Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina

Kwa majibu haya naona watu wengi mmelizika ninaswali kwenu, Je Mbowe nae akija na majibu kama haya mtalizika? ??
 
Watu wengi hawaelewi system ya elimu ilivyo kuwa kipindi cha Nyerere na cha Mwinyi. Hasa kule usukumani, watu walikuwa wanasoma mpaka darasa la saba, wakifanya mtihani wa darasa la saba wakifeli mtihani ule walikuwa wanarudia darasa, sasa atarudiaje darasa, walikuwa wanachukuwa majina ya watu ambao wameacha shule. Mfano anaweza kuchukuwa jina la mtu yuko darasa la tano au la nne. Na kwa kuwa yeye anauzoefu wa madarasa yaliyo mbele yake walikuwa wanafaulu sana. Sometimes walikuwa hawafaulu, kwa hiyo walikuwa wanarudia tena na tena na tena. Ndio maana ulikuwa unakuta mtu yuko form one lakini anawatoto. Hilo ni kosa la zamani lilifanyika huwezi ku correct sasa. Kuna ma Prof wengi wa vyuo kikuu wana majina ambayo basically sio yao. Hivyo ndivyo naweza kuona kitu kilicho mkumba Migulu nchemba
 
Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja.
Mwigulu,
very interesting!.

Pasco
 
Nimefurahi mno kwa majibu ya Kiungwana kabisa Kama hivi ulivyofanya. Hongera Kweli Umekomaa kisiasa
 
Kuna maswali mengine yanaleta kero.Si kila mtu ni fukuza maana baadhi yenu mngefurahi sana serikali ya JPM ikionekana inafeli ili mpate cha kuongea. Kwa mtazamo wangu mnaelekea kumwambia hata majina ya rais JPM ni feki.
Magufuli ni jina la Kitu cha kufungia mlango(Pad lock) na hivyo ni Feki, Joseph si jina lake hilo ni la Mme wa Maria aliyemlea Yesu hivyo ni Feki! Jina Pombe hata usiseme maana ni jina la kileo ni Feki! Kwa hiyo atafute majina yake original.
Tutaelekea wapi tukiwa na ufahamu mdogo ili kufurahisga ego za watu kadhaa?. Mwigulu amejieleza. Ungetaka kusikia Rais amemtengua kwa sababu jina Mwigulu si lake ni jina linalomaanisha Mbunguni na yeye yu ngali duniani? Hivyo rais ameamua atenguliwe? ( On a light note)duh mwaka huu kuna watu!
haifanani. hapa sio raisi anajadiliwa.. raisi hana shida ya majina yake, yako sawa kabisa.
 
Watu wengi hawaelewi system ya elimu ilivyo kuwa kipindi cha Nyerere na cha Mwinyi. Hasa kule usukumani, watu walikuwa wanasoma mpaka darasa la saba, wakifanya mtihani wa darasa la saba wakifeli mtihani ule walikuwa wanarudia darasa, sasa atarudiaje darasa, walikuwa wanachukuwa majina ya watu ambao wameacha shule. Mfano anaweza kuchukuwa jina la mtu yuko darasa la tano au la nne. Na kwa kuwa yeye anauzoefu wa madarasa yaliyo mbele yake walikuwa wanafaulu sana. Sometimes walikuwa hawafaulu, kwa hiyo walikuwa wanarudia tena na tena na tena. Ndio maana ulikuwa unakuta mtu yuko form one lakini anawatoto. Hilo ni kosa la zamani lilifanyika huwezi ku correct sasa. Kuna ma Prof wengi wa vyuo kikuu wana majina ambayo basically sio yao. Hivyo ndivyo naweza kuona kitu kilicho mkumba Migulu nchemba
ss wa zamani tunajua hilo, je mlengwa alichukua jina la mtu?
 
mi nadhani tuna mambo mengi ya kujadili.
mhusika kashatoa ufafanuzi
kwa mtu mwelewa atakuwa ameeelewa.


tusipende sana siasa .
 
