Mahusiano yanataka kuniumiza akili

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Habari humu ndani?

Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha JF

Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya wengine tutoe yanayotuumiza mioyoni mwetu.

Ipo hivi, nimekua kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 9 na huyu mwenzangu. Tulianza mahusiano tukiwa chuo kikuu. By the time tumeanza mahusiano, sikuwahi kufikiria ndoa. Ingawa mwenzangu alinitamkia mara kadhaa ingawa sina hakika kama ni hali ya utani ama la.

Sasa tumekua watu wazima 30+. Kila mtu ana kazi yake, mi mdada nimepanga kwangu na mwenzangu anaishi kwao bado. Kiukweli maisha ambayo tulikua tunayaishi sikuyapenda. Kila mara mwenzangu anatoka kwao kuja kwangu. Ingawa mimi nina kipato kikubwa sana zaidi ya mwenzangu, lakini bado mimi ni mwanamke ninayehitaji mapenzi ya mwanaume. Lakini mwenzangu amekua kama mtoto kwangu. Anakuja nyumbani kwangu, kila kitu nafanya mimi. Na bado kuna muda ananiomba nimnunulie zawadi.

Kiukweli nilikaa naye chini nikamueleza. Binafsi kupata pesa nyingi zaidi yake sikuona kama ni kikwazo. Nilichohitaji ni kufanya vitu vya kimaendeleo zaidi kuliko starehe. Ila mwenzangu utasikia "Naenda kwenye mpira sasa utanitumia nipate japo mbili tatu?" Kiukweli hali hii ilinifanya nipunguze sana mapenzi kwake. Mwenzangu akaanza wivu labda nina mtu.

Kiukweli, nimejaribu kuongea naye mara kadhaa. Mwenzangu hata mpango wa kujiinua yeye kama yeye hataki. Na sasa nimegundua kwamba wamerudiana na ex wake. Nilichokifanya sikumwambia lakini nilimuomba same day same time, kila mtu afanye maisha yake. Amejaribu kunibembeleza lakini sioni cha maana anachokiongea.

Kuna baadhi ya mali zake ambazo zipo kwangu, nimeshamuomba mara kadhaa azichukue na hataki. Nikimwambia kuwa nazigawa anasema atatuma mtu azifate. Ikifika siku ya kuzifata hata nimwambie mtu anamletea, hajibu chochote.

Nimeamua kuondoka kwenye maisha yake. Sioni future wala sioni akibadilika. Ila l feel bad. Though najua kuèndelea kumganda mtu wa namna hii, itanifanya mimi nisipige hatua ya maisha.

This is what l wanted to share with you JF family.
 
Anyway, binafsi sioni kama kuna jambo linalo kutesa zaidi nafikiri kwasasa wewe umemuona huyo mpenzi wako hakufai kwasababu hafanani tena na wewe.

Maana kama ni tabia ungeweza kuzigundua mapema tangu mkingali chuoni, na ninadhani amerudiana na Ex wake kwasababu anaona hapati mapenzi tena kwako kama zamani.

Kurudi kwake kwa Ex maana yake Ex anakitu cha ziada kinacho mpa furaha kuliko wewe.

Ebu achana na mapenzi mkuu, fanya mambo mengine.
 
Umekimbia mwanaume ambaye Hana akili ya maisha lakini ana mapenzi, unakutana na mwanume mwenye akili ya maisha lakini ni hit and run, Hana muda na wanawake Wala mapenzi ......

Huwezi pata mwanaume mkamilifu hii dunia ...

Unachofanya unakimbia tatizo tu ,
 
Habari humu ndani?
Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha jf. Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya wengine tutoe yanayotuumiza mioyoni mwetu.

Nadhani umefanya maamuzi sahihi. 30+ ni umri wa mtu kujielewa na kujiwekea dira thabiti ya maisha.

Kwa tabia ulizotaja hapo, sidhani kama huyo mwanaume anastahili kuwa mume. Wengine wanabahati kuwapata wanawake wachakarikaji na wanyenyekevu ila bado hawaoni umuhimu wa kujenga ushirikiano wa kuwakwamua kwenye umasikini.

Kwako mimi sioni kama unateseka, naona unajitambua na kikubwa umeshajua tabia ya M wenzako mapema. Ni suala la kusimama na maamuzi yako tu.
 
Sasa tumekua watu wazima 30+. Kila mtu ana kazi yake, mi mdada nimepanga kwangu na mwenzangu anaishi kwao bado.
Kiukweli maisha ambayo tulikua tunayaishi sikuyapenda. Kila mara mwenzangu anatoka kwao kuja kwangu. Ingawa mimi nina kipato kikubwa sana zaidi ya mwenzangu, lakini bado mimi ni mwanamke ninayehitaji mapenzi ya mwanaume. Lakini mwenzangu amekua kama mtoto kwangu. Anakuja nyumbani kwangu, kila kitu nafanya mimi. Na bado kuna muda ananiomba nimnunulie zawadi.
Mimi sipendi unafiki... SIKUHURUMII, narudia... SIKUHURUMII...

