Mahusiano na mume wa mtu ni shughuli pevu

nakubaliana na wewe to some extend,ila akiendewa kwa kalmanzila kama ilivyo hali ya sasa,mbona nyumba ndogo itafaidi na nyumba kubwa watateseka
 
Kuna wanaume wengine walivyo na kero na maudhi ya moyoni ni bora hata ungekuwa nyumba ndogo yake ukamuona kwa masaa machache akarudi na gubu lake kwa mkewe...! Waiiiii...!!!
 
Unavyomchimba unataka akitoka hapa atumiwe msg "nimeona ujumbe wako mjanja wewe ila Mungu atanilipia " hahahahhaha mana watu wanavyojua kumsakizia Mungu hataree

Hahahaaa😂😂😂😂😂😂 Umejua kunichekesha!
 
Haaa anasemaje sasa mwenye mume jamani... ila umekua honest


Hahahaaa naona kishachoka, siku hizi anafanya yake tu. Mwanzo alinichokoza sana sema mi ndo muda wa kujibu jibu mtu huwa sina nina kiburi na kisirani cha asili.
Siku hizi kamrudia Mungu, kuna kipindi aliomba aongezewe dola Elfu tatu ili aende Nigeria kwa TB Joshua.
#maombioyeeeeeeeeee
 
Umeona ee, maana tunayaona huku mtaani

Ujue kuna kitu sijakielewa hapa, na ninadhani na nyinyi wanawake hamkielewi! Kukaa na mumeo kwenye nyumba nzuri na watoto hapo hapo wakati akitaka kutuliza moyo, mtu wa kucheka naye, mtu wa kumpa furaha si wewe mke wake ni mchepuko ina maana gani? Mchepuko hasikudanganye mtu, ata kama nimeupangia nyumba vichani but mi mwenyewe napata raha huko si mbaya!
Mnasema eti anautumia mchepuko, si kweli! Kama mchepuko unaupenda, unaupenda kuliko hata mke wa nyumbani! Then nikwambie kitu, kama umeolewa utaniambia, ata kwenye swala la mapenzi mchepuko unafaidi kuliko mke wa nyumban! Utajitupa kwenye romance, kunyonya hapa na pale, lakini ukirud nyumbani unatimiza wajibu, round moja inatosha!

Sasa unapoudumiwa si kwamba wewe ni bora kuliko mchepuko ila jamaa anawaudumia wanawe, so nawe unaponea hapo hapo! Kwa hiyo unakuwa kama house girl na estate manager, si mpenzi, mtu wa kwanza kufikiriwa akiwa na amu ya mapenzi! We michepuko unaijua au unaisikia? Inategemea na mchepuko lakini, lakini kuna mingine safi sana na haiendekezi kuongwa, ukiwa nacho unampa, kama huna anakuelewa! In short mchepuko nao unapenda tu kama wewe unavyopenda, na si kweli kuwa michepuko hipo kimaslahi!
 
Hahahaaa😂😂😂😂😂😂 Umejua kunichekesha!

Ha! shauri yako bintikiziwi angekuwa mume wangu huyo ningekutoa macho uwe Binti Kipofu mume anauma mama ila ndo hivyo in some cases inabidi tu uwe mpole mtu kuchepuka kuna sababu nyingi sa zingine kabla hujavamia mtu inabidi ujitathmini kwanza kwa nini kachepuka ila ndoa za siku hizi ngumu jamani.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaa sijaona mchepuko anasukuma v8 mtakua wa vikobe mpk mshangae😆😆😆!nyumba kubwa nikubwa tena hadi nikuhurumie sana na nilikupa vits hahahaaa umetumika sana,kuna kidada kimoja kihindi alikua anajidai mpk picha watsup hahahaa sasa ya pata 30z anahaha km kobe stress kibao waume zawatu wanawaachia vidonda n u find its tooooooo late!mke haachwi kirahisi ivyo .kama ww bingwa wa kudatisha datisha kijana mwenzio😂😂😂
 
...kuna wadada wamewekeza kwa waume za watu, huwaambii kitu...
hapo umewapigia mbuzi gitaa tu..!

Kwanza hakuna kitu kama mapenzi na mume wa mtu! ila kuna kuzini na mume wa mtu! hawa wadada wanapaswa kuambiwa ukweli! Hapo hakuna furaha yoyote labda kama mtu hajui furaha inafananaje! Furaha na raha ya kweli inaanzia moyoni! Dhamiri ikiwa safi! Huwezi kupata furaha ya kweli wakati dhamiri inakusuta kuwa unamwibia mwenzio, na dhamiri huwezi kuipa rushwa, itakusuta tu! Hata kama nawapigia mbuzi gitaa, tukiwapigia sana siku moja watajifunza kuucheza mziki!
 