Haya siyo majibu niliyotegemea toka kwa waziri. Kuna watu wanapongeza lakini nadhani ni kwa sababu wanadhani umetupendelea kutoa majibu. Waziri unatakiwa utoe majibu yenye muelekeo wa ukweli na wakati mwingine ukubali kwamba ulikosea ktk maisha yako, u hata ukubali kwamba kwa wakati ule hukuwa na control na mambo kama hayo, labda wazazi au ndugu au nesi au mwalimu alikusaidia kuingia kwa majina yasiyo yako.

Ulichokifanya hapa ni kutafuta huruma kwamba umekulia mazingira magumu sana! Kwamba kwa juhudi zako umeweza kujinasua na hali hiyo ngumu. Kwamba unastahili pongezi kwa kuchunga ng'ombe na baadaye leo wewe ni waziri (performance aside). Huruma zimekuangukia na ndiyo maana unaona pongezi hizo. Binafsi sioni jibu la matatizo ya shule na majina yako. Umeulizwa na watu hapa ueleze ktk kuacha shule na kurudi shuleni mara kadhaa uliwezaje kuchota jina lile lile kila wakati? Miaka ya 80 tayari ilikuwa hairuhusiwi kurudia shule. Usingeweza kuacha na kurudi rahisi kiasi hicho. Lazima kuna mtu ktk familia aliyekusaidia ktk udanganyifu huo.
Huyu ni zaidi ya hatari:-[:-[
 
Hii inaonyesha hakukuwa na jina lingine zaidi ya kuombwa nesi amchagulie jina! hivi unataka kusema baba yake hakuwepo hapo amchagulie mwanae jina au huko kwao majina yalikuwa yameisha kabisa hadi nesi apewe heshima ya kuchagua jina!

Embu nunua hata katuni ya nyau peleka nyumbani muulize mtoto wako huyu tumuite nani lazima atakutajia jina!

so how comes jina la huyu mheshimiwa lilikuwa na utata! Je alipatiza jina gani akiwa mdogo!

Mkuu hapa kubali ukweli ulitumia cheti cha Mwigulu Nchemba aliyeacha shule mwaka 1984/1985 ndio maana unajaribu kufanya connection eti mifugo ilikufa ndio maana ukaamua kurudi tena na jina na dactari ina maana kabla ya kuacha ulikuwa unatumia jina la Lameck Madelu Mkumbo.

Sasa inadhihirisha kuwa wewe ulimaliza shule mwaka 1984 kama Lameck Mkumbo na ukafeli sawasawa ukaamua kwenda kuchunga hao Ng`ombe hewa unaojitetena nao. Then ulipoona mifugo anakufa na hakuna dili tena uliamua kuomba masaada wa kwalimu watafute jina na mtu aliyeacha shule ili wewe utumie jina hilo kufanya mtihani wa darasa la saba, hapa ndipo unapoibuka na uongo wa kuungaunga eti uliporudi ulichukua jina la dactari ( Uliwezaje kulikumbuka yapata ilikuwa ni more than 12 years tangu ulipozaliwa)

Je ni kwanini ulichukua majina yote ya huyo unayemwita dactari hadi la ubini na ukaamua kuachana na ubini wako wa mkumbo?

Tukumbuke: Enzi hizo kulikuwa na utamaduni wa mwanafunzi akifeli anatafutiwa shule nyingine na jina lingine ili arudie shule kutokana na nafasi za kuchaguliwa wanafunzi kwenda sekondari zilikuwa chache sana hivyo altenative was ilikuwa na kurudia kwa majina ya mwanafunzi mwingine aliyeaacha kwenye shule nyingine.

Hii ameionyesha wazi mh. pale alipokiri kuwa walimu walikuwa wakishinda nyumbani kwao kumwomba arudi shule hapa ukweli ni kwamba walimu walikuwa wanajua kuwa mh alikuwa na uwezo mzuri japo hakufaulu kwa mwaka husika hivyo wajaribu chance nyingine.

