Maisha mapya baada ya kuvunjika kwa mahusiano

Strictly Syrup

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,219
1,793
Maisha baada ya kuachana yanategemeana na mtazamo wako wewe. Kama ukiutumia muda huo kujijenga kama kujifunza lugha mpya, kwenda kutalii (kama una akiba) kuanzisha ratiba ya mazoezi, kujiendeleza kielimu na vingine vingi kama kuongeza bidii kwenye utafutaji wa pesa, utayafurahia sana maisha yako mapya.

Lakini ukikaa ndani kumfikiria X wako muda wote, kujuta, kuhuzunika, kuwa na sonona ni kujitafutia msongo wa mawazo na kuharibu afya yako. Kitu kizuri ni kukubaliana na kila hali ya maisha unayopitia hata ikikuumiza vipi lakini inakuweka huru, hiyo ndiyo moja ya kazi ya ukweli. Endelea kuboresha maisha yako, penda wachache ulionao kama familia, watoto, marafiki na watu wengine unaokutana nao katika harakati za kila siku.

Kumbuka ukiendelea kuwa na mawazo ya mtu ambaye hayupo kwenye maisha yako, utakuwa mtu mwenye huzuni na utashindwa kufungamana na ukweli.

Haishauriwi kuanzisha mahusiano mapya kama kigezo cha kumsahau mtu aliyepita, jipe muda wa kujipanga upya, kuruhusu maumivu yapite. Muda huo ni mzuri hata kuanzisha hobby mpya kama kutengeneza muziki, kusikiliza muziki, kubadili mtindo wa kimavazi, kubadili maeneo ya kufurahia maisha kama kwenda beach, kutalii, kwenda kunywa kahawa, kuzungumza na watu wazima pia kutakujenga zaidi na mengine mengi. Maisha ni mazuri sana ukiyaishi kwa moyo mkunjufu bila kuwa na king'ang'anizi kwa watu au vitu.

Na kumbuka, ukimpenda mtu hata kama asipokuwa na wewe utaendelea kumpenda kikubwa unajua ana furaha. Kumpenda mtu si lazima awe wako, na hata kama ulifanya mema usijilaumu wala kujuta kwani upendo wa kweli ni kutoa na siyo kutegemea malipo ya fadhila.

1626673689780.png

 
Hivi kabisa kuna watu wakiachana, wanawaza weee, mpaka wanakonda???
Kama haukuwahi kuwa na moyo wa upendo maishani mwako ntakubalinaa na hoja yako. Lakini kama ulishawahi kupenda lazima kuna hali kama hii utaipitia, na ubaya watu wengi hupenda wakiwa bado hawana hekima juu ya mapenzi. Watu wengi hupenda kwa dhati bila kujua wanatakiwa wawe selfless ili mtu akiamua kuondoka wanakuwa huru kuwa fungulia mlango. Kwa hiyo watu wengi hujifunza the hard way kwenye suala la mahusiano na hakuna ambaye hajawahi kupenda kweli na akaumizwa.
 
Sasa si Bora huumie kwa wakati mmoja. kuliko kuendelea kuumia kila siku kwenye mahusiano yasiyo na furaha tena
Thats the point, kuna watu wanapitia mengi mpaka wanafikia kufanya maamuzi ya ajabu sana kwa sababu ya kulazimisha upendo. Kizuri ni kujifunza ni wakati gani sahihibwa kubadili maisha yako.
 
Ndomaana nasema ata huyu Nema aliemchoma mwenzie sie yeye. Ukute aliwekeza kwa mwenzie kumbe mwenzie hampendi.
Thats the point, kuna watu wanapitia mengi mpaka wanafikia kufanya maamuzi ya ajabu sana kwa sababu ya kulazimisha upendo. Kizuri ni kujifunza ni wakati gani sahihibwa kubadili maisha yako.
 
Back
Top Bottom