Maisha ya Mtumishi wa Serikali ni Magumu mno. Mungu aingilie kati

Huku kwenye kujiajiri na biashara ndio usiseme, kwa siku unaweza unauza cement mifuko 3. Halafu faida ya mfuko mmoja ni 500, mabati hayatoki nondo hazitoki yaani watu hawajengi sijui wenzangu wa hardware biashara mnaionaje..


Sent using Jamii Forums mobile app

watu hawawezi kujenga kama hawa hela, kikubwa ni mzunguko wa hela kwa wananchi umekuwa mdogo sababu nayoiona mimi ni ujenzi wa hii miradi mikubwa ambayo yote macontractor wake ni wageni, mimi ningeishauri serikali kwenye hii miradi ingehakikisha marighafi zote zinatoka ndani lakini pia hizi kampuni zingekuwa na joint venture na kampuni za ndani hela nyingi zingebaki kwenye mzunguko hapa nchini. kingine kumfanyisha mtu kazi miaka 6 bila kumpandisha daraja ni uonevu na kuumiza uchumi. majukumu mtu aliyonayo mwaka wa kwanza wa ajira siyo hayo aliyonayo baada ya miaka 6, familia inaongezeka pamoja na mahitaji yake pia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dooh!

Game taiti kweli...!
Haya makato ni balaaa! Yaani ukiangalia kule juu na kinachobaki huku chini ni vitu viwili tofauti...

Yaa kodi makato ni almost 50%. ..

Hope serikali itaangalia hili.
 
Dada unapiga kelele unapeleka nyumbani 400,000/= kwanza nakupa Hongera sana, ukiona za wenzio itashukuru Mungu
 
on serious note,mkuu aliangalie swala hili la nyongeza ya mishahara kwa watumishi watu wana hali mbaya wamechoka mimi ninapofanyia kazi ni shirika la umma kuna mishahara ya aina tatu kuna watu wanapata mpaka milioni 5 na mwingine anapata laki tatu na nusu hao wenyewe kuanzia milioni tatu hizo wanawachukulia poa balaa hawa wadogo wapunguze kodi ya payee kwanza na waongeza salary
 
Mtu umesomeshwa kwa tabu na gharama, umepata ajira. Ila ndio hivo tena ajira yenyew haina raise,haina posho, haina maruprupu na unabid uutegemee mshahara kwa kila kitu(usafir,chakula malazi,kusomesha,ndugu,kujenga,magonjwa n.k).

Sema kuna watu wanakera sana. Unakuta eti unamfananisha mtoa mada na watu waliokosa ajira au na watu wanao okota makopo barabarani. Sio sawa hata kidogo.
Aliyekosa ajira halingani na huyu mdau aliyetumikia miaka 13 kazini.
Anaye okota makopo naye ndio ajira yake maana hakusoma.
Ila kama mtumishi lazima ujitafutie shughuli zingine za kukuingizia kipato mbali na mshahara. Pole mdau.
 
Kweli kabisa watumishe wanasema hali ni mbaya

Hili nililishuhudia mwaka 2017 nilipo maliza masomo nilienda kijijini kwetu kupumzika, hivyo shule ya sekondari jirani na kijijini kwetu nikawa nafundisha
Huku walimu wamekata tamaa hasa walimu wa kike wa shule za msingi

Ufanisi wa kazi unapungua... Inasikitisha Sana.
 
mkuuu mshahara unaokula uncle wangu yupo daraja D Anakula nusu yake ana hali.ngumu sana
 
Back
Top Bottom