Labda bi.mkubwa nae ana kiserengeti boy chake anaona poa tu we nenda na aunty suzzy kikazi me niache na house boy kwa raha zetu! ndoa hizi zina mambo

Inawezekana kabisa hizi ndoa za fashion mama ana hamsini zake wala hana tym,majanga
 
Hahaaa mnafanya kitu moyo unataka

Hapana! Wanafanya kitu shetani anataka! Hawapendi lakini wameshakuwa watumwa wa tamaa! Wangetamani waache lakini nguvu ya kuacha hawana! Kwa kweli ni mateso! Wengine wamepewa limbwata! Limbwata ni pepo, mtu anakuwa zoba mpaka basi!
 
Ladies always date with a married man juc because, ladies love beautiful and expensive things which their boys cannot afford them. Like it or not... This cannot stop to ladies ever in case they will continue liking luxurious an' posh life!

Its very true Alphanetcom
 
Last edited by a moderator:
Ila nna shoga angu..mume wa mtu alianza kulala sikumojamoja..ikaja wiki..now miez yuko kwake..alimpangia chumba sasa kampangia bonge jumba kimara .na kaz kamtafutia na sasa a

Usitamani kinachoendelea kwa shoga yako! Maisha ni zaidi ya Nyumba! Mungu atakupa/ameshakupa wako wa halali atakayekujengea Nyumba na ukafaidi penzi tamu la halali na moyo mweupeeee!!! Maisha yako yana thamani kuliko Nyumba! Hitaji lako ni kubwa kuliko nyumba! Unahitaji amani ya moyo ambayo haipatikani kwa pesa wala kwa kuwa na nyumba nzuri! Inapatikana kwa kumcha
Mungu.
Mimi ni mpenzi wa mapenzi halali moto moto!! Ni matamu mpaka basi!
 
Darln nimejitahidi kuongea frankly kadri nilivyoweza. Binafsi huwa sina cha kupoteza kwasababu mwanaume kwangu ni emergency.

Inawezekana alichowahi kukifanya aliyeitwa babaangu ndicho kinachonitafuna hadi keshokutwa. Japo kwa sasa nahisi kufurahia mahusiano.

Bado nina tatizo na wanaume ndio maana huwa nawaambia kabisa sana jitahidini kutulia kwa wake zenu, wanaatjiri sana watoto wao, maana kuna manyang'au yakiwadaka nje huwa wanapoteza vitu vingi sana.

Mwanaume haibiwi kwa kuwa sote tunajua wanaume hawabakwi kwa hiyo ni wao ndio ambao huwa wanaamua kuibiwa![/QUOT

Nimesoma post zako humu, kwa dhati kabisa nakupongeza kwa kuwa wazi! Kwa dhati pia nakupa pole kwa sababu umekuwa mhanga wa mazingira! Siwezi kuthubutu kukulaumu japo ni kweli kuwa unachoendelea nacho si sahihi.

Ila ninachoweza kukushauri ni kuwa angalia uwezekano wa kutengeneza maisha yako. Unasema kuwa una furaha, hiyo ni dalili ya kwanza ya tatizo lako. Huwezi kuwa na furaha na amani katika hali uliyonayo hata kama ukionekana kuwa una kila kitu na moyo wako ni shahidi katika hili. Unasema una furaha kama njia ya Ku suppress hisia kuwa kuna watu hawana tatizo kama lako, hivyo unataka uonekane kuwa uko sawa tu na wengine wakati siyo! Ndio maana unasema kuwa hata mke wake hakuzidi kitu! Hapana , anakuzidi yeye anakula kwa amani iliyo haki yake, wakati wewe unapokonya haki ya mwingine! Dhamiri yako lazima itakusuta!

Ushauri wangu kwako, you are still young! Mwambie Huyo mchepuko wako , siwezi kuendelea kuiumiza dhamiri yangu kwa kuishi na mume wa MTU! Lawama zote ni za huyo bwana lakini msamehe!

Mwombe Mungu akusamehe na akuokoe! Anza maisha mapya, vinginevyo kuna siku Mungu atasikia kilio cha huyo mama mwenye mume, huwezi jua Mungu atafanyaje? Afadhali uamue mapema wakati bado kijana, Mungu atakupa mume maana ni haki yako, mwamini Mungu!
 
Ha ha haaa lazma ujisikie vibaya hasa ukigundua mwanaume mwenyewe ndo kashachanganyikia na kusahau familia..jamani wadada tuwe na huruma japo kidogo kuiba tuibe ila sometym tuwe tunawaboost waheshim wake zao hata kwa maigizo

Tafadhali usiibe! Hakuna sababu hata kidogo ya kufanya hivyo! Si Mungu atakupa wa kwako peke yako! Nguvu zake zooote zitaishia kwako! Usipoiba hutaibiwa! Inawezekana! Halafu ukisubiri wa kwako mapenzi yake matamu sana hakuna mfano! Hakuna raha duniani kama kuishi na mume/mke kwa uaminifu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom