Maji ya Lady Jay Dee yamepigwa stop!!

Mbona watu mnashindwa kuelewa si swala la mchina mhindi au mjerumani. Maji ni mali ya taifa hamuelewi. Akitaka auze juice halafu ayaite Lady what ever....nchi zilizoendelea hutaona eti maji yana jina la mtu nani kasema hao wenye pesa hawajaliona hilo. Idara husika inafanya kazi yake sawa sawa rudisheni maji. Huu ndio mwanzo wa kutawaliwa. Mbona viwanda vya bia havijazindua hata bia moja kwa jina la mtu.

Anaitwa Judith Wambura, Lady Jay Dee sio jina lake, labda utoe sababu nyingine.
 
Mbona watu mnashindwa kuelewa si swala la mchina mhindi au mjerumani. Maji ni mali ya taifa hamuelewi. Akitaka auze juice halafu ayaite Lady what ever....nchi zilizoendelea hutaona eti maji yana jina la mtu nani kasema hao wenye pesa hawajaliona hilo. Idara husika inafanya kazi yake sawa sawa rudisheni maji. Huu ndio mwanzo wa kutawaliwa. Mbona viwanda vya bia havijazindua hata bia moja kwa jina la mtu.
Hehehe unasoma darasa la ngapi?
 
Ukibadilisha brand unatakiwa kufata taratib za usajili upya.. ni kama kubadilisha jina la mtu unatakiwa kuapa maakamani upya. Mbona vtu simpo tu.. Waacheni TFDA wafanye kazi yao.. big up kwao
 
jaydee_water_stop.jpg

Mamlaka ya udhibiti wa Chakula na madawa TFDA jana imetoa tamko la kuzuia utumikaji wa maji ya Lady Jaydee mara moja baada ya taratibu za usajili wa maji hayo katika mamlaka hiyo kutofuatwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wahusika mamlaka hiyo imetoa agizo kwa kampuni inayotengeneza maji hayo A-One products & Bottlers ambayo ni kampuni tanzu ya Mohammed enterprises kuzuia na kutengeneza pamoja na kurudisha kiwandani chupa zote zenye maji hayo
Taarifa hiyo ilisema maji hayo ya Lady Jaydee yalizinduliwa siku ya Alhamisi iliyopita katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Paradise jijini bila kufuata tarartibu husika za usajili wa bidhaa zozote zinazolika ama kunywewa.

Taarifa zaidi kutoka kwa wakurugenzi wa mamlaka hiyo ya chakula na madawa inasema mbali ya kuamuru chupa hizo kurudishwa mamlaka hiyo imetawanya sehemu mbali mbali wakaguzi wake ili kuzuia usambazaji au uuzaji wa chupa ambazo tayali zilishaingia sokoni au kwenye maghala ya kuhifadhi vitu.

Ni kosa na hairuhusiwi kisheria kwa mtu yeyote kuzindua, kutawanya au kuuza bidhaa ya chakula ama kinywaji bila kupata idhini ya mamlaka hii ya TFDA alisema mkurugenzi wa Chakula bwana Raymond Wigenge.
Sisi tulipata taarifa ya kuwapo kwa maji hayo tarehe 31 ya mwezi wa kumi na mbili 2010 na kuanza kufuatilia kwa watengenezaji pamoja na mawakala wao wa usambazaji wa maji hayo.

Tukimnukuu bwana wigenge alisema "Ilibidi kuchukua hatua za za haraka kusimamisha uzalishaji ikiwemo kuzirudisha chupa zote na kusimamisha matangazo ya promosheni ya bidhaa hiyo ya maji na pia kuwapa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya kuendelea kuzalisha maji hayo.

Alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo mume wa Lady Jaydee ambaye ndio meneja wake alikiri kupokea taarifa hiyo na kusema mchakato wa kufuata utaratibu wa usajili katika mamlaka husika tayari umesha anza na hivyo wanategemea hautapita muda mrefu uzalishaji wa maji hayo utaendelea.

Source:Bongo5
kama magufuli na serikali yake ni wazalendo haswaa ningependa kuona wakimpa support huyu mzawa na maji yake yauzike.. sio kila siku mnawapa wahindi tu kiki. wazawa mnawamaliza na vikwazo kibao.
 
Kiiruuuu! kuanzia leo nitakuwa makini kusoma tarehe ya "siledi", kumbe ni thread ya mwaka 2011!!!!
 
kama magufuli na serikali yake ni wazalendo haswaa ningependa kuona wakimpa support huyu mzawa na maji yake yauzike.. sio kila siku mnawapa wahindi tu kiki. wazawa mnawamaliza na vikwazo kibao. mlaaniwe
Wacha kukurupuka na nyuzi za miaka kibao, pia pitia comments uone kipi kilikwamisha mchakato,sio kila kitu mnalaumu tu, alaa
 
Sisi tulipata taarifa ya kuwapo kwa maji hayo tarehe 31 ya mwezi wa kumi na mbili 2010

Hii ni aibu kwa serikali kwamba tangu 2010. Hata kama imekosewa kuandikwa ikawa pia labda ni 2016.. ni muda mrefu sana wao kuja kuongea leo.

Majipu yamejaa bado
 
Back
Top Bottom