Umuhimu wa maji katika mwili wa binadamu

Dr James G

Senior Member
Oct 16, 2016
147
242
Umuhimu wa maji katika mwili wa binadamu ni mkubwa sana tofaut na binadamu tunavyochukulia,watu wengi wanakunywa maji kwa mazoea,inashangaza watu hawajui maji ndio kinywaji cha kwanza kuubwa na Mwenyezi Mungu kutokana na umuhimu wake wa kusafisha mwili,na kuufanya mwili kutoishiwa au kupungukiwa maji(dehydrated).

Mwili wa binadamu umeubwa na uhitaji wa maji wa asilimia 70%, ili kuufanya mwili na akili kufanya kazi vizuri.

Maji safi na salama yana kazi ya kutoa sumu mwilini,kuupa mwili akili na nguvu ya kufanya kazi ,kupunguza mwili uzito ulio pita kiasi(lose weight) nk.

Kama tutakula mlo kamili,kupata muda wa kupumzika,kufanya mazoezi na kunywa maji ya kutosha basi tutakua na mwili usiosumbuliwa na magonjwa ya mara kwa mara.

Kutokana na ripoti ya taasisi ya afya ya Mayo clinic,mwanaune anatakiwa kunywa vikombe kumi na tatu 13 vya maji sawa na lita 3 ya maji kwa siku.na mwanamke anatakiwa kunywa vikombe 9 vya maji sawa na lita 2.2 ya maji kwa siku.

NB:Make as much water as you want.H2O.
 
Kunywa maji mengi pia sio vizuri kwa afya yako kijana, everthing toomuch is harmfull.
Kunywa unapohisi kiu, kunywa kidogo sana pale usipohisi kiu.

Kugugumia hayo malita kwa siku sio njema kiafya pia.

Hizo lita ziko calculated kaka ni kwel kila kitu kipo kwa kiasi lkn maji hutaki kunywa tu unapohisi kiu ,maji ni muhimu ,Kama usipo sikia kiu kwa siku hutakunywa maji kabisa na utawezaje kupata 70% ya maji yanayotakiwa kwenye mwili wako ?
 
Kunywa maji mengi pia sio vizuri kwa afya yako kijana, everthing toomuch is harmfull.
Kunywa unapohisi kiu, kunywa kidogo sana pale usipohisi kiu.

Kugugumia hayo malita kwa siku sio njema kiafya pia.

Wapo wagonjwa ambao kutoka na maradhi yao ya kimfumo huwa wanashauriwa kupunguza kiwango cha maji kwan unakuta mifumo yao hairuhu Taka mwili kutoka nje kwa njia ya Kukojoa ,lkn ni had Ushauriwe na wataalamu mbali na piga maji kwa uwezo wa mwili wako sio had upate kiu
 
Maji yanaendana na kilograms zako mkuu, sio tu kwamba ukijisikia kiu ndo unatakiwa unywe maji
 
Asubuhi nikiamka nina kikombe cha nusu lita nakikata, baadae nikipiga tea nanunua maji ya lita 1, mpaka lunchtime hayapo, saa 8 hv nadaka mengine ya lita1 mpaka muda wa kurudi home yameisha, nikifika home najaza kabisa kikombe changu cha nusu lita mpaka muda wa kulala kimeisha, hiyo ni ratiba daily
 
Wapo wagonjwa ambao kutoka na maradhi yao ya kimfumo huwa wanashauriwa kupunguza kiwango cha maji kwan unakuta mifumo yao hairuhu Taka mwili kutoka nje kwa njia ya Kukojoa ,lkn ni had Ushauriwe na wataalamu mbali na piga maji kwa uwezo wa mwili wako sio had upate kiu
Nashangaa mtu ananunua maji ya lita1 asubuhi hadi jioni, yaani hayo nikiweka mdomoni nikishusha yapo katikati, maji ni dawa kubwa sana ni vile watu hawajui tu
 
Asubuhi nikiamka nina kikombe cha nusu lita nakikata, baadae nikipiga tea nanunua maji ya lita 1, mpaka lunchtime hayapo, saa 8 hv nadaka mengine ya lita1 mpaka muda wa kurudi home yameisha, nikifika home najaza kabisa kikombe changu cha nusu lita mpaka muda wa kulala kimeisha, hiyo ni ratiba daily

Naamin kwa unywaji huo Tatzo la nguvu za kiume sio shida kwako,watu hwajui maji yanasiaidia Damu iweze kusafir vzr sehem mbali mbali za mwli ,na Taft ndogo niliyofanya yanasaidia sana hata wakati wa tendo la ndoa
 
Nashangaa mtu ananunua maji ya lita1 asubuhi hadi jioni, yaani hayo nikiweka mdomoni nikishusha yapo katikati, maji ni dawa kubwa sana ni vile watu hawajui tu

Hata watu wanaosumbuliwa na Matatzio ya Ngozi au chunusi wanatakiwa kunywa maji tu,maji ni Tiba maji ni tiba maji ni tiba
 
Inategemea na ratiba ya siku hasa nikiwa sehemu ambayo sitaki kwenda kukojoa mara kwa mara, ila nikishinda geto kukata 3L and more ndo routine, siku nyingine 2L everyday
 
Ebu tupe Faida unazopata ukipiga maji mengi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom