na fujo ili nyinyi mumuone kama anafanya kazi kumbe hafanyi kitu.

Nikamuambia msikae vijiweni mkadanganyana kuwa Mbunge wenu alifungwa kwa kuonewa sio kweli.

Hata hivyo Rais MAGUFULI ni muungwana sana akaamua kumtoa kwa msamaha siku ya Muungano naamini atakuwa ameshajifunza kwamba siasa bila matusi inawezekana.

Nikaendelea kumuambia Rafiki yangu huyu kwamba CCM inawajali na kuwathamini vijana wa Jiji la Mbeya na ndio maana imetoa fursa ya vijana wa Mbeya kusoma mafunzo ya ufundi bure, Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole alipofanya ziara Jijini hapa mnamo mwezi wa February mwaka huu alitoa ahadi hiyo na tayari imeshaanza kutekelezwa, nikamgeukia yeye nikamuuliza je ameshawahi kusikia juu ya fursa hiyo?

Akanijibu ndio lakini hakuwa na taarifa kamili, nikamuambia aache kufuatilia masuala ya CHADEMA kwani hayatamsaidia katika maisha yake bali aanze kutafuta taarifa sahihi za CCM na Serikali ndizo zitakazomsaidia kwani fursa nyingi kama mikopo na mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana.

Nikaendela kumuambia kwamba sasa hivi awamu ya 5 Boda Boda na machinga wa Mbeya mnafanya biashara zenu kwa Uhuru bila bughudha; Rais MAGUFULI anawalinda msiweze kuonewa ili mpate riziki zenu kwa halali na kwa amani kabisa. Kama kina Sugu na wapinzani wenzie wanaona huo ndio udikteta basi ni udikteta mzuri.

Kutahamaki nikawa nimeshafika Sangu na rafiki yangu David akaishia kuniomba namba ya simu na kuniahidi anaenda kuichoma kadi yake ya Chadema kwani sio chama chenye agenda ya kumkomboa kijana bali kumtumia kama karatasi ya plastiki na kisha kumtupa.
 
Mimi naendesha bodaboda mitaa ya Sangu na ndiye nilikubeba, huwa spendi story nikiwa naendesha chombo cha moto ili nikufikishe salama pamoja na ujinga wako.
Halafu masuala ya kumzungumzia mbunge wetu na vitu vya ajabu acha.

sasa nikuulize maswali;
Nb: una umri gani, tabia ya kuvaa suti za kondakta daladala na yebo uache.
1. Kubana matumizi maana yake nini?
2. Baraza dogo la mawaziri maana yake nini? Baraza lina wajumbe wangapi na ni dogo ukilinganisha na nini?
3. Utawala wa sheria maana yake nini? Kwanini watumishi hawapandishwi mishahara na vyeo wakati ni suala la kikanuni na watumishi hewa wameondoka?
4. Suala la vyeti feki kwanini linabagua?
5. Kwa taarifa yako nilikuona huna lolote nikaamua kutulia unipe hela yangu upotee.
 
Bahati mbaya kwako mlamba viatu wa ufipa
Bodaboda niliyemkodi kituo chake sio Sangu na hana Smart phone.
Pole yako
 
Hii ndo aina ya waumini wa sisiemu!! Mwenyekiti alivyowaambia mpambane sana kujibu hoja mitandaoni hakua na maana ya kuleta utumbo unaonuka kma huu!!! Rudi lumumba kajifunze kuandika vizuri
 
anang'oa kupe waliokuwapo kwnye zizi lake mwenyewe (ccm)hata na hvyo ameshndwa sbb hao kupe wamehamia mpaka kwnye zizi lingne la (serikali)na kuibinafsisha km yao as if wao ndyo wenye hatimiliki.dawa ya kupe c kung'oa ni kupiga dawa na dawa yao ni bunge imara na katiba mpya
 
Bahati mbaya kwako mlamba viatu wa ufipa
Bodaboda niliyemkodi kituo chake sio Sangu na hana Smart phone.
Pole yako
Ulimkagua ukajua hana smart phone!! Ulijuaje kama kituo alichokuchukulia ndo anapofanyia shughuli zake siku zote!! Afu nyie wana lumumba mnafikiri kwa kutumia nn!!? Kila anaekuja na hoja kinzani mnadhani ni mwana CHADEMA!! naeza kuwa napinga hoja zako lakini haimanishi mie ni CHADEMA!!
 
