Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,646
Siyo kweli! Katika Baraza la kwanza la Mawaziri ambao walikuwa kumi kulikuwa Waislamu kama kina:
1. Tewa Saidi Tewa
2. Chief Abdallah Fundikiria
3. Rashidi Mfaume Kawawa
5. Amiri Habib Jamal
Sasa ubaguzi unaosemea uko alioufanya Nyerere (Mwenyezi Mungu amweke pema) uko wapi hapo?
Hawa uliowataja si ndo wale waislamu wa mwanzo waliomsaidia kumsomea dua Nyerere ili waingereza wasimfunge kwa kosa la uhani. Hata yeye alikiri kuwa waislamu walimsaidia sana na ndo chanzo cha Nyerere kuvaa balaghashia mpaka alipokuja kuwasaliti waislamu mwaka 1972. Mimi nazungumzia waislamu wapya baada ya uhuru!!!! Ukimzungumzia Tewa Saidi Tewa, huyu alikuwapo tangu enzi za upigania uhuru so ubaguzi hapa usingeweza ku-apply.
Kitu ambacho hamuwezi kukikubali ni kwamba Nyerere aliwaahidi waislamu kwamba akipata urais atawapa kipaumbele kitu ambacho hakukitekeleza baada ya kupata uhuru. Ya nyerere ni kama ya jomo kenyatta wa Kenya. Alimwahidi Jaramogi Oginga Odinga kwamba angempatia nafasi nyeti lakini hakufanya hivyo. Ikumbukwe kwamba Jaramogi alikataa vyeo kadhaa kutoka kwa waingereza mpaka Mzee Jomo atakapotoka gerezani. juhudi za Jaramogi zikafanikiwa mzee akatoka jela lakini Mzee Jommo hakutekeleza wala kutambua mchango wa Jaramogi. Ndipo kulikopelekea mgogoro mkubwa sana na kutoelewana kati Ya Mzee Jomo Kenyatta na Jaramogi Oginga Odinga. Mpaka siku moja walitukanana hadharani kiasi kwamba vrugu kubwa ikatokea na watu 23 waliuawa na polisi.
Kwa Tanzania hii ndo msingi wa waislamu kuona kuwa wanaonewa na wanadhulumiwa. Ikiwa wao ndio waliofunga na kukesha wakisoma dua kali za kung'arisha nyota ya Nyerere mpaka mzungu akachemsha (maana dua ilisomwa kiasi kwamba ukimtafuta Nyerere kwa ubaya humuoni japo unapishana naye) iweje leo uwasahau na kuwatupa? Suala hili linaangaliwa kwa upeo mdogo lakini linamadhara makubwa sana. mfano mwaka 2005 Mahakama ya kadhi ya waislamu iliwekwa kwenye ilani ya uchaguzi lakini baadaye ikafutwa maana yake unawaahidi kitu waislamu kisha unawageuka!!! Kwa kuwa jambo haliwahusu wakristo ndo maana wanasema kirahisi tu kwamba haina haja kuwa na mahakama ya kadhi eti kwamba fedha za kuendeshea hizo mahakama za kadhi zisitoke serikalini!!! Wamesahau kwamba hospitali za mission huwa zinapewa ruzuku ya serikali!!!!! Mgogoro huo ndo utaendelea mpaka siku Tanzania itakapoamua kusikiliza kilio cha waislamu ama Mungu atakapoamua.