Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,412
Mimi katika uzee wangu na ingawa siyo mwanasheria nasema majaji wetu waliotoa hukumu ya mkataba wa DP World huko mbeya sina hakika kama wanao uelewa wa kutosha juu ya ukuu wa mamlaka ya muhimili wa mahakama juu ya mambo ambayo hayaendani na katiba katika kusimamia haki katika taifa letu.
Mahakama ndicho chombo pekee chenye uhalali (legitimacy) katika kutafsiri sheria yoyote katika taifa letu.
It has the right and duty to decide wether any law or act is valid under our constitution
The constitution is what the judges say it is wala siyo bunge au rais. Hayo ninayo yasema ni kwa mujibu wa jaji mkuu msitaafu, charles evans hughes wa uingereza wa miaka hiyo.
Mahakama ni dira na daraja maalumu kati ya serikali na bunge katika usimamizi wa haki ndani ya jamii/taifa
Kuhusu hii hukumu ya bandari iliyotolewa mbeya miye nitoe angalizo tu kwa kutumia nukuu ya bwana dooley wa uingereza aliyewahi kutilia shaka heshima ya uadilifu wa muhimili wa mahakama na akasema kwamba
It is this habit we have in mind when we say, every man ought to have a right to his day in court, the day when the legal political system is focused on him and his problems as an individual.
Je , kupitia matamshi mepesimepesi tu kama ya hawa majaji kuandika na kutamka hadharani kuwa wao yaani muhimili wa mahakama eti hawawezi kuingilia muhimili wa bunge!
Je kwa tamko hilo hatuoni kuwa hawa majaji kufumbia macho baadhi ya misingi imara ya haki sasa tunalea utamaduni wa hovyo kwa kumomonyoa misingi muhimu ya uadilifu , uzalendo na utaifa na weledi, professionalism ndani ya muhimili wa mahakama zetu !
Nijuavyo duniani kote ni muhimili wa mahakama pekee ndio wenye uhalali wenye hatimiliki ya kuikataa na kufuta sheria yoyote yenye mapungufu dhahiri.
Narudia hawa majaji kwa kuandika na kusema hadharani kuwa hawana uwezo wa kingilia muhimili wa bunge kuhusu sheria kadhaa zenye ukakasi ndani ya jamii hakika sasa tanzania kitaifa tumekwisha.
Ni aibu iliyoje kwa hawa vijana wetu tunao waamini kwa kuwaita waheshimiwa kuandika na kutamka maneno hayo na mengineyo katika hukumu yao !!!
Hakuna anayepinga uwekezaji bali muhimu
Uwekezaji husika uwe wenye uhalali kisheria.
Au hao majaji ni wagonjwa wa dudu baya liitwalo
Intellectual dishonesty !!!
Kama ni hivyo na hata kwa wao kukiri kuwa mkataba huo una mapungufu kadhaa ni kwa masilahi ya nani katika taifa letu kutuambia kuwa basi hayo mapungufu yanavumilika.
Hivi wamesahau zile busara kwamba
Katika vazi la mke wa mfalme tone moja tu la shahawa sawiya adhabu ya kifo ni halali kwake huyo mama?
Tumia tafakuri jadidi tafadhali .
Nawasilisha
#UPDATE
MOJA ya majaji waliotoa hukumu hiyo ya Mbeya amepewa zawadi na kupandishwa mpaka Mahakama ya Rufani.