Majibu ya hoja za Lissu kuhusu ruzuku ya Chadema

Hata Idd Amin hakuangushwa madarakani na wanajeshi wa Tanzania bali aliangushwa na wanajeshi wake ambao walijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

CHADEMA itaangushwa na wanachama na viongozi wake wanaokihama chama na kujiunga na vyama vingine.

Siasa za chama Kikuu cha Upinzani nchini zina muda wa uhai kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF.

Hata vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF vilipoanza kupukutika, kuna viongozi wao waliojitokeza na kupiga bla bla huku wakiukataa ukweli kama anavyofanya Tundu Lissu.

Maelezo ya Tundu Lissu yanasadifu ukweli unaosemwa kuwa CHADEMA ni chama cha Mbowe. Yaani chama kinamwagiza Mbowe akakope popote kwa mtu yeyote halafu baada ya kukopa hawaambii amekopa wapi na kiasi gani bali anachowaambia ni kiasi anachotaka walipe. Gosh!

Maisha ya CHADEMA kama chama kikuu cha Upinzani yako ukingoni.

Waingereza wana msemo usemao, ''Beware the last kicks of a dying horse''.

Swali la kujiuliza kwa sasa ni hili, Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Chama gani kitakuwa ni chama kikuu cha upinzani baada ya CHADEMA?
Kilaza
 
Najaribu kufikiria jinsi Mbowe alivyoweza kupenyeza Chadema hadi kushinda urais ktka nchi isiyojali demokrasia wala haki za binadamu. Huyu jamaa Mungu atamlipa!!!

Hua nikimsikia Lissu anavozungumza mpakaa mwilibhua unasisimka. Huyu jamaa ni ORATOR. Sauti hii ni muhimu sana kizazi hadi kizazi. Mimi simpendi Jiwe, nampenda MBOWE kwanza na LISSU pia!!!

CCM tunapata tabu mbona!!
 
Dah! Yaani kamati nzima inamuagiza Mbowe atafute pesa!!! Kokote!!! Ooooh Tanzania .....kauli ya Tundu Lissu hii .....ooooh Tanzania ....
Watu wakisema chadema ni mali ya mbowe wanabisha.Haiwezekani chama kikawa kinapata 200M+ kwa mwezi plus pesa wanazochangishwa wabunge kikashindwa kuwa na miradi kwa ajili ya kujiendesha.Chama kila ttz kinamuangalia mbowe,Hiki chama au saccos ya mtu binafsi.Kwa maana hiyo bila mbowe hakuna chadema.

Ukiangalia tayari kuna conflict of interest kati ya mbowe na chama.Yani chairman anafanya biashara na chama.Maelezo ya lisu ni kukivua chama nguo na kupigilia misumari hoja ya chadema ni Mali ya mbowe.
 
mkuu, kuna mambo yanakera sana na yasipozungumzwa wakati fulani ndio tunaingia kwenye mtanziko. Hata hivyo, kukaa kimya kwa watuhumiwa tusiwatafakari kwamba ni wajinga. Umewahi kufahamu kwa Lissu ndiyo alikuwa wakili wa Chacha katika kesi zake?
Mambo mengine bwana . . .tusiamshe vilivyo lala kwa sababu za kipuuzi
Skendo iliyopo ni chadema kupitia mbowe wanahusika na kifo cha chacha.Kwa maelezo ya lisu ukitumia akili ya kawaida lzm uamin kweli chadema wanahusika.Anakili chacha alikua na ugomvi na viongoz wenzie,anakili chacha kutangaza kutaka kiti.Kilichomtokea huwez kuacha kuunganisha dots zote hizi.Mwita kusema mbowe alimwambia atamshughulikia chacha na ukiunga na haya maelezo ya lisu unapata picha.Hizi blah blah za ooh nilimsaidia kesi mara cjui nini hazina mcng wwt ktk kujieleza chadema kuhusika na kifo cha chacha.Kiufupi desa la lisu kuanzia chacha hadi hbr za ruzuku ni kwamba kakikaanga chama badala ya kukisafisha.
 
Hata Idd Amin hakuangushwa madarakani na wanajeshi wa Tanzania bali aliangushwa na wanajeshi wake ambao walijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

CHADEMA itaangushwa na wanachama na viongozi wake wanaokihama chama na kujiunga na vyama vingine.

