Majibu ya Membe: Mchango wa Tanzania kutatua mgogoro wa Libya ni Kupitia African union(A.U)

Usahuri wangu kwa Ben. Usiwe mwepesi kutumika ktk mambo yasiyokuwa sahihi. Anayekutuma anakudharau kwa kuona unatekeleza jambo lake la kipumbavu. Kabla hujasema kitu, na hasa kinachohusu Taifa hili, jitahidi kufanya utafiti wa kutosha, usiwe kama Dr. Wilbroad Slaa anayetangaza vifo vya watu kila kukicha bila ya kuwa na uhakika na taarifa anazoletewa. Hakuna hukumu ya kukaa kimya, bali kuna hukumu, tena kubwa ya kusema uongo. Naenda kulala, tutakutana tena nikiamka.

Sijatumwa na yeyote.Sasa kumbe unajua umuhimu wa tafiti sio?Sasa mbona unasema uongo bila kufanya Tafiti?Sitaki kuingia katika mtego wa kuhisi kuwa wewe umetumwa au unatumika,ila sitaki kufikiria hivyo kwa sababu utanishushia upeo kufikiri.Huwa ninajadili issues based on facts and credibility Period.Nitarudi bado
 
Nyoooooooooooooo mpaka tutupe bakuli la kuwa omba omba, Ajaribu aone kama hajawa kama mugabe na hivi ni zuzu ndo hata mwaka hauishi mkate sh laki nane
 
Inaonekana unalijua vizuri sana jambo hili na nini kinachotakiwa kufanyika. Je, unaweza kutueleza ni nini kinachotakiwa kufanyika na kwa namna gani?[/QUOTE]

Msimao wangu uko hapa.
Natoa onyo kuwa serikali isipochukua hatua ya kutazama mwenenndo wa misimamo katika siasa za kimataifa, basi upo uwezekano mkubwa wa heshima ya Rais na hadhi ya nchi kuchafuka katika medani za kimataifa”.
Nitatoa mfano.

Serikali ya Kenya kupitia Rais wake Mwai Kibaki imekataa kupeleka kesi za watuhumiwa wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo (post election violence) katika mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita (International Criminal Court –ICC).

Na izingatiwe kuwa katika jitihada za kutafuta kuungwa mkono, serikali ya Kibaki ilimtuma makamu wake wa Rais, Kalonzo Musyoka kufanya ushawishi wa kidiplomasia ili nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania iwaunge mkono (Shuttle diplomacy).


Umoja wa nchi za Afrika (AU) umeunga mkono msimamo huo wa serikali ya Kenya wa kukataa watuhumiwa hao wa vurugu za uchaguzi kupelekwa mahakama hiyo ICC nchini Uholanzi na badala yake wanataka watumie mahakama maalum za ndani ya Kenya (Special Tribunal Courts) kushughulikia tuhuma hizo. Serikali yetu ya Tanzania nayo kupitia AU imeunga mkono msimamo huo wa kukataa watuhumiwa hao kupelekwa ICC.


Lakini naomba itiliwe maanani kuwa msimamo huo wa serikali ya Kibaki si msimamo wa Wakenya walio wengi, kwani kwa mujibu wa matokeo ya kura rasmi ya maoni iliyopigwa hivi karibuni, asilimia zaidi ya 60 ya Wakenya wanataka watuhumiwa hao wakashitakiwe katika mahakama hiyo ya IC iliyoko The Hague nchini Uholanzi.


Pia hata Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila Amolo Odinga, yupo upande wa Wakenya walio wengi akipinga uamuzi huo wa Kibaki na wenzake.


Tatizo ni nini?

Tatizo ni kwamba serikali yetu kupitia AU imeunga mkono uamuzi wa serikali ya Kibaki wa kutowapeleka watuhumiwa hao ICC na jitihada za serikali hiyo za kutaka kujiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa Roma (Rome Statue) wakati Wakenya walio wengi hawataki.

Ikumbukwe Tanzania ilipata fursa ya pekee ya kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Kenya baina ya upande wa Kibaki na Odinga, heshima hiyo tulipewa kwa heshima ya kuaminiwa (Honest broker) katika kusimamia matakwa ya Wakenya.

Na kwa kutambua mchango wa nchi yetu, Rais alipewa zawadi ya kutunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Umma cha Jomo Kenyatta.


Kwa mantiki hiyo, kwa msimamo ambao serikali yetu imeonyesha, wa kutofautiana na Wakenya walio wengi (zaidi ya asilimia 60), ni dhahiri upo uwezekano kwa nchi yetu kujiingiza katika mgogoro wa kidiplomasia baina yetu na wananchi wa Kenya.


