Majaji wa Tanzania hawajui kiingereza - Tundu Lissu

jana waziri aliposema hukumu kuandikwa kwa kiswahili ni ngumu alikosea

Mimi naona bora ziendelee kuwa hivyo hivyo kwa kiingereza

Sitashangaa kama biblia ilitafsiriwa na wazungu wanaojua kiswahili. Tafuta tafsiri za kiingereza zilizofanywa na waswahili, makosa ni mengi sana
 
Kwakweli lissu ame mwambia ukweli baada ya Hamad Rashidi kusema Capital punishment ni adhabu ya viboko!

Kwa kweli lissu katoa somo kubwa sana na ilionekana kuwaingia wabunge wote, na alisema sisi ni watumwa kama wana bisha basi katiba mpya itambue lugha ya kiswahili kama lugha ya kutumia sehemu zote!

Kwakweli bonge lote lililowa kabisa maana misumali aliyo gongelea ilikuwa ni yenyewe!

Hakuficha maneno na kusema majaji, wabunge wote hatujui kingereza!

Huo ndio ukweli hata Lissu amemchana Hamad Rashid kwamba hajui kiingereza.
 
Mbona watu wana tabia ya kukataa kuambiwa ukweli? mambo ya ajabu kabisa kwani alichokisema Mh Tundu Lissu ni sahihi.
 
vihiyo nchi hii wapo katika sekta nyingi na sio elimu ya mulugo pejke yake.
 
Naona Tundu Lisu aende mbali zaidi hadi kuna ma waziri hawajui kimombo, kama Issue ya waziri Mulugo, ni aibu kwa Taifa,
na Mpaka sasa hajaomba radhi
 
Hongera kamanda Tundu Lissu kwa kuleta ukweli mchungu,bado huyu kilaza mulungo naibu wa elim,jana jumatano asubuhi alipokuwa anahojiwa na radio one alichapia tena kwa kusema kwamba nanukuu"consultant ataangalia wenye shule binafsi kama wanatoa lunch ya mchana na dinner ya usiku"
Nyingine kipindi kitaruka jumapili saa 4:30 asubuhi akihojiwa kuna mahali anasema,nanukuu"mimi sikwenda moja kwa moja direct chuo kikuu"
My take:nadhani kale ka ugonjwa ka slip of tongue kamemtait jamaa....
 
Ni kweli kingereza ni taabu kwa mfano sisi tuliofundishwa na walimu wa upe hatukuambulia kitu kingereza tulikikuta sekondari hivyo ni lazima kitupe shida kukielezea na kukiandika.watu wengi ni wajanja wa kuongea na sio kukiandika wala kukisoma.Haiwezekani kuamasisha kiswahili ni lugha ya taifa wakati unahukumiwa kwa kingereza.
 
Kuna generation flani hapa Tanzania ambayo kingereza ni tatizo kubwa. Watu wengi walisoma shule za msingi za serikali(ukiacha Olimpio na Arusha School) kati ya miaka ya 80s hadi sasa hawana backgrond nzuri ya kingereza. Ndio maana utakuta watu wengi wenye umri kati ya around 50yrs kurudi chini hadi around 25yrs hawawezi kuandika/kuongea kingereza fasaha. Kwa bahati mbaya ndio hao watendaji na viongozi makazini serikalini na mashirika binafsi. Baada ya kugundua hilo tatizo wengi kama sio wote wenye uwezo wakawapeleka watoto wao shule za English medium ambazo zilianzishwa miaka ya 90 kama uyoga. Sasa hivi kuna vijana wako vyuoni wanaongea kingereza vizuri sababu wamesoma kwenye shule hizo za English medium. Tutegemee wafanyakazi wanaojua kingereza vizuri huko mbeleni wakishaingia hawa vijana kwenye soko la ajira. Hiyo ni analysis yangu ndogo tu

Tatizo la lugha litakuwa kubwa sana siku zijazo kama hatutaangalia namna nzuri ya kuifanya Lugha yetu ya taifa kuwa mhimili wa maendeleo katika nyanja zote.

Juzi initoka Kawe kuelekea mjini nilipanda daladala la Kawe-K/Koo, kwa bahati nzuri konda alikuwa hana roho mbaya kwani karibia nusu walikuwa wanafunzi! Tofauti hapa ilikuwa wale wanafuzi wa secondary inaelekea wanasoma shule zakata na wale wa primary (wengiwao walipandia Mikochen B na Kwa Warioba) wabasoma academies na saint schools. Wale wa primary walikuwa wanaongea kiingeleza kizuri mno (katika maongezi yao ya kishule) na watu wengi tulistaajabu na kuwasifia ila wale wa secondary hakuna hata mmoja aliyeweza hata kuunda sentensi moaj ya kiingeleza na waliposikia wadogo zao wanamwaga ngeli ya uhakika wakaanza kulaani shule walizopitia na walizopo kwa sasa na kuonyesha kukata tamaa kabisa.

sasa ukiangalia ya wanafunzi katika aina hii 2 ya shule utagundua tu kama hakutakuwa na commitment ya kueleta mageuzi katika lugha huko mbeleni itakuwa ni full vichekesho!
 
Naona Tundu Lisu aende mbali zaidi hadi kuna ma waziri hawajui kimombo, kama Issue ya waziri Mulugo, ni aibu kwa Taifa,
na Mpaka sasa hajaomba radhi

Ameshaomba radhi kwenye kipindi kimoja hivi cha radio!!
 
lisu kasema kweli mfano mzuri ni yule kilaza naibu waziri mzee wa 11961 badala ya 1961 yewiiiiiiiiiiiiii!??????
 
