Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,141
Faida za kunywa maji ya kutosha
Kunywa maji safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza kuyaboresha maisha yako na kukufanya ujihisi mwenye afya na furaha zaidi . Kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi. Tukichukulia kunywa maji ya kutosha ni mithili biashara kati ya wewe na afya yako, biashara hii inalipa.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji ya kutosha .
Pia kunywa maji ya kutosha kunaongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.
Unaweza kuboresha sura na mguso wa ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha kwani maji yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi .
Pia ongezeko la ufanisi wa figo na ini kutokana na kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa mazao ya mafuta ya ziada mwilini. Maji hayaongezi nishati mwilini, kwa hiyo unywapo maji badala ya juisi,soda au vyakula au vinywaji vingine ambavyo huongeza nishati au mafuta mwilini unaongeza uwezekano wa kupungua uzito.
"Usinisingizie Mimi Mzizimkavu Sijasema ushindie maji asubuhi mpaka jioni."

- kusaidia mmeng'enyo wa chakula.
Pia kunywa maji ya kutosha kunaongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.
- Dawa ya maumivu ya kichwa.
- kuboresha afya ya ngozi.
Unaweza kuboresha sura na mguso wa ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha kwani maji yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi .
- kusaidia akili yako.
- kutatua tatizo la kukaukiwa haja kubwa (constipation)
- kuboresha hali ya viungo na misuli
- kuondoa uchovu
- kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa.
- Maji yanaweza kusaidia katika kupunguza uzito.
Pia ongezeko la ufanisi wa figo na ini kutokana na kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa mazao ya mafuta ya ziada mwilini. Maji hayaongezi nishati mwilini, kwa hiyo unywapo maji badala ya juisi,soda au vyakula au vinywaji vingine ambavyo huongeza nishati au mafuta mwilini unaongeza uwezekano wa kupungua uzito.
"Usinisingizie Mimi Mzizimkavu Sijasema ushindie maji asubuhi mpaka jioni."
- maji ni kiburudisho