Bahati mbaya kwako mlamba viatu wa ufipa
Bodaboda niliyemkodi kituo chake sio Sangu na hana Smart phone.
Pole yako
Uliangalia kitambulisho chake? Ulimsachi mifukoni na hukuiona smart phone? Acha uzubezubempunyenye.
Kwanza yawezekana weye ni kibaka. Ulishindwa kumpora pikipiki ukaanzisha vistori vyako huku ukijidai ni usalama wa taifa fake! Hahahahaaaa
 
Kuwa CCM ni mzigo mzito wenye tani kadhaa juu ya kichwa.Unavuruga utendaji kazi wa ubongo na kuharibu ufanisi wa mishipa ya fahamu!
 
We kama nani hapa nchini hadi atake kusikia maoni yako juu ya Raisi!!?
 
Mleta uzi ni hovyo kabisa. Yaani anawafanya watu wote kuwa mazezeta.
 
Leo tarehe 1/6/2018 nikiwa katika Jiji la Mbeya nimekutana na kijana aliyenitajia jina moja la David ambaye anafanya biashara ya usafirishaji maarufu kwa jina la Bodaboda.
Alinisafirisha kutoka eneo la Soko Matola mpaka Sangu.
Tukiwa njiani tulifanya mazungumzo mbalimbali,David akataka kusikia maoni yangu kuhusu Rais MAGUFULI,nikamuambia Rais MAGUFULI anafanya kazi ngumu ya kung'oa kupe wanaomnyonya Ng'ombe.
Rais MAGUFULI ana taka Ng'ombe asiwe na kupe ili atoe maziwa yatakayotutesheleza watu wote tunywe mpaka tusaze.
Hata hivyo kazi ya kung'oa kupe hao sio rahisi ,tuzidi kumuombea.
Ni kiongozi mwenye maono anayetaka wote tunufaike na raslimali zilizopo ataifikisha nchi hii pazuri.

Akakaa kimya akatikisa kichwa , kisha akanitwika swali jingine , "mbona Mbunge wetu walimfunga "
Nikamjibu Mbunge wenu alifungwa kutokana na kutoa matamshi ya matusi ,nikazidi kumuambia kwamba Mbunge wenu hatimizi majukumu yake hivyo anafanya vurugu na fujo ili nyinyi mumuone kama anafanya kazi kumbe hafanyi kitu.
Nikamuambia msikae vijiweni mkadanganyana kuwa Mbunge wenu alifungwa kwa kuonewa sio kweli.
Hata hivyo Rais MAGUFULI ni muungwana sana akaamua kumtoa kwa msamaha siku ya Muungano naamini atakua ameshajifunza kwamba siasa bila matusi inawezekana.

Nikaendelea kumuambia Rafiki yangu huyu kwamba CCM inawajali na kuwathamini vijana wa Jiji la Mbeya na ndio maana imetoa fursa ya vijana wa Mbeya kusoma mafunzo ya ufundi bure ,Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg, Humphrey Polepole alipofanya ziara Jijini hapa mnamo mwezi wa February mwaka huu alitoa ahadi hiyo na tayari imeshaanza kutekelezwa ,nikamgeukia yeye nikamuuliza je ameshawahi kusikia juu ya fursa hiyo? .
Akanijibu ndio lakini hakua na taarifa kamili, nikamuambia aache kufuatilia masuala ya Chadema kwani hayatamsaidia katika maisha yake bali aanze kutafuta taarifa sahihi za CCM na Serikali ndizo zitakazomsaidia kwani fursa nyingi kama mikopo na mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana.
Nikaendela kumuambia kwamba sasa hivi awamu ya 5 Boda Boda na machinga wa Mbeya mnafanya biashara zenu kwa Uhuru bila bughudha Rais MAGUFULI anawalinda msiweze kuonewa ili mpate riziki zenu kwa halali na kwa amani kabisa.Kama kina Sugu na wapinzani wenzie wanaona huo ndio udikteta basi ni udikteta mzuri.

Kutahamaki nikawa nimeshafika Sangu na rafiki yangu David akaishia kuniomba namba ya simu na kuniahidi anaenda kuichoma kadi yke ya Chadema kwani sio chama chenye agenda ya kumkomboa kijana bali kumtumia kama karatasi ya plastiki na kisha kumtupa.
Upumbavu huu umeurithi toka kwa mmoja wa wazazi wako
 
Back
Top Bottom