Majambazi wa benki na maarifa ya wizi

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Angali nilipokuwa mdogo, niliwahi kusimuliwa hii story.

__________

Wakati wa uvamizi wa benki moja, majambazi walipiga kelele kwa sauti mbele ya kila mtu "lala chini, pesa ni ya serikali lakini maisha ni yako" kila mtu alilala chini. Hii inaitwa dhana ya akili, kubadili akili za waliokuzunguka.

Wakati wanaiba fedha, mhudumu mmoja wa kike alikuwa akisita sita sana na kuogopa, jambazi mmoja akamwambia "tafadhali kuwa mstaarabu, huu ni wizi na sio ubakaji" hii inaitwa akili ya utaalamu, yaani kuwahimiza watu wafanye kile wanachopaswa kufanya tu.

Mara tu baada ya majambazi hao kuondoka Meneja wa benki alimwambia msimamizi wa benki kutoa taarifa kwa vyombo husika na kuwaita polisi haraka. Msimamizi wa benki akamwambia "subiri, hebu na sisi tuchukue kiasi fulani cha fedha kisha tuongeze deni lililoibiwa na majambazi" hii inaitwa kuogelea na wimbi. Pale ambapo hali mbaya inapokukuta basi unaendana nayo na kubadilisha nyakati kuwa njema. Meneja akasema "wazo zuri, itapendeza kama wezi watakuwa wanakuja kuiba kila Mwezi" hii inaitwa kujipa kipaumbele, yaani maslahi yako ni bora kuliko kazi yako.

Wakiwa katika makazi yao, jambazi mdogo zaidi alimfuata mkubwa wake na kumwambia tuhesabu sasa tumepata kiasi gani. Yule jambazi mkubwa akamuangalia na kumuambia "wewe ni mjinga sana, kuna kiasi kikubwa sana humu itatugharimu muda mrefu mno kuhesabu. Leo jioni taarifa ya habari itaonyesha benki imeibiwa kiasi gani nasi tutafahamu." Huu unaitwa uzoefu kazini, uzoefu ni bora sana kwenye maisha ya sasa.

Haya bwana, siku iliyofuata taarifa za habari ziliripoti kwamba kiasi cha shilingi milioni 100 kilikuwa kimeibiwa kutoka benki. Majambazi walifurahi sana, lakini walipohesabu walihesabu na kuhesabu na kuhesabu na kujikuta wana shilingi milioni 20 tu. Majambazi hao walikasirika sana na kulalamika "tulihatarisha maisha yetu lakini tumefanikiwa kuiba milioni 20 tu wakati Meneja akiwa amekaa tu aliiba milioni 80 kwa kukunja tu vidole vyake. Kweli akili ni bora kuliko nguvu na juhudi zisizo na maana". Maarifa ni ya thamani sana kuliko akili ya wizi.

•Akili ku mkichwa.

Amani Dimile

1691496805152.jpg
 
Back
Top Bottom