Mahusiano ya mume wangu na mimi ni kama baba na mtoto wake

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Tumsaidieni dada huyu wanaJF na tutajifunza mengi kwa hiki kisa chake.

Mimi nimeolewa miaka 2 iliyopita tunaishi vizuri na mume wangu japo mi sina raha na hivi ninavyoandika hii msg nimenuna toka jana. Tatizo langu ni huyu mume ananijali ananitimizia ila uhusiano wetu ni kama baba na mtoto kasoro ni kwamba tunakula chakula cha ndoa. Yaani heshima nayoitaka mi nimechoka jamani. ndoa haina utani, hakuna kucheza, yaani ni mama mama mama basi. hicho chakula cha ndoa ni lazima kitandani na style ni ile ile kila siku. nimejaribu kumueleza ananimbia mimi ni mkewe sio mwanamke wa mtaani so lazima aniheshimu. nimejaribu kumuwekea movies za kumchangamsha anajidai kama haelewi. kuna siku nikamfuma yuko na rafiki zake stories alizokuwa anapiga huwezi amini nipotokea alibadilika ghafla. jana nikatumia msg ya kichekesho chenye matusi kidogo tu nikamforwadia nae acheke jamani hakujibu jioni amenisema kuwa natarajia nini kutuma msg kama ile lazima nijiheshimu nk nk hadi nimenuna. naombeni msaada nimfanyaje maana nishaanza kuboreka. sikumjua wakati wa uchumba maana uchumba wetu ulikuwa wa mbali. yaaani natamani nipige kelele
 
1.Mshukuru Mungu kwa vile una mme ANAKUJALI na ANAKUTIMIZIA na mechi unapata kila siku.Ila sijui kama magoli anafunga au mikwaju yote UNADAKA.
2.Wanawake wengi wa Dar wanatafuta mme atakaewatimizia hiyo ni firstpriority na hawawapati.
3.Wewe unae unalalamika oooh hatutaniani,hatuchezi?........hayo hataki anadhani utamdharau.
4.Kubali matokeo,hilo ni tatizo dogo sana kwenye ndoa,auuuu,eeeeh au umepata KADUMU?/HAWARA anaekuchekeshachekesha nakukutekenya tekenya sasa una mwona mwenzio ni TATIZO?.Mvumilie.
5.Taratibu sana anza kuingiza vijiutani kwa umakini na kwa uangalifu mkubwa,.......itachukua muda atakuzoea ataanzakufanya unavyotaka wewe.
6.Zidisha mapenzi mama,ukimpenda sana sana,akaingia LAINI,atafanya chochote unachotaka,
7.Hata hivyo binadamu huoa/huolewa na binadamu wenzao,hawaoi/kuolewa na MALAIKA hivyo kuna kasoro,mapungufu kibao VUMILIA
8.Wewe nawe una kasoro zako nyingi tu.......au unasemaje HUNA?
9.Usiige wanandoa wengine wanaishije UTAPOTEA, eti sijui kutwa nzima wenzenu wanataniana,wanacheka wanateknyana....weeeee?WAONGO hao hiyo ni danganya toto kukuzuga wewe wakirudi home ngumi mtindo mmoja,matusi kibao utasikia ''paka wee'',wakilala ni mzungu wa nne huyu kageuka huku yule kule.
10.Pia mmeo huenda anawaza kuwa mkitaniana na kucheza,utamzoea halafu mambo yatakuwa hayaendi?akirudi nyumbani anaomba chakula njaa inauma unamjibu kwa utani ''kale kwa hawara yako aliekuchelewesha hadi saa hii''
HATA HIVYO NAWASHAURINI WANAUME WENZANGU,MPE MKEO ILE KITU ROHO yake INAPENDA,kutaniana nae,kucheza nae kunafanya Nyumba iwe ya furaha na AMANI masaa yote. MTU Unaingia ndani kwako kama kituo cha polisi,au maktaba,ooooh NO.hAYO SI MAISHA na naona hayana raha yoyote........na ole wako siku shemeji akikutana na wajanja huko nje!!!!!!!!!!!!!!weee utalia.
 
