Maisha ni Safari!

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,822
3,651
Safari yangu ya kujitafuta na hatimaye kujitegemea imekuwa tofauti kidogo!

Maisha ya ghetto nilianzia chuo! Wakati huo ilikuwa rahisi sana, pesa ilikuwepo na fursa zilikuwa nyingi. Sikuona ukali wa maisha.

Wakati namaliza kidato Cha sita familia yetu iliingia kwenye migogoro kidogo. Bi mkubwa na mshua walizinguana na ghafla mshua akavuta jiko jingine ikawa noma sana hofu na mashaka tele kuhusu mustakabali wetu!

Ikawa inapita hata miezi mitano bila mshua kurudi home bahati nzuri bi mkubwa alikuwa anafanya biashara so pesa ya kubadilishia mboga ilikuwepo. Home hakukuwa na utofauti wowote pia mshua alijitahidi Sana kunicheki kwenye simu na kunitumia pesa Kila nikihitaji, maisha yalikuwa fresh japo bi mkubwa alikuwa na huzuni!

Nikaenda chuo. Hapo mshua hali yake ya kifedha kidogo ilikuwa imetetereka mambo yake ofisini yalikuwa hayajatulia na hakutaka nijione mnyonge, akauza gari Ili niende chuo! Nikaenda chuo na hela ndefu Sana! Kufika chuo nikakuta hostel za chuo zimejaa ikabidi nikapange!

Bahati nzuri Kuna nesi alikuwa anahama mji so anauza Kila kitu nikakutana nae nikanunua vitu vyake na chumba nikalipia pango nikahamia! Chumba kina Kila kitu! Nikajikuta ghafla tu nipo ghetto halafu ghetto la kishua hatari!

Nipo mwaka wa tatu mdogo wangu na yeye akapata chuo kwenye mji huo huo ila tofauti na chuo ninachosoma Mimi! Akaja kuona ghetto langu akalikubali Sana na yeye akapambana akapata ghetto lake fresh!

Nilipomaliza chuo sikutaka kuuza vitu vyangu. Bahati nzuri kwenye nyumba aliyokuwa anaishi dogo kulikuwa Kuna chumba hakitumiki nikaongea na mwenye nyumba akaniruhusu nihifadhi vitu vyangu kwenye chumba hicho kwa malipo kidogo tu! Mimi nikarudi nyumbani kujipanga!

Kufika home bi mkubwa ananiambia mshua kastaafu so nisicheze mbali soon anapokea pensheni! Bahati nzuri na mshua pia akaniita akasema nisiondoke Hadi apokee Hela zake! Miezi miwili mbele akapokea pensheni yake, pesa fulani imetakata Sana!

Akanitia hela ndefu mno, ndefu Sana! Akaniambia nimjengee bi mkubwa nyumba maana yeye yupo kule kwa bi mdogo so atashindwa kufanya kote! Mzee nikatafuta fundi tukapanga bajeti nyumba ya milioni 50! Kazi ikaanza!

Nipo na fundi kuanzia kuchimba msingi na Mimi nashika sururu, saidia fundi! Fundi alikuwa muwazi Sana! Hakuna janja janja! Kwani tulifika mbali? Pesa iliisha! Kiukweli nilijengea sifa! Haikuwa nyumba Bali jumba tofauti na maelekezo ya mshua ila alinielewa! Na yeye akaja kuhakikisha project inaisha!

Hadi nyumba inakamilika tushatumia zaidi ya milioni 100! Hizo ni zile hesabu ambazo tulizirekodi mfano cement, nondo, tofari, madirisha, rangi, tiles, gharama za ufundi n.k! Mshua akawa proud Sana na Mimi! Kiukweli nyumba ilikuwa ya kidon yaani hata ukiibwaga pale Masaki huchafui mazingira!

Mshua safari za kuja home zikawa haziishi anakuja na marafiki zake na lazima anipe credits engineer!! Kule mji ambao dogo alikuwa anasoma na ananitunzia vitu vyangu kumbe ameviuza bila Mimi kujua! Alinitumia laki Moja kama kifuta jasho nikasema Alhamdullilah! Maana angeweza kunizima mazima! Ila ninachojua vitu vyote bei ya hasara Sana basi alipiga kama milioni hivi! Alhamdullilah!!

