Majeruhi ajali za bodaboda tishio, MOI hupokea wagonjwa 280 kwa mwezi

Wangezikataa kama baadhi ya Nchi Serikali itafute maeneo iwekeze kwenye kilimo kweli ikiwezekana hao vijana wapewe ajira huko ila sio kwa boda boda tutakua na Taifa lenye vilema wa ajali wengi sana huko baadae ni vile wengi wanaoshauri wanatumia maneno ya dhihaka ila ukweli boda sio suruhisho kwa ajira ya vijana...
 
60% ya boda boda hawana leseni.

Wengi hujifunzia mitaani

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Na watakufa sana, maana akikamatwa anatoa alizokusanya na kama hana anakimbia mpaka anapandilia korongo au kuuvaa mti kabisa

Sijui tulaumu nani hapa maana kuna wenye tamaa ya kujenga baada ya miaka 2 tu na hao wanaotafuta riziki
 
Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imekiri kupokea majeruhi wa ajali za bodaboda wastani wa watu 9 hadi 10 kwa siku ambapo ni sawa na 70 kwa wiki na 280 kwa mwezi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye mafunzo ya kimataifa ya matumizi ya mashine za upasuaji yaliyoandaliwa na Taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha Weill Cornell Medicine cha New York nchini Marekani, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface amesema kuna ongezeko la ajali hususan za pikipiki ambazo zinasababishwa na kutofuatwa kwa sheria za barabarani ambapo wahanga wengi hawavai kofia ngumu (Helment).

“Kuna ongezeko la ajali kwa asilimia 5 hadi 6 kwa mwaka ambapo kwa siku tunapata majeruhi wa ajali za barabarani 10 hadi 15 kati ya hao 10 ni bodaboda kwa mwezi ni 350 hadi 400 ambao wa bodaboda ni 280,” amesema Respicious.

Daktari Bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kutoka MOI, Dk Hamis Kimaro amebainisha kuwa wagonjwa wengi wa upasuaji walioumia vichwa, mgongo wanatokana na ajali za barabarani ambao wanachukua robo tatu ya wagonjwa wote wa upasuaji.

“Changamoto kubwa tunayoipata kwa wagonjwa wa majeruhi wa ajali wengi wakija hawana ndugu wa kuwahudumia, hawana kadi ya bima hawana hela mfukoni, hii imekuwa changamoto kwa sababu ni zaidi ya asilimia 75 na taasisi ndiyo inayoingia gharama za kuwahudumia,” Dk Kimaro.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Chuo kikuu kishiriki cha MOI, Dk Victor Meza amesema imekuwa ni muhimu kwa wao kupata ujuzi huo ambapo yatafanyika kwa siku tano, mbili zikiwa za darasani na tatu zikiwa za vitendo kwani watapata elimu na uzoefu wa kutosha kuweza kuwahudumia wahitaji wa upasuaji ambao wengi wao wanatokana na ajali.

Chanzo: Mwananchi
 
Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imekiri kupokea majeruhi wa ajali za bodaboda wastani wa watu 9 hadi 10 kwa siku ambapo ni sawa na 70 kwa wiki na 280 kwa mwezi.
Boda kazi ya laana watamuelewa Lema wakiwa wamepotea wengi sana, anajaribu kuwatetea,lakini anawatetea watu wasioelewa.
 
Swali rahisi ambalo alihitaji elimu ya chuo

Hao bodaboda wakiacha iyo kazi mtaweza kuwaajiri........na kama mtashindwa kuwaajiri je kuna picha gani inakujia kichwani baada ya kuto waona bodaboda kwenye vijiwe vyao na barabarani
 
Mbona sioni Hoja inayoeleza Kuwa Bora Bora wengi Leseni zao ni za mchongo , zinapatikana bila ya wao kushiriki mafunzo , .

Lipa laki 2 chukuwa Leseni utajua wewe na jamii yako .

Boda boda ni silaha ya maangamizi
 
Back
Top Bottom