Huyo ameamua kuweka distance na wewe. Hicho anachokifanya ni mtindo wa kizamani wa mababu zetu: walifundishwa kutokuzoeana na mke. Kuweka umbali na kujenga "heshima" naye. Huenda amelelewa kihivyo na wazee wake/mababu (kama kakulia huko). Anaona mkizoeana sana pengine heshima inaweza kupungua. Hiyo ni aina ya upendo tu. Usijali sana, nenda naye hivo hivo, pengine taratibu atabadilika. usikate tamaa wala usidhani hakupendi. La! Hivyo ndivyo alivyofundishwa na wakongwe (mababu) jinsi ya kumpenda na kumheshimu mke ili naye akuheshimu.
 
umakini ni muhimu katika hili. hopely unamjua vyema mumeo japo si sana. mvumilivu hula mbivu na vumilia na mpeleke taratibu mwisho utafika. nahisi kuiga ndiko kunakufanya uishi bila raha.
 
Ni jambo gumu kuishi na mtu wa namna hiyo ukiamua ni kesho tu atabadilika. Ukitumia nguvu sana utamkosa ila ukitumia utundu mliofundishwa kwenye unyago utawini.
 
1
HATA HIVYO NAWASHAURINI WANAUME WENZANGU,MPE MKEO ILE KITU ROHO yake INAPENDA,kutaniana nae,kucheza nae kunafanya Nyumba iwe ya furaha na AMANI masaa yote. MTU Unaingia ndani kwako kama kituo cha polisi,au maktaba,ooooh NO.hAYO SI MAISHA na naona hayana raha yoyote........na ole wako siku shemeji akikutana na wajanja huko nje!!!!!!!!!!!!!!weee utalia.

nashukuru kwamba angalau katika para ya mwisho umejikosoa kwa yale uliyoeleza hapo juu! maisha ya ndoa yana mambo mengi sana, kula kunywa, kufanya ngono ni sehemu tu ya maisha ya wanandoa, kuna mengi zaidi ikiwemo hayo anayolalamikia huyo dada, mie najua kile kitu ambacho anakizungumza. mimi nimeolewa karibu miaka 20 iliyopita, mume wangu ni kaka, ni baba, ni rafiki yangu mkubwa, ni mume n.k. n.k. kunawakati tunakaa kama mtu na kaka tunapeana ushauri, au kama baba wa watoto na hata kwangu pia, kuna wakati tunaishi kama wapenzi tuliokutana jana, mara kama marafiki wapenzi kwa kupiga story kucheka, kutaniana n.k. na wakati mwingine tunakua kama mke na mume. na haitupunguzii haeshima wala kuleta dharau. mie nimpe pole dada huyo na kumtaka aendelee kumbadilisha mumewe taratibu atabadilika tu, cha msingi ni kuwa na mawasiliano ya kutosha ndani ya nyumba.
 
Mie sina la kuongezea... Mengi yamesemwa na Muhanga pamoja na Tall...
Nimefurahishwa sana na ushauri wao...
 
Huyo mwanaume ni mnafiki tu. Kama ulimfuma akipiga stori za kipuzi kisha akauchuna basi ana mambo yake. Aidha umvumilie au na wewe utafute faraja kwingine maana inaonyesha unapenda kinky sex. Kitu kingine ni kuwa akikuangalia anashindwa kuamua kwani labda inaonyesha umekaa kitawa zaidi (sister). Hayo yapo ila ukimchunguza utaona kuwa mambo hayo ya mautundu kuna wanawake wanayafaidi toka kwake kwani akiwatazama anaona wamekaa mkao wa kimahaba na kiuchokozi zaidi. Kazi kwako
 
Huyo mwanaume ni mnafiki tu. Kama ulimfuma akipiga stori za kipuzi kisha akauchuna basi ana mambo yake. Aidha umvumilie au na wewe utafute faraja kwingine maana inaonyesha unapenda kinky sex. Kitu kingine ni kuwa akikuangalia anashindwa kuamua kwani labda inaonyesha umekaa kitawa zaidi (sister). Hayo yapo ila ukimchunguza utaona kuwa mambo hayo ya mautundu kuna wanawake wanayafaidi toka kwake kwani akiwatazama anaona wamekaa mkao wa kimahaba na kiuchokozi zaidi. Kazi kwako

Duu!
 
Alitakiwa ambane the same day alipomfuma akipiga story! Alikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa hayuko fair huyo mumewe! Unajua kina baba tukibanwa kwenye kona unakubali yaishe!:target:
 
Hivi kuna mkate mgumu mbele ya chai kweli?

Mleta Uzi tungependa kupata mrejesho tafadhali....
 
Back
Top Bottom