Siasa za chama Kikuu cha Upinzani nchini zina muda wa uhai kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF.

Hata vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF vilipoanza kupukutika, kuna viongozi wao waliojitokeza na kupiga bla bla huku wakiukataa ukweli kama anavyofanya Tundu Lissu.

Maelezo ya Tundu Lissu yanasadifu ukweli unaosemwa kuwa CHADEMA ni chama cha Mbowe. Yaani chama kinamwagiza Mbowe akakope popote kwa mtu yeyote halafu baada ya kukopa hawaambii amekopa wapi na kiasi gani bali anachowaambia ni kiasi anachotaka walipe. Gosh!

Maisha ya CHADEMA kama chama kikuu cha Upinzani yako ukingoni.

Waingereza wana msemo usemao, ''Beware the last kicks of a dying horse''.

Swali la kujiuliza kwa sasa ni hili, Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Chama gani kitakuwa ni chama kikuu cha upinzani baada ya CHADEMA?
Kaka jaribu kutafakari mambo kabla ya kuandika.
 
Watu wakisema chadema ni mali ya mbowe wanabisha.Haiwezekani chama kikawa kinapata 200M+ kwa mwezi plus pesa wanazochangishwa wabunge kikashindwa kuwa na miradi kwa ajili ya kujiendesha.Chama kila ttz kinamuangalia mbowe,Hiki chama au saccos ya mtu binafsi.Kwa maana hiyo bila mbowe hakuna chadema.

Ukiangalia tayari kuna conflict of interest kati ya mbowe na chama.Yani chairman anafanya biashara na chama.Maelezo ya lisu ni kukivua chama nguo na kupigilia misumari hoja ya chadema ni Mali ya mbowe.
CCM wanamradi gani zaidi ya kupola mali za umma tu, sukita yenyewe imewashinda pamoja kuwa walitumia resources za umma kuianzisha
 
MAJIBU KWA TUNDU LISSU BAADA YA KUMSHAMBULIA MAREHEMU CHACHA WANGWE AKIWA KABURINI

Sehemu ya Kwanza


Kwanza nikupe hongera sana Tundu Lissu kwa kuendelea kupona maana juzi nimeona picha yako ukiwa unakata kilaji, hiyo ni ishara kuwa umepona na hutumii tena dawa, maana dawa nyingi hawashauri wakati unakunywa uwe pia unakunywa pombe, hiyo ni ishara kuwa sasa umepona kimwili (sijui kisaikolojia na kiakili) na unaweza kabiliana na hoja za kisiasa.

Nimesoma andiko lako la kumtetea mwizi wa ruzuku na dikteta aka Mwenyekiti wa kudumu wa chama chenu kama sehemu ya kupooza muamko ulio ndani ya chadema wa wanachama kuchoka chama kuongozwa kwa matakwa ya kifamilia na ya kikundi cha watu wachache, ambao sasa kwa pamoja wamekuwa wakihoji matumizi ya mamilioni ya ruzuku ya chadema na matumizi yake ambayo ni dhahiri kuwa huo ni mradi wa Freeman Mbowe wa kudumu wa kumuingizia kipato haramu kupitia kodi ya watanzania wanyonge.
Wakati nasoma andiko lako nilichefukwa sana na roho kwa kukosa kwako hekima, busara, ubinaadam, nidhamu na shukrani kwa Mungu kwa kumshambulia Marehemu Chacha Wangwe, aliyekuwa mbunge wa Tarime na Makamu Mwenyekiti Chadema Tanzania bara (kabla hamjamsimamisha kwa njia haramu wewe na genge la watesi wenzako).