Kuna nyumba mshua alikuwa anajenga kimya kimya ukiondoa nyumba ambayo alimjengea bi mdogo! Sasa alipoona Mimi nimevurunda bajeti zangu ilibidi Ile nyumba isimame Ili aje anipe sapoti Mimi! Kwahiyo bajeti ya hiyo nyumba ikawa imehamishiwa huku kwangu!

Bahati nzuri ilikuwa imeezekwa, ilipigwa lipu nje na ndani, sakafu ilikuwa tayari, frame za madirishani zilikuwa zimewekwa (hakutaka kuweka almunium), milango ilikuwa tayari! So baada ya nyumba ya bi mkubwa kuisha mshua akanionyesha hii nyumba nyingine! Na kwamba nihakikishe napambana niimalizie maana yeye hawezi sababu bajeti yake ilihamishiwa kwa bi mkubwa!

Muda wote huo serikali imetangaza ajira awamu tatu na zote nimekosa! Sasa nyumba nitaimaliziaje! Ndio akili inakuja Sasa kwamba hivi kwanini nisingejenga tu nyumba ya kawaida halafu nikachota hata milioni Kumi nifanye biashara? Maana niliachiwa Kila kitu! Why? Why? Why?

Sema mshua masta akaingia Tena mchezoni! Akanipa mtaji niingie shambani nifanye kilimo! Na akanikutanisha na washkaji zake ambao wapo kwenye kilimo muda mrefu wanipige msasa kabla sijaenda kuzika mtaji wangu! Nikapigwa msasa na kuelezwa changamoto za kilimo! Nikaingia shambani!

Huu mwaka wa tatu, sio haba! Nimeweka madirisha Ile nyumba niliyoachiwa niimalizie! Nimeweka umeme na maji na nimehamia! Bado Haina Dari Wala rangi! Napambana nimfanye mshua awe proud zaidi! Na Sasa hivi amekuwa mshkaji wangu kinoma Kila siku lazima tuonane! Akipata michongo hanisahau!

Dogo alimaliza chuo akapata ajira chap kwa haraka maana mwenzangu alisomea udaktari saa hizi yupo mpakani huko anajipambania!

Ila nilichojifunza ni kwamba hakuna kitu kigumu kama kutafuta hela! Kutafuta hela ni shughuli nzito hasa kwa tuliojiajiri! Sometimes vitu vinagoma kabisa ila hakuna jinsi lazima maisha yaende!

Now mshua na bi mkubwa wapo vizuri wana enjoy maisha kwenye nyumba yao (kazi ya mikono yangu japo Hela alitoa mshua).. pia mshua namkubali Sana maana kipindi Cha migogoro japo alivuta jiko ila hakupoteza focus la sivyo mtafutano WA saa hizi ungekuwa balaa!

Leo nimetafakari tu njia nilizopita, sio njia ngumu kiukweli ila zimenipa funzo kubwa!
 
Hongera sana.
Nashukuru kupata support kutoka kwa wazazi.

Same to me.
 
Hongera sana.
Nashukuru kupata support kutoka kwa wazazi.

Same to me.
Asante sana mkuu.... Kiukweli mzazi hatakiwi kumuacha mtoto! Hata kumpa moyo tu na miongozo maisha ni magumu kwa sisi tunayoyaanza!
 
Write your reply...Mkuu wewe Ni mmoja wa wale watoto waliojaliwa baba wanaojielewa,Baba yako Ni jembe sana muombe Mungu aendelee kumbariki na kumpa maisha marefu yenye amani na furaha hapa Duniani.
Namshukuru Mungu kwa hilo! Mshua alisimama Sana migogoro yake na bi mkubwa haikumfanya atutelekeze sisi watoto! Japo hakuwa anafika nyumbani ila simu zake ziliita Sana! Sometimes alikuwa akisafiri kwenda mikoa mingine kikazi ananitumia nauli na Mimi niende... Ananiambia chanzo Cha migogoro kiukweli ilikuwa changamoto sijui nisimame upande gani ila mshua hakuwahi kunilazimisha niwe upande wake yeye alitaka tu niujue ukweli nisimchukie!
 
Hongera sana..
Mimi hapo kwenye milioni 100 ukashindwa kuchomoa 10M ukizingatia hauna ajira na huo sio wizi unaamisha baadae ungemwambua mzee angeelewa tu.
 
Back
Top Bottom