Hii ilithibithishwa na matokeo yako ya form IV,VI, UDSM and Masters kwamba uko vizuri.

Ila ipo siku mwingulu nchemba mwenyewe ataibuka baada ya kuchoka kujificha!
 
Kubadili majina kama hakutokani na kubadili dini au migogoro mingine ya kifamilia, siku zote huwa ni ku-take advantage kwenye kitu fulani.

Wewe Mwigulu unatakiwa utueleze ulikuwa una-take advantage ya nini!?
 
Mwingulu nadhani umeona watu walivyo wengi kwenye mitandao ifike mahali kabla ya kufanya maamuzi bungeni muwe mnaleta hoja kwenye social media watu wachangie kwanza then mnapeleka sasa bungeni kutokana na hoja za wadau.
 
Toka jana watu 77,543 wameview page yako, je ikiachwa kwa siku 5 ni zaidi ya laki 3 watakuwa wameview hiyo page hata kama kuna hoja ya msingi watu wanaweza kutoa mawazo yao siyo wote tunaweza kuingia bungeni. nawasilisha
 
Kwa tuliobahatika kukaa mjini ambapo shule za secondari za serikali za kutwa (sio boarding) tutamzonga huyu mheshimiwa maana kwanza wengi wa mjini pass mark ya kuingia form one haikuwa kubwa kivile na shule zlikuwa za kutosha pamoja na kwamba wengi walikuwa hawachaguliwa yaani mtu akipata jumla ya maksi zote 80/150 (masomo matatu anaingia form one) wakati kijijini ili uingie secondari wengi wao walikuwa wanafaulu kwa marks za juu yaani mpaka 130/150 (masomo matatu) lakin bado hawachaguliwi kwa kuwa walitegemea zaidi shule za boarding.

Hata kama ingekuwa ametumia jina la mtu toka primary kwa wakati ule ilikuwa sawa tu kwani wengi walikosa elimu ya secondari kutokana na uchache wa shule za serikali kiasi kwamba mtu ukichaguliwa form one (tulikuwa tunaita kufaulu) unafanyiwa sherehe. Kilichokuwa kinafanyika wenye nia ya elimu walikuwa wanaomba baada ya wale watoro sugu kuacha na kutokomea kusikojulikana na kuchua namba ya mtoro sugu kisha baadae wanabadilisha shule ambapo kwa sasa shule ni nyingi za secondari ukienda kinachoangaliwa ni nafasi tu kama ipo unaingia kwa jina lako
 
Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari.

Sentensi hizo zinaonyesha kuwa Mwigulu alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi darasani kwa hiyo walimu wake hawakufurahishwa na kitendo cha Mwigulu kuachishwa masomo kwa ajili ya kuchunga ng'ombe na ndiyo maana walikuwa wanashinda nyumbani kwa baba yake kumshawishi amurudishe Kijana wake shule.

Mbali na walimu kutoa msaada wa kumshauri baba yake kumrudisha Mwigulu shuleni msaada mwingine uliotolewa na walimu hao ni kutafuta jina ambalo lilikuwa bado liko kwenye system litakalomfanya mwanafunzi aliyeacha shule aendelee na shule na jina lenyewe ni la Lameck Mwigulu ambalo linaelezwa kuwa lilikuwa ni jina la daktari na upande mwingine linaelezwa kuwa ni jina la mwanafunzi aliyefauru lakini kutokana na ufukara wake alishindwa kuendelea na masomo ya juu.
 
Kosa la mwigulu siyo uhalali wa majina!!
Laa hasha, wala hatugombani na ubora wa akili yake kimasomo.
Tunapambana na UDANGANYIFU.
Sisi tunafahamu kuwa mtu ajulikanaye kwa jina la Lameck Mkumbo alifanya mtihani wa darasa la saba mwaka (.. ) katika kituo cha mtihani cha shule ya msingi (.....) akafeli
Halafu mtu yule tunayemfahamu kwa jina la Lameck Mkumbo anafanya tena mtihani wa darasa la saba mwaka (.....) katika kituo cha mtihani cha shule ya msingi (....) this time kwa jina la Mwigulu Nchemba, Akafaulu!!!!!