Salaam wanabodi

Mbunge wa Singida na mwanasiasa machachari Katika siasa za Tanzania ndugu Tundu Lissu ameendelea kuwasakama majaji wa Tanzania kwa kusema hawajui kiingereza.

Akichangia leo bungeni amesema ukisoma hukumu nyingi za majaji wa Tanzania utasikitika 'watu wanahukumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa kwa sababu majaji hawajui kiingereza ambayo ndiyo lugha inayotumiwa kwenye sheria za Tanzania,hivyo ameshauri sheria zote ziandikwe kiswahili.

Wakati umefika kujimuvuzisha kwenye kiswahili katika technical and skilled knowledge! kizungu hakifai kutumika
kila mahala!!
 
Naona Tundu Lisu aende mbali zaidi hadi kuna ma waziri hawajui kimombo, kama Issue ya waziri Mulugo, ni aibu kwa Taifa,
na Mpaka sasa hajaomba radhi

Amewaambia ukweli pale pale bungeni kwamba ndani ya hili Bunge tukufu kuna watu hawajui kiingereza na hawajakanusha wala kuomba muongozo,nimemsikiliza kwa makini sana, kweli Lissu ni mfano wa kuigwa kwa kusema ukweli bila kumung'unya maneno.
 
SASATELE, unayosema ni moja ya ukweli ambao hata mimi ninaukubali. Kuna wale waliofundishwa na waalimu wa miaka ya 70 wao wanaandika na kuongea kiingereza fasaha.
1. Kwa watanzania wengi walio UK, moja ya jambo linalowatofautisha na waafrica wengine ni Kiingereza. Hili halina ubishi (hata kama wataamua kubisha ukweli huu)wengi hawawezi kuandika wala kuongea hasa unapowalinganisha na waafrika wengine waliohamia UK.

2. Waafrica wengi Kiingereza ni lugha ya pili,tatu au nne (wanazo lugha zao za asili),lakini watanzania walio wengi tunakuwa hatujiwezi kabisa.
3.Kuna watu wengi wamekaa UK miaka zaidi ya 10,lakini hawawezi kuandika sentensi 5 zilizosimama kwa kiingereza.

4. Hata waliosoma hapa,baadhi yao (walio wengi) wanaongea na kuandika kiingereza cha kiwango cha mtoto wa miaka 7 - 12. Hii nina maana ya kuandika, kusoma na kuongea!

5. Tatizo ni mfumo wa maisha, kiwango cha uchumi lakini pia tamaduni zetu ambazo huwa: (a) ujeuri wa kijinga ambao umezaa uzembe - nikimaanisha tuna tabia ya kujiona tunaweza, lakini hatufanyi jitihada za makusudi na kutoa kipaumbele kwa mambo mengi tunayoweza ili kuweza kuufikia mwisho ule tunaoutaka. *Hata wanaosoma kiingereza hawafanyi maamuzi ya kutaka kujua kwa ufasaha hiyo lugha. Hapa utaona tatizo letu sio kiingereza tu - hata kiswahili. Tuna watu wanataka kuongea kiswahili kama wakenya/ wamerekani.Tunaishi kujua vitu nusunusu.

6.Kutokujua kiingereza kwa mtu anaeishi mazingira hayohayo kila siku - inaacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa maana ya kuwa kama miaka 10 hujaweza kumudu lugha,hayo mengine kama taaluma na ukuzaji wa vipaji utapata taabu (you will be challenged).

7.Kama wanaoishi ulaya wanataabika na lugha hivyo kulazimika kufanya kazi ambazo wasingezifanya kama wangekuwa na uwezo wa lugha, hili la majaji na wabunge ni moja ya kielelezo cha tatizo kubwa zaidi.

Hivyo basi,badala ya kuendeleza ujeuri na ubishi - kila mtu ajikwamue kivyake kwa kujenga uwezo wa yale tunayoyafanya ikiwemo lugha ya kiingereza. hii inahitaji kubadili attitudes zetu towards our inferiority and confidently overcoming any challenge we have in life including knowledge in English. Kama nilivyosema kabla juu ya waziri mulugo - tatizo halikuwa kiingereza,tatizo lilikuwa ni capacity and his competence. And this is our problem!
 
wewe una umri gani?mimi ninajua kiingereza,lakini siko fluent simply because sikitumii kiingereza kwenye activities zangu za kilia siku..............nadhani wewe hauzungumzii kujua kiingereza,unazungumzia kuwa fluent.ili mtu aweze kuwa fluent anatakiwa awe na zile core pillars of language;speaking,listening,writing and reading...............huwezi kuniambia mtu mwenye degree hajui kiingereza,labda awe amenunua cheti.................hao watoto unaosema wamesoma english medium walete ushwahilini kwetu halafu uwacheki tena baada ya miaka miwili kama bado wataendelea kuwa fluent.lugha kama vitu vingine inahitaji practices for practice make perfect.............

Mkuu, mimi nadhani huyu bwana aliyefanya utafiti mdogo kuhusu umri wa wa-TZ wanaoongea au kujua kiingereza kwamba ni wale wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na chini ya miaka 25 yuko right.

Pamoja na kwamba umempinga ebu angalia wewe mwenyewe ulivyoandika hapo nilipopatilia wekundu. Hiyo kwa wenyewe wanaokijua kiingereza ilitakiwa isomeke practice makes prefect.....
 
Back
Top Bottom