Nimekuona wewe ni mtu muoga (you are a coward), ulishindwa kumkabili Marehemu Chacha Wangwe akiwa hai, leo umeamua kumshambulia akiwa amelala katika nyumba yake ya milele pale kijijini kemakorere, unamshambulia na kumdharirisha marehemu akiwa tena hayuko katika ulimwengu huu ili asiweze kujitetea na kujibu hoja zako, mlimshambulia akiwa hai, mkamvua nafasi aliyopata kwa kupigiwa kura kikatiba na wanachadema wenzake kwa njia za hila, mkamuua, bado hamjaridhika mnaendelea kumshambulia hadi leo akiwa kaburini ambako hawezi kuwajibu, hii sio tu dhihaka kwa familia ya Marehemu Chacha Wangwe bali ni tusi kwa wakuria wote na dharau isiyo na kifani kwa watu wa Tarime.
Umeibua hoja kadhaa kumshambulia marehemu Chacha Wangwe, kinyume kabisa na utamaduni wetu sisi waafrika, sisi waafrika tuna utamaduni wa kutomsema vibaya marehemu, lakini wewe sio tu umemsema vibaya bali umemzushia uongo ili kuendelea kuharibu taswira ya jina lake na kazi yake nzuri aliyoifanya angali akiwa hai. Japo mlifanikiwa kumuua bado mnahangaika na kivuli chake, na ninawaambia maadam Mungu yupo basi malipo ni hapahapa duniani, damu yake haitawaacha salama nyote mlioshiriki uovu ule.

Marehemu Chacha Wangwe akiwa hai, aliibua hoja ambazo hadi leo ndio kilio kwa wanachadema, ukabila,udikteta, matumizi mabaya ya ruzuku n.k. Kwa kuwa hamkuwa na majibu mkaanza kusema yeye ni msaliti na ametumwa na CCM, mkatumia magazeti na vyombo vingine vya habari kumchafua kwa njia zote, kwa kuwa hoja zake zilikuwa na mashiko na ni kilio cha wanachadema wengi hadi leo bado mkashindwa, mkaamua kumuondoa ili mbaki huru, na pamoja na hayo yote bado leo mnahangaika nae akiwa kaburini, kweli damu yake bado inawalilia kutoka kaburini. Muongo mmoja ‘miaka kumi’ toka kifo chake bado hoja zake zinawahangaisha hadi mnaenda kaburini kumzushia na kumnenea uongo marehemu.

Umemshambulia Marehemu Chacha Wangwe kwa hoja zifuatazo:-
  • Kuchaguliwa kwa kura nyingi.
  • Kutochangia gharama za kesi.
  • Kuhamia Dar baada ya kuwa Mbunge.
  • Kwenda Tarime kwa lift za wazungu akiwa mbunge.
  • Kuwaambia wanatarime hatogombea ubunge 2010
  • Kuhusu tuhuma za ruzuku na ukabila “uchagga” alizoibua ndani ya Chadema.
Kwa kuwa umeamua kuendeleza mashambulizi dhidi ya mtu aliyepumzika, ambaye hawezi kukujibu, na kwa heshima ‘legacy’yake unayojaribu kuendelea kuiharibu, na kwa heshima yake, ya familia yake, na ya watu wa Tarime, ambao mmefikia hatua ya kuwadharau kwa kiasi hiki naomba nijibu hoja zako kama ifuatavyo:-

  • Kuchaguliwa kwa kura nyingi.
Umesema kwamba wewe kwa mtazamo wako matatizo yalianzia kwa kuwa Chacha Wangwe alichaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge yeyote Tanzania. Huo ni mtazamo wako, ambao kimsingi uko ‘biased’. Wewe kama ulivyosema umekutana na Marehemu Wangwe 2003, sisi tulioishi nae, tunayejua harakati zake tunajua kwa nini tuliamua kumpa ushindi wa kishindo, ni kwa kuwa yeye alikuwa shujaa na mtetezi wa wanyonge, wewe huna mamlaka ya kuhoji ni kwa nini tulimpa kura nyingi maana wananchi wa Tarime hawawajibiki kwako, na kwa taarifa yako Marehemu Chacha hakuwa mshamba wa kuzuzuka kwa sababu ya kura nyingi alizopewa na wanatarime, ni mtu aliyekuwa na exposure ya kutosha.