Upo uwezekano pia wa nchi yetu kujiingiza katika mgogoro wa kidiplomasia baina yetu na serikali ya Kenya katika siku za usoni kama Rais wa nchi hiyo atakuwa Raila Odinga wa chama cha ODM ambaye tayari ameshatangaza azima yake ya kuwania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2012.


Ninatoa wito wa kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, kutoa tamko la kuueleza umma wa Watanzania kwanini wameiingiza nchi yetu kwenye msimamo unaopingwa na Wakenya wengi ambao ni majirani zetu na ni ndugu zetu wa karibu. Je, waliona ni busara tu kumuunga mkono Kibaki na wenzake wachache na kupuuza matakwa ya
Wakenya walio wengi?

Je hawaoni kwa kufanya hivyo wanalichonganisha taifa na majirani zetu wa karibu?

Katika hali ya kawaida nilitarajia kuona serikali yetu ikiheshimu matakwa ya Wakenya na msimamo wetu wa awali ambao ulikuwa ni kusimamia maslahi ya Wakenya walio wengi.

Kimsingi, sera na misimamo yetu katika siasa za kimataifa, hasa diplomasia ya uchumi, vimekuwa vikiyumba, badala tumetilia mkazo diplomasia ya kuomba misaada na kushukuru. Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kisera, mchakato wa kupata katiba mpya ni vema ukatumiwa kufanikisha mabadiliko hayo.




Typical of a vindictive and malicious person. Discussion hii kwa muda mrefu imejikita kwenye personalities na vitu vya kufikirika. Hivi umeambiwa hao BRIC au hayo mataifa unayoyazungumzia wana policies ambazo hazifungamani au haziangalii maslahi ya wakubwa? Mengi yaliyozungumzwa humu ynalenga ku-discredit waziri as if kuna mambo yalikuwepo huko nyuma na sasa yameharibiwa na yeye. Niambie ni wakati gani katika historia ya nchi hii sisi tulikuwa na sauti kwenye vyombo vya maamuzi huko UN kama Security Council? Sasa unalaumu nini leo? Issue ya Somalia ni fupa ambalo limeishinda dunia nzima ni hiyo ni kwa sababu za historia ya Somalia na nature ya society yao na hata namna mgogoro wao ulivyo. Sasa ulitegemea kwamba kipimo cha ufanisi wa AU ni kuangalia suala la Somalia? Mbona hata South America unaowa-adore wameshindwa kutatua tatiza la Colombia na FARC na limekuwepo kwa miongo kadhaa sasa na bado wewe unaona kwamba wako okay.

Ukweli ni kwamba mijadala mingi ya watu wa aina ya Ben ni ile ambayo imechochewa na ajenda nyingine na inayochomekwa na watu wenye ajenda binafsi na ndiyo maana watu wanatoa disclaimer kabla kwa sababu wanajua kwamba ita-attract criticism ya hali ya juu kutoka kwa watu ambao ni objective and right thinking. Ukweli ni kwamba ubora wa foreign policy ya nchi siyo kuwa na policy yenye ukinzani na Marekani maana hata Blair na ukubwa na historia ya kutukuka ya nchi yake bado alikuwa perceived kwamba anaendeshwa au kutumikia sera ya nje ya Marekani. What is a big deal about us here?

Kwenye Nchi za BRIC kwanza nikusahihishe Siku hizi zinaitwa BRICS (Baada ya South Africa Kujiunga),mataifa hayo yanazinagtia maslahi yao hayazingatii maslahi ya wakubwa kama unavyotaka kupotosha hapa.Haingii akilini kusema ati kwa Mfano China au Russia wanaweza kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya wakubwa kama US.

Kuhusu kwamba ni lini tuliwahi kuwa na sauti katika jumuiya kimataifa.Kumbuka Serikali ya Mwalimu nyerere ilikuwa na Sauti katika Jumuiya ya Kimataifa,Tanzania ilikuwa mojawapo wa nchi zilizokuwa na sauti na influence katika NAM

Tanzania ilishawahi kuisusia Jumuiya ya Madola kupinga Serikali ya Kikaburu ya Afrika kusini kuhudhuria mkutano wa jumuiya ya Madola

Tanzania ili-abstain Katika kupinga au kupitisha mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia,Comprehensive Test Ban Treaty(CTBT).

Tanzania ilishawahi kushiriki na hata kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel katika kupinga unyanyasaji dhidi ya Palestinians
 
Mbona walivyokwenda Comoro hawakusubiri AU.

Democratization is not our top Priority in our Foreign policy.Wakati tunakuwa mstari wa mbele kupinga mapinduzi ya kijeshi au kuondoa serikali zilizochaguliwa kidemokrasia yet hatupingi Electoral malpractices katika chaguzi mbali mbali Afrika

Pia hatuna Rekodi ya kutetea haki zaBbinadamu
 
Back
Top Bottom