Mahubiri mengine bwana… ati uzalendo

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Kwa siku za karibuni tumekubaliana katika mengi yanayokwenda vibaya kama nchi. Ambacho hatukubaliani ni njia ipi na mikakati ipi itumike kuyakabili na kuyarekebisha yale tunayofanya vibaya.

Nijikite kwa moja ambalo tunakubaliana – “Watanzania wa leo hatuna uzalendo”.
Makundi yote, watawala, wanasiasa, watawaliwa na hata mafisadi wanakubali hili.

Tukirudi upande wa pili katika nini kifanyike ili kurudisha UZALENDO, hapo tunaanza kuachana. Kila mmoja anakuja na mbinu na mkakati wake. Kwa leo naomba tujikite kuangalia moja ya mikakati unayozungumziwa sana “Tutoe mafunzo juu ya uzalendo shuleni kuanzia msingi ….ikiwezekana toka chekechea”.

Binafsi naamini elimu ni mkakati mzuri katika mambo mengi lakini tunaanza lini na tunaanzaje kufundisha?

Nionavyo mimi tumekwisha anza kufundisha tena kwa bidii kubwa.
Hivi somo la ubaya wa ulevi tukimpa baba afundishe saa 5 usiku akiwa amerudi amependeza na mkononi amebeba kiroba litaelewekaje?

Hapa watoto wale hawatamwelewa na huenda wengine wakaanza kuvizia kiroba kile nao waonje waone anachafurahia baba.

Je, ni mtoto yupi atakubali mahubiri ya uzalendo wakati anafundishwa akiwa amekaa kwenye jiwe darasa la vumbi lisilo na dirisha wala mlango wakati anajua mwenzake wa jirani anasoma ulaya kwa rasilimali zetu?

Naamini tumeanza siku nyingi kuwafundisha watoto wetu somo la uzalendo, ni vile tu tunatumia njia mbaya- tunawapa machungu na kuwajengea vinyongo(wimbo wa mjomba). Mtoto anayekalia jiwe anafundishwa na anajua ubaya wa kuwa mzalendo. Kwa bahati mbaya zaidi awe na baba ambaye amefanya kazi serikalini kwa uaminifu mpaka akastaafu na sasa anaishi Manzese na anategemea pensheni kiduchu, TV ni mpaka wakatizame kwa jirani.

Naomba Great thinkers tutafakari na kujadili hili