  • Kutochangia gharama za kesi.
Kwa wewe kumshambulia Marehemu Wangwe, nimeanza kwa kusema ni kukosa utu, ubinadamu na shukrani kwa Mungu, haswa kwa jinsi alivyokuokoa wewe na shambulio lililofanyika dhidi yako, unaonyesha ni jinsi gani ulivyo jeuri na usivyo na kiburi.
Nakumbuka siku mliposhinda kesi ya rufaa dhidi ya ubunge wake iliyofunguliwa na Mh. Werema Kisyeri Chambiri pale Musoma, nilitoka Mwanza na nikaja Musoma siku hiyo ya hukumu. kwa akili ya kawaida kabisa siamini kwamba wewe kama wakili, tena wakati huo haujawa corrupt na wale jamaa na kupata vipesa, kwamba Marehemu Wangwe alishindwa kuchangia gharama za kesi hiyo. Huu ni upotoshaji wenye nia ya kuharibu jina lake. Kwa akili ya kawaida kabisa mbunge aliyekatiwa rufaa hawezi shindwa kugharamia kesi itayopelekea yeye kuangushwa ubunge. Hapa sielewi mantiki ya hoja zako, kuwa Marehemu hakuwa na uwezo wa kulipia hizo kesi hadi hata wakati akiwa mbunge ili kutetea ubunge wake?

  • Kuhamia Dar baada ya kuwa Mbunge.
Katika mashambulizi yako dhidi yake, umesema kuwa moja ya kero za wanatarime dhidi ya Chacha Wangwe eti ni yeye kuhamia Dar es Salaam baada ya kuwa mbunge. Kwanza kabisa nikupe taarifa kuwa Marehemu Wangwe hakuwa mshamba kama wewe, alifika, kuishi na kusoma Dar, na nje ya Tanzania wewe bado ukiwa kijijini kwenu. Hivyo kuleta hiyo ni kama kuonyesha kuwa ubunge ndio ulimpa uwezo wa kuishi Dar.

Kwanza wewe u nani hadi umpangie mtu mahala pa kuishi? Wabunge wangapi wa chadema wasioishi Dar? Mbona pamoja na kihelehele chako hujawahi waambia wakaishi majimboni? Wewe mwenyewe toka uwe mbunge mbona hujarudi kuishi jimboni kwako? Mbona umeamua kuzeeka na unafiki na hadi unataka kuishi nao hadi uende nao kaburini?

Pili unapotosha kuwa Marehemu Wangwe alihamia Dar, huo sio ukweli hata kidogo kwa sababu katika jimbo la Tarime alikuwa na miji (nyumba) tatu, Kemakorere, Rebu na Bomani. Pia alikuwa na mji Dar, na alikuwa na nyumba pia Dodoma, na zote hizi ni kumuwezesha yeye kutekeleza majukumu yake kama mbunge. Wakati huo serikali nzima ilikuwa Dar, kwa hiyo ulitaka akija kushughulikia na kufuatilia miradi ya Maendeleo afikie nyumba ya kulala wageni? Alikuwa na mji kurahisisha yeye kufanya majukumu yake ya kibunge na sio kama unavyopambana na kumchafua kuwa alihamia Dar. Mtu akisoma upotoshaji wako ataamini kuwa huyu ndugu alifunga vilago na kukimbia jimbo, muogope Mungu wewe Lissu, na uwe na kiasi, wewe ni binaadam na hujafa hujaumbika. Mbona husemi kuwa alihamia Dodoma kwa kuwa alikuwa na makazi Dodoma? Pili wewe ni mwanasheria gani unayehoji mtu kuwa na makazi sehemu nyingine ya jamhuri? Ina maana unaingilia mipaka ya mtu na kutaka kumuamulia mtu pahala pa kuishi.

  • Kwenda Tarime kwa lift za wazungu akiwa mbunge.
Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi, tena ajabu mtu anapomtukana mtu aliyenyamaza milele. Eti Lissu unasema Marehemu Mbunge wetu alikuwa anakuja Tarime kwa lift za wazungu, lol. Wacha nishangae kama watu wa mjini. Maneno haya kama nilivyotangulia kusema awali sio tu ni matusi kwa marehemu bali ni matusi makubwa zaidi kwa wanatarime kwamba Mbunge wao alikuwa hana uwezo wa kupanda ndege hadi apate lift za wazungu. wewe ndio ulikuwa unamsindikiza kupanda ndege za wazungu?. Sisi tunatambua mchango wa marehemu Wangwe katika kutafuta haki ya wananchi wa Nyamongo na Tarime kwa ujumla kupitia mgodi wa Nyamongo, wewe unasema ulikuja kutetea wanatarime mwaka 2003 (tena usirudie kusema ulikuja, sema uliletwa, nitaelezea hapo chini kidogo), lakini kwa taarifa yako toka mwaka 1998 baada ya mgodi wa Placer Dome kuanzishwa Nyamongo, Marehemu Wangwe amekuwa akiwapigania wananchi, na hadi siku anafariki alikuwa na hoja binafsi bungeni ‘VUGUVUGU LA ARDHI’ ambao ulikuwa na lengo la kutetea wananchi wenye migogoro ya ardhi na wawekezaji kama wa Nyamongo ili wananchi wapate haki zao.

Dhamira ya dhati ya Marehemu Chacha Wangwe katika kutetea wananchi, isiyo na unafiki na kutumiwa na wazungu kama wewe kibaraka ndio imepelekea watu kuendelea kumuenzi kutokana na kazi aliyoifanya Tarime, rudi tena ukasoma historia yake na harakati zake Tarime. Miaka kumi baada ya kifo chake bado mnapambana kuharibu jina (image) yake, hakika mtaendelea kushindwa, maana mwangwi wa alichokipigania na kukitetea unaishi hadi leo.

Maneno yako kujaribu kuwaaminisha watanzania kuwa Marehemu Wangwe aliungana na wazungu kuwakandamiza wananchi, leo kama una kifua nenda pale Tarime na uyaseme uone kama utatoka ukiwa hata na ukucha, maana wananchi wanajua jinsi Wangwe alivyojitoa kuwatetea hadi mauti yanamkuta. Hivyo na pamoja yuko kaburini bado huwezi ondoa ukweli wa juu ya ushujaa wake, wivu wako endelea kukaa nako huko ubelgiji, una wivu ambao hata wanawake hawana.

Wewe unasema ulikuja kuwatetea wanatarime mwaka 2003, na kauli hiyo unairudia mara kwa mara kwamba wewe umekuwa mtetezi wa rasilimali hasa madini Tanzania, kitu ambacho huwa huwaambii watanzania ni kuwa ulikuwa unawatetea kama nani, unapenda sifa na ushujaa hata katika vitu ambavyo sio vyako. Unachoshindwa kuwaeleza watanzania ni kuwa wewe ulikuwa mwajiriwa wa LEAT, NGO inayoshughulika na mazingira, bila wao kukupa jukwaa (platform), na kukupa mshahara na kukutuma leo usingesema hayo, ila kwa unafiki na ubinafsi huwa unajitwalia utukufu peke yako bila kutambua mchango wa LEAT na timu yake katika hizo kazi unazojivunia kila siku. Kama risasi ulizopigwa hazijakupatia umaarufu basi usitafute umaarufu kupitia mtu aliye kaburini.

Baada ya mgodi wa Palcer Dome kuanza shughuli zake Tarime, Marehemu Chacha Wangwe aliajiriwa kama afisa mahusiano, akapewa nyumba nzuri, akapewa posho nene, akapewa gari nzuri. Lakini pamoja na hayo yote aliendelea kuwatetea wananchi wapate haki zao kupitia rasilimali hizo. Jambo lililopelekea mgodi umpe chaguo la kufanya, ama aendelee na kazi au aache kuwatetea wananchi, Marehemu Chacha Wangwe aliamua kuacha kazi, gari, nyumba nzuri na posho na mshahara mkubwa na kuamua kuwa upande wa wananchi katika kupigania haki zao. Kwamba unataka kuwaaminisha watanzania kuwa Chacha Yule aliyeacha mshahara mnono na marupurupu kibao huku akiwa hana kipato kingine na kuamua kuwa upande wa wananchi eti leo baada ya Mungu kumfanikisha kuwa mbunge na mwenye kipato kizuri kuwa atawasaliti wana Tarime na kuketi meza moja na watesi wa wananchi? Muogope Mungu wewe binadamu. Tofauti na wewe ambaye ulipewa jukwaa na LEAT kuwatetea watanzania na baada ya kufika bei kwa wazungu ukawatekeleza wananchi na hadi leo umekuwa kibaraka wa kuwatetea wawekezaji wanyonyaji katika sekta ya madini baada ya kulambishwa rushwa (hili nitalieleza kwa undani makala ijayo ili watu wakuelewe vyema zaidi)

Wewe unajidai leo unaijua Chadema kuliko Marehemu Wangwe, kwa taarifa yako tu ni kuwa wakati wewe hujajiunga NCCR-Mageuzi tayari yeye alikuwa mwanachama wa CHADEMA na mwaka 1994 aligombea udiwani kwa tiketi ya Chadema, na kama sio figisu basi alikuwa ameshinda. Wewe umejiunga Chadema baada ya NCCR-Mageuzi kuyumba ila una kihelehele kuliko hata Mzee Mtei aliyeianzisha.