You're 30+ halafu bado unaleta mapenzi ya Form II?! Look at you... unaweza kukuta "boy" wako keshagonga 35 halafu bado LINAKAA kwao! Ina maana hadi upelekwe kwa psychologist ndipo uambie na miaka 30+ yako una-date kivulana kilicho in his early 20's?

Being 30, 35, 45, is just a number... umri halisi wa mtu upo kwenye mind yake na utaonekana kwa yale anayofanya na kuyasema hadharani na sio kwa miaka aliyoishi duniani!!

Utalea watoto wenye umri mkubwa hadi lini dadangu? Umri ndo huo unaenda, and it's matter of time kabla watu wa size yako kuwa akina chige tulio in our 40's, na bado tutakuona kizee!

REMEMBER... I may be 10+ years older than you, lakini ni wewe ndie utakuwa unakimbilia kwenye expiration date badala ya mimi!! Tumia akili kuchagua mtu sahihi kwako badala ya kutumia moyo or emotion!

Moyo always mislead and make people behave and look stupid!

Eti rafiki yangu Prishaz, unaonaje nikijiweka hapa?! Manake kwa staili za u-snitch wa mtaa, huwa tunaanza kusaga sumu kwanza :D!
 
Habari humu ndani?
Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha jf. Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya wengine tutoe yanayotuumiza mioyoni mwetu.
Miaka 9 ni muda mrefu sana na sio rahisi kumwondoa mtu akilini haraka haraka. Umefanya jambo sahihi.. japo Umechelewa Sana. Sasa Utulie na Utapata mtu unayestahili. Aliyemzidi huyo jamaa kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na kujali, na pia kiwa responsible. Mambo mazuri hayataki haraka. Usimuonee huruma sababu yeye HAKUONEI HURUMA. Ni mbinafsi sana. Be strong. Ila usiwe na pupa sasa. Tulia na utapata mti sahihi.
 
Habari humu ndani?
Kwa kweli ashukuriwe sana alieanzisha jf. Maana kuna muda unatamani kuongea you dont know mtu wa kukusikiliza. Ila JF inasaidia sana kufanya
Aiseee haya mapenzi mimi mbona sina? Yaani amekugeuza chuma ulete wewe ndo mtoa pesa? Uko nae miaka 9? Wewe umerogwa sio bure, mpuuzi anaishi kwao miaka hiyo yote?

Kweli kuna wanawake mnapenda kiboya sana.mimi mwanaume ambae hatowi chochote kwangu siwezi mvumilia zaidi ya miezi 3.

Amka usingizini, huyo fala anakuona wewe ndo una shida sana wewe ndo unamuhitaji kuliko yeye snavyokuhitaji.

Manina zake nyau huyo.mpigie simu mwambie aje muongee, akifika uwe umeshaandaa nguo zake mkabidhi funga mlango.

Au muulize alipo akisema yupo nyumbani mwambie unakuja kumuona, nenda na mizigo yake yote.
Ikiwezekana hama huo mtaa, mwambie vitu vyake umeviacha ndani akavifate, kha yaani nimesikia hasira sana huu upuuzi siwezi ufanya.

Mpuuzi huyo ana nini cha maana kinachokufanya uendelee kuwa mtumishi wake?

Mwanaume wa hivyo awe wa mwisho kwako, umepoteza muda mwingi sana.sasa amka usingizini.

Ukipata mwingine, hakikisha usimfiche ualisia wako muoneshe mwanzoni kuwa anatakiwa kuwajibika kwako kama mwanaume.lazima atowe pesa kwa ajili yako.

Tangu niwajuwe wanaume walivyo wapuuzi siteswi na mapenzi, zamani nilikuwa nawaza atanionaje nikimwambia mambo ya pesa?niliteseka sana

Nikawaza hawa ni wa kuwambia indirectly.

Kuna mmoja huyoanataka kunipandisha nyeunge niende kwake ahaaaaa nimenyoosha maelezo, nikamwambia mimi sipandi basi masaa 13 nimekalisha tako kwenye basi kukufata, nikamwambia nasubiri tiketi ya ndege asipotuma kwangu nakula nakusaza. Na ataituma asipotuma sina cha kupoteza kwake.

Inabidi nimzoeshe hivyo asije niona mimi ni wa kusafiri na nyeunge kha. Mtu uwezo anao afu nijitese? Nyooolooo zake😂

Dada leo hii hakikisha huyo tegemezi anaondoka kwako mwambie umepata mwanaume mwingine. Ishiiiiiy
 
Miaka 9 ni muda mrefu sana na sio rahisi kumwondoa mtu akilini haraka haraka. Umefanya jambo sahihi.. japo Umechelewa Sana. Sasa Utulie na Utapata mtu unayestahili. Aliyemzidi huyo jamaa kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na kujali, na pia kiwa responsible. Mambo mazuri hayataki haraka. Usimuonee huruma sababu yeye HAKUONEI HURUMA. Ni mbinafsi sana. Be strong. Ila usiwe na pupa sasa. Tulia na utapata mti sahihi.
Good umechangia vizuri fala yule analelewa miaja 9? Mimi hayo mapenzi sina. Huyo mchunaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom