Majambazi watatu wauawa na Jeshi la Polisi Kahama, Shinyanga

Huwa nashangaa saana watu kuwatukana Polisi matusi ya nguoni hawa jamaa wanachofanya ni msaada kwetu.

Imagine mtu anasonga mbele kwenda kuweka roho rehani...je unapaswa kumlipa tshs ngapi unadhani? Lakini so far ndo watu wanaolipwa kiduchu licha ya hatari ya kazi yao lakini bado tunaendelea kuwakebehi ifike kipindi tuone Polisi wanafanya hisani kubwa tu kwetu Raia.

Pongezi kwenu wazee.
Mafunzo wanayopewa yanagharama kubwa na mbinu ni nyingi..sio kama kupiga sakadi ukutani..kinachowaudhi wengi ni hawa askari kutotumia mbinu na kuwa legelege..
 
Hakuna cha vijana wala nini watanzania tunataka kuona mkataba wa Lugumi na jeshi la polisi ukiwalishwa tujue kampuni ya Kitwanga na Kipillimba zilihusika vipi?

UKAWA sasa wamepata hoja ya kudandia maana wenyewe huwa hawana hoja zao za kuanzisha.Humu jamii forums hata ukianzisha hoja ya kilimo wao wataleta ya Lugumi.
Hoja unayojibu unachanganya maada mkuu.Ya LUGUMI kayajadili kwenye topic husika tafadhali
 
Unachojadili mbona kama unavyotaka hakipo?
 
UKAWA sasa wamepata hoja ya kudandia maana wenyewe huwa hawana hoja zao za kuanzisha.Humu jamii forums hata ukianzisha hoja ya kilimo wao wataleta ya Lugumi.
Hoja unayojibu unachanganya maada mkuu.Ya LUGUMI kayajadili kwenye topic husika tafadhali
Sasa mhusika mkuu wa LUGUMI anajifanya kuuwa majambazi wakati na yeye anatakiwa auwawe
 
Yaah!hawa watu hawafai kupelekwa kwa pilato hawa coz mtu kukuvamia anakuwa kajitoa muhanga maisha yake akili inakuwa haipo wanaua watu hovyo kupunguza kazi ya pilato na kuwahudumia kwa kodi zetu wakiwa lupango mimi kwa dhati naiunga mkono hoja yako.

Ameongea kamanda mpya Mkoa Mwanza jana kwamba hakuna sababu ya kuwajeruhi maana wao lengo ni kukuua wewe ukicheka nao itakula kwako ua alafu taratibu zingine zitafuata lakini unajua ushapunguza,,,,, Hawa hawana uzuri wowote yaan ..... Mungu aendelee kuwasaidia aisee maana hata mishahara na malimbikizo yao na yanatia hasira sana JPM anapaswa kuwafikiria upya.
 
Hiyo ilikuwa sera ya tossi pori la kimisi waqt alipokuwa kamanda kagera.
 
UKAWA sasa wamepata hoja ya kudandia maana wenyewe huwa hawana hoja zao za kuanzisha.Humu jamii forums hata ukianzisha hoja ya kilimo wao wataleta ya Lugumi.
Hoja unayojibu unachanganya maada mkuu.Ya LUGUMI kayajadili kwenye topic husika tafadhali
Kwaiyo unataka ya Lugumi yasizungumziwe?
 
Ahsante mleta mada. Kulingana na maelezo majambazi waliokamatwa wakiwa hai si walitakiwa wawe ni wawili na wala siyo mmoja? Kuna aliyejificha jengo la jirani na kisha kukamatwa akiwa hai na mwingine aliyebakia baada ya mmoja kuuawa eneo la Mhungula wakati wengine wakikimbia. Hivyo walitakiwa wawe wawili.
 
Noma sana...matukio yote hayo ndani ya mwezi mmoja? RPC shinyanga ni wa kutumbuliwa pia
 
Yani hapa maeneo ya soko jipya cdt kuna jamaa alikuwa anatoka sokoni akakutana na risasi majambazi walikuwa wanaelekea maeneo ya shule za kilima, dah! Kiukweli matukio ya ujambazi kahama yamezidi
 
Nani kasema ya Lugumi yasiongelewe? Anzisha thread yako maalum kwa Lugumi, sio unaona mwenzio kaja na hoja yake we unadandia na kuingiza mambo ya Lugumi, huo ni ung'ombe.
Mbona umepanic kama umechomwa na kitu chenye nchakali kwa nyuma?
 
Ambapo kuliibuka majibizano makali ya risasi ambapo polisi walifanikiwa kumwua jambazi mmoja na wengine kukimbia na pikipiki huku mmoja akijifungia jengo la jirani na kujibizana risasi na polisi.

Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumtia mbaroni jambazi huyo akiwa hai huku wale waliokimbia na pikipiki wakikamatwa eneo la Mhungula nje kidogo ya mji ambapo pia kuliibuka majibizano ya risasi na jambazi mmoja kuuwawa huku mwingine akikamatwa na wengine kukimbia kusikojulikana.

Mpaka kufikia mida ya SAA 1 idadi ya majambazi waliouwawa ni 2 na mmoja amekamatwa akiwa hai huku wengine wakitokomea mitaani wakiwa na silaha kali.Huku watu wanne wakijeruhiwa kwa risasi katika eneo la tukio.

Ukifanya hesabu kwa kufuata hayo maandishi yenye rangi utakuta waliouawa ni majambazi wawili na waliokamatwa na majambazi wawili....., kila alipouawa jambazi mmoja kuna mwingine alikamatwa
 
Jioni hii katika eneo la jirani na msikiti mkuu wa Ijumaa ambapo kuna maduka kadhaa ya jumla, kulitokea tukio la majambazi 6 wenye silaha za moto kuvamia maduka na kumuua mfanyabiashara mmoja aliyefahamika kwa jina la Emma na kisha kuwajeruhi watu wengine wawili.

Walipomaliza kupora duka la kwanza na kumuua mmiliki huyo waliingia duka la pili kisha kuchukua pesa na kisha kuingia duka jingine ambapo mda huo askari polisi walishapata taarifa wakafika eneo la tukio.

Ambapo kuliibuka majibizano makali ya risasi ambapo polisi walifanikiwa kumwua jambazi mmoja na wengine kukimbia na pikipiki huku mmoja akijifungia jengo la jirani na kujibizana risasi na polisi.

Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumtia mbaroni jambazi huyo akiwa hai huku wale waliokimbia na pikipiki wakikamatwa eneo la Mhungula nje kidogo ya mji ambapo pia kuliibuka majibizano ya risasi na jambazi mmoja kuuwawa huku mwingine akikamatwa na wengine kukimbia kusikojulikana.

Mpaka kufikia mida ya SAA 1 idadi ya majambazi waliouwawa ni 2 na mmoja amekamatwa akiwa hai huku wengine wakitokomea mitaani wakiwa na silaha kali.Huku watu wanne wakijeruhiwa kwa risasi katika eneo la tukio.

Nikiwa mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo nawasifu polisi kwa kuwahi kufika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu ila kosa kubwa walilolifanya ni kuja moja kwa moja na gari la polisi eneo la tukio, ambapo maduka hayo yako pembezoni mwa barabara hiyo na majambazi walipoona gari la polisi walianza kuwashambulia na kupiga tairi zote za mbele ndipo askari wakashuka na kuanza kujibizana nao kwa risasi.

Pengine askari wangeacha gari mbali na eneo hilo kisha wangezingira eneo hilo ndipo waanze kushambulia pengine wangeweza kuwakamata wote.Sikuweza kupiga picha kutokana na mazingira ya tukio hilo, ambapo milio ya risasi ilitawala kila kona.Hili ni tukio la nne tangu mwezi huu kuanza ambapo katika matukio mengine hakuna jambazi waliowahi kukamatwa.
huyo mfanyabiashara Emma kama namfahamu,ana gest kule maeneo ya phantom?
Duh,kama ndiye wamemkatiri kweli kijana mambo yake yalikuwa yameanza kunyooka sana
 
Back
Top Bottom