Maji ya bomba Makambako ni machafu na mamlaka ya maji (NJUWASA) ipo kimya

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049

Hii video nimeirekodi leo hii Januari 10, 2024 nikiwa maeneo ya Shule ya Mwembetogwa, Wilayani Makambako Mkoani Njombe.

Hivi ndivyo uhalisia wa maji ulivyo kuhusu Makambako na viunga vyake mfano maeneo ya Lupila na Kitisi.

Mimi ni mgeni eneo hili nina miezi kadhaa lakini tangu nimefika sijawahi kuona maji ya bomba yanayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Njombe (NJUWASA) yakiwa masafi, nimelazimika kuwa nanunua maji ya dukani kwa ajili ya kunywa kila siku.

Kuna mwenzangu mmoja aliamua kunywa maji hayo ya bombani kama baadhi ya wenyeji wanavyofanya alichokipaya amesema hatarudia tena, aliumwa tumbo balaa.

Changamoto hiyo imefikia hatua maji masafi ya Lita 20 yanauzwa kwa Shilingi 10,000.

Sasa fikiria ukiwa na familia na unahitaji wote wanywe maji masafi unadhani gharama yake itakuwaje.

Nifupishe tu kuwa maji ni machafu na kibaya zaidi maafisa wa NJUWASA wengi wao hawafiki kwenye mita husika kuzisoma kwa ajili ya bili, wao wanatengeneza kwa kukadiria, hivyo uwe umetumia au hujatumia bili inakuja kila mwezi.
 
Njuwasa wapo mji wa njombe makambako ni makuwasa bwana
 
Back
Top Bottom