AMELIONGOPEA TAIFA.
Anaweza kuwaongopea wanyaturu
Hawezi na haitawezekana awaongopee wanyiramba wa kata nzima ya kyengege!!!!!

Kwa ucha MUNGU wao, wakazi hawa dhamira zinawasuta kuona huu mwendelezo wa kulidanganya taifa.

Labda kama uongo sio kosa kwa namna yoyote.

Sikutaja majina ya shule na miaka kama wito kwa Mwigulu Aliombe radhi taifa kwa uongo ule
TAIFA KAMA TAIFA LIKO TAYARI KUMSAMEHE ONCE AND FOR ALL.
Huu unaitwa uongo mtakatifu ana kosa,muache afanye kazi vyeti c vyakwake,tatizo lipo wapi,tena uyu ni mpiganaji ninae muunga mkono kwa 100%,mbona watu wana tawala kwa kugushi matokeo ambwabwaji na awaombi radhi.

Mwiguru katumia plan ili afanikiwe,kama JPM alivyotumia M4C na akafanikiwa mbona amjamwambia aombe radhi.

Utamaduni huu ni wa binadamu yoyote akishindwa plan A anabadili B,ongera Magu kwa kutumia M4C kilichokuwa kinatakiwa ni kufanikiwa basi,watanzania acheni umbea fanyeni kazi, HAPA KAZI TU vyeti makaratasi
 
Kuna uwezekano kabisa alisomea jina la mtu, hiyo haikuwa tatizo kipindi cha zamani. Mi nakumbuka kuna watu sasa hivi ni ma Prof, wengine ni wakubwa, lakini walirudia rudia sana shule na ilikuwa sio rahisi kurudia kwa kutumia jina lako la kwanza, ilikuwa unatumia jina la mtu aliye acha shule ambaye bado yuko kwenye system. Wengine ilikuwa inawalazimu wanarudia darasa la sita au la nne kabisa. Wengi sana walifanya haka kamchezo, hasa wale waliokuwa wanasoma kijijini kama jamaa alivyo eleza
In short ni kweli mweshimiwa anaweza kuwa na yeye alipita njia hiyo hiyo. Hilo sio tatizo, ila inaonyesha jamaa aliyechukuwa jina lake ni msukuma unajua kipindi kile wasukuma wao walikuwa hawajali shule kazi yao ilikuwa kuchunga ng'ombe tu.
ss wa zamani tunajua hilo, je mlengwa alichukua jina la mtu?
 
Safi sana kwa wadhifa wako nilijua hautakuja hapa kujibu.... Asante Kiongozi
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
 
Hakuna ulichojibu zaidi ya propaganda nadhani wanaokusifia ni washabiki wako kutoka kulee lichama pendwa Tupiamo wasifu wako kamili tuone tangia shule ya msingi,upili....
 
Mnawatafuta wenye vyeti feki wa nini sasa huko makazini hali ya kuwa watu wanachapa kazi??
DNA babako kadanganywa.
Huu unaitwa uongo mtakatifu ana kosa,muache afanye kazi vyeti c vyakwake,tatizo lipo wapi,tena uyu ni mpiganaji ninae muunga mkono kwa 100%,mbona watu wana tawala kwa kugushi matokeo ambwabwaji na awaombi radhi.

Mwiguru katumia plan ili afanikiwe,kama JPM alivyotumia M4C na akafanikiwa mbona amjamwambia aombe radhi.

Utamaduni huu ni wa binadamu yoyote akishindwa plan A anabadili B,ongera Magu kwa kutumia M4C kilichokuwa kinatakiwa ni kufanikiwa basi,watanzania acheni umbea fanyeni kazi, HAPA KAZI TU vyeti makaratasi
 
Back
Top Bottom