Majambazi ya DRC yaua askari wa Tanzania ziwa Tanganyika, OC-CID apigwa risasi kifuani

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Wanajami, leo mchana kumetokea mapigano makali kati ya askari wa jeshi la polisi na Jwtz kwa upande mmoja na majambazi kutoka congo. Katika mapigano hayo Oc-cid wa Kigoma bwana Mohamed Kilonzo amepigwa risasi kifuani pamoja na askari polisi mwingine amepigwa risasi ya shingo. Kwa upande wa Jwtz, askari mmoja kavunjwa miguu, mwingine risasi imeingia kiunoni na mwingine kapigwa mkononi. Hadi ninapoleta taarifa hii, majeruhi wapo theatre takribani masaa manne sasa na madaktari wanaendelea kufanya jitihada za kuwasaidia. Na kwa upande wa adui, habari zilizopo ni kuwa wote wameuawa. Chanzo cha tukio hili ni kuwa majambazi hao kutoka Congo kumteka raia wa Tanzania na askari wetu kutaka kumuokoa. Tuombe Mungu awaponye


Updates:

FIKRAPEVU: Majambazi wa DRC waua polisi wa Tanzania ziwani, JWTZ wajeruhiwa

ASKARI mmoja wa Tanzania amepoteza maisha baada ya kutokea mapigano katikati ya Ziwa Tanganyika kati ya majambazi yenye silaha toka nchi jirani na askari wa Tanzania wakiwamo polisi na wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Taarifa zilizoripotiwa katika mtandao wa JamiiForums.com na kuthibitishwa na polisi zimeeleza kwamba askari wa Tanzania akiwamo Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kigoma Mohamed Kilonzo, walikwenda kumuokoa Mtanzania aliyetekwa na majambazi hayo na kutokea mapigano hayo.

Katika tukio hilo majambazi wote sita waliuwawa na askari mmoja wa Tanzania alifariki kutokana na majeraha makubwa wakati wengine sita wakiwamo askari wa JWTZ walijeruhiwa baadhi yao vibaya sana.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Frassa Kashai, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea taarifa tukio hilo baadaye, kwa kuwa wakati huo walikuwa wakishughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuwahudumia majeruhi na kufuatilia usalama wa eneo hilo.

Taarifa katika mtandao wa JamiiForums.com zilizotumwa na mwanachama wa mtandaoa huo mwenye jina la KAUMZA zilieleza;
"Leo mchana kumetokea mapigano makali kati ya askari wa jeshi la polisi na JWTZ kwa upande mmoja na majambazi kutoka Congo (DRC). Katika mapigano hayo Oc-cid wa Kigoma bwana Mohamed Kilonzo amepigwa risasi kifuani pamoja na askari polisi mwingine amepigwa risasi ya shingo. Kwa upande wa JWTZ, askari mmoja kavunjwa miguu, mwingine risasi imeingia kiunoni na mwingine kapigwa mkononi.

"Hadi ninapoleta taarifa hii, majeruhi wapo theatre takribani masaa manne sasa na madaktari wanaendelea kufanya jitihada za kuwasaidia. Na kwa upande wa adui, habari zilizopo ni kuwa wote wameuawa. Chanzo cha tukio hili ni kuwa majambazi hao kutoka Congo kumteka raia wa Tanzania na askari wetu kutaka kumuokoa. Tuombe Mungu awaponye"


Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea huku ukifuatilia: Mapigano katika Ziwa Tanganyika

http://www.fikrapevu.com/habari/maj...ika-polisi-wa-tanzania-auwawa-jwtz-wajeruhiwa
 
tuwaombee mungu makamanda hawa na wote wale wenye jukumu la kuilinda nchi na wananchi wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania.
 
cdhan km TANZANIA inacondact military drill za kutosha kwa majeshi yetu.....kuna haja sasa ya military drill zifanyike mara kwa mara ili majeshi yetu yawe na hari ya utayari kuliko kushitukizwa lasivyo maafa yatakua makubwa
 
Bro. hii taarifa ni kubwa, Rekebisha hiyo Titre yako. weka neno 'Ziwa Tanganyika' ili ieleweke vizuri. Mungu awasaidie hao makamanda wetu waweze kupona.
 
Bro. hii taarifa ni kubwa, Rekebisha hiyo Titre yako. weka neno 'Ziwa Tanganyika' ili ieleweke vizuri. Mungu awasaidie hao makamanda wetu waweze kupona.

na hiyo uliyo andika na wewe ni nini!coloured
 
Daah! its so sad, ila Mungu atawapa ahueni wote waliojeruhiwa katika tukio hilo na kurejea katika hali zao za kawaida. Tuzidi kuwaombea Watanzania wenzetu.

Serikali nayo inatakiwa kuwa makini kidogo na matukio ya aina hii yanayojitokeza ktk mipaka yetu, kama watu wanaweza kuingia hadi ndani ya mipaka ya nchi yetu kuteka raia na kutaka kuondoka nao hii inamaanisha sisi kama raia hatupo salama hata kidogo ndani ya nchi yetu.

Haya ni matokeo ya kila kitu kuendeshwa kisiasa nchini ambapo vyombo vya ulinzi na usalama kazi yake kubwa kuwashikisha adabu wapinzani na kuwalinda viongozi wa serikali badala ya kuwalinda Watanzania wote.
 
Iweke vizuri kwani hii itawachanganya wana jamii.
1.Inaonekana hapa kuna vita vya aina mbili, moja ni askari wetu wenyewe kwa wenyewe yaani TPDF(JWTZ) na PF (POLISI)
2.Inaonekana hapa kuwa vita vya pili ni kati ya majambazi toka DRC wakipambana na Polisi wetu....Ni hivyo?
 
Acha ujinga wa kishamba na wewe mbwa kwani hujawahi kukosea kuandika?watu tunaumia kusikia watz wenzetu wameumia nawewe unaleta ujuaji wako hapa pambafu!
wanganyika ndo wapi? Usiwe na papara wakati unaandika!
 
Bad enough, askari wetu waliku wanatumia mitumbwi. Zana za patrol ziwani kama boti za fibre zipo na hazina mafuta. Askari wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Wapo ktk risk na vipato vyao ni duni. Serikali haiwathamini kabisa
 
poleni makamanda wetu, kweli mazingira ya kazi yenu si kama ya wahasibu, Mungu atawalipa kwani serikali yetu haina pesa
 
Nimeshasema sana humu, sisi hatuna jeshi, jeshi letu has been corrupted. Ma-askali wetu wanachojua ni kuiba tu kama kina Lt. Gen. Shimbo, lakini kwenyd battle field hakuna kitu, sasa wacha wafundishwe adabu hawa jeshi-ccm...
 
hawa ma_boya wanachojua ni kupiga wananchi wasio na silaha wanaoandamana kwa amani, waoneshe uwezo wako kwa wenye SMG kama wao ili tujivunie jeshi letu , zaid ya hapo they are all Pu***es
 
Back
Top Bottom