  • Kuwaambia wanatarime hatogombea ubunge 2010
Huu ni mwendelezo wa majungu yako, una kihelehele utafikiri wewe ndio msemaji wa wanatarime. Hakuna mkutano wowote ambao Marehemu Wangwe aliwahi waambia wanatarime kuwa hatogombea Ubunge 2010, kwa jinsi ulivyo mzushi ukirudi nakushauri ujiunge na shirika la wambea duniani ‘SHILAWADU’. Mimi ni mwana-Tarime, na wanatarime wengi hawana hizi taarifa ila wewe unazo, usijipendekeze kwa kiwango hicho kwetu. Huu ni uongo wako mwingine na kushauri kuwa umekua na uache uzushi, tena wa kumzushia marehemu ambaye hana uwezo tena wa kuandika, huna aibu hata kidogo pamoja na kuwa na umri mkubwa namna hiyo.

  • Kuhusu tuhuma za ruzuku na ukabila “uchagga” alizoibua ndani ya Chadema.
Hizi tuhuma ndani ya Chadema ni tuhuma za kweli na hazina uongo hata kidogo. Baada ya Marehemu Wangwe kupambana na hizi tuhuma aliungwa mkono na wanachama wengi kwa sababu ndio ukweli uliomo ndani ya chadema. Wakati huo Chadema ilikuwa ikipokea ruzuku ya milioni 66 kwa mwezi tofauti na wewe unavyojaribu kupotosha kuwa ruzuku ilikuwa haifiki milioni 50.

Na wakati huo Chadema ilikuwa na wabunge watano (5) wa kuchaguliwa majimboni, na wabunge sita (6) wa viti maalum. Ambapo katika wabunge sita (6) wa viti maalum, ambao walipaswa kutoka sehemu mbalimbali za nchi ili kuleta uwiano mzuri lakini hilo halikufanyika, bali wabunge watano wa viti maalum kati ya sita walitoka mkoa wa Kilimanjaro pekee, na jambo la aibu zaidi ni kuwa kati ya hao wabunge sita wa viti maalum, wabunge watatu walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mwenyekiti wenu, utamaduni ambao ameuendeleza hadi leo ndani ya Chadema wa kutoa wabunge wa viti maalum kwa rushwa ya ngono na sasa amefikia hadi hatua ya kuzaa nao kabisa.

Wakati Chadema ikiwa na hiyo ruzuku ya milioni 66, sio wewe tu bali hata Mwenyekiti Mbowe mlikuwa mnaweza chukua hadi miezi sita hamjakanyaga ofisi za makao makuu pale mtaa wa Ufipa. Kwa taarifa yako matumizi mengi ya ruzuku yalikuwa yakifanyika ofisi za Club Bilcanas, na mimi, Mwenyekiti Mbowe na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wakati huo Bwana Anthony Komu mara kadhaa tulikaa kupanga bajeti ya matumizi ikiwemo na mikakati ya kutafuta fedha. Hata akaunti iliyotumika kukusanya michango baada yaw ewe kushambuliwa niliifungua pale CRDB Mbezi beach. Hivyo nafahamu ulaji wa ruzuku unavyofanyika ndani ya Chadema.

Labda nikugusie kidogo, umejaribu kusema kuwa Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali (CAG) anawaonea Chadema kwa kusema kuna matumizi mabaya ya ruzuku, labda kwa uchache ili nisiandike makala ndefu nieleze kidogo kuhusu hoja hizo za CAG kwa ufupi na mfano mmoja tu.

Kampuni aliyosema CAG kuwa iliingiziwa bilioni mbili (2,000,000,000/=) kwa kufanya matangazo inaitwa Milestone Int Limited, ni kampuni ya Freeman Mbowe ambaye wakati ananitambulisha mwaka 2008 kwa shemeji yake, Bibi Kineneko Mtei tukiwa Club Bilcanas (ofisini), alinieleza kuwa “huyu ni Kineneko Mtei, shemeji yangu na Mkurugenzi wa Kampuni yangu ya Matangazo ya nje (Outdoor Advertising). Hiyo ndio kampuni ambayo imekuwa ikikwapua mabilioni ya ruzuku zinazoingia kuwa inafanya matangazo, kwa uelewa wangu kampuni hii ilikuwa na bango moja tu la ukubwa wa 3*6 lililokuwa nje ya maegesho ya magari ya Club Bilcanas, na siku hizi halipo. Sasa kama kampuni inalipwa kwa kufanya Outdoor Advertising na haina mabango, na Mwenyekiti kashindwa kuthibitisha matumizi halali ya hizo pesa asiseme? Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa hoja za CAG dhidi ya Chadema pekee ndio sio za kweli ila dhidi ya CCM na dhidi ya serikali ndio za kweli?

Kwa sababu ya kutowachosha wasomaji niishie hapa kwa leo, kwa kuwa kuna muendekezo wa makala hii nitaandika zaidi tena kuhusu hili na kwa mifano. Hivyo hoja ya ukabila na matumizi mabaya ya ruzuku ndani ya Chadema ni kweli kabisa na Marehemu Chacha Wangwe aliipigania hadi mauti ilipomkuta, na aliposhinda umakamu Mwenyekiti ruzuku ilianza kutumwa wilayani na mwezi alipofariki ruzuku ikakoma kutumwa mikoani.

NB: Nimejitahidi kujibu kwa ufupi sana nisiwachoshe wasomaji. Hii ni sehemu ya kwanza, nitaendelea na sehemu ya pili, na ikiwezekana sehemu ya tatu.

Imeandikwa na:-
Deo Meck
Aliyewahi kuwa Msaidizi wa Mwenyekiti Chadema Taifa, Freeman Mbowe.
 
Buku saba haijawahi kuwatosha unaamua kulazimisha teuzi komaa atakuona maana anampango wa kumtumbua rais wa Dar
Hii yote ni uwenyekiti wa Mbowe ndio unaowatoa jasho.

Lumumba wanafanya kadri iwezekanavyo kuokoteza watu waliokuwa Chadema kujifanya "wanayajua ya Mbowe" hivyo kuonekana Mbowe hafai.

Kwa haya mashambulizi ya Lumumba kwa Mbowe basi inaonesha hakuna Mwenyekiti wa Chama wanayemuogopa kama Mbowe.
 
Ndani ya chadema ni wizi mtupu.

Hamna kipindi ambacho chadema ilichangiwa fedha nyingi na wapenda mabadiliko kama kipindi cha uchaguzi mkuu 2015, lakini mpaka leo hamna report ya mapato na matumizi ya fedha hizo!
Badala yake vyombo vya habari vilimripoti Mbowe akitorosha mabilioni ya pesa kwenda nje ya nchi tukiwa mwishoni mwa uchaguzi huo!!.
Yote haya yanatokea hamna bawacha ,bavicha wala mnywa madawa yoyote wa kuhoji wizi wa michango ya wanachama mchana kweupe kiasi hiki !
 
Kwan Lissu hoja yake ilikuwa kumshambulia marehem Wangwe, au ufafanuzi juu ya visingizio vya wanaohamia ccm kwa kumshambulia mbowe huku wakitaja sababu ni ruzuku na kuuawa kwa Wangwe?

Naona hujaoanisha mtiririko wa hoja aliyokuwa akiieleza Lissu mpaka, umeegemea kumshambulia kisa bila kuzingatia nini hoja yake kuu mpaka kumtaja marehemu Wangwe. hapa umechemka vibaya mno bwana deo kajipange urudi tena labda utaeleweka, Lissu ni level nyingine kabisa sio saizi yako broo, we kaendelee kulamba viatu vya wakubwa huko lumumba ipo siku na wewe utaukwaa udc au uras kama wenzio akina machali, kitambi, na wengine wa aina hiyo.
 
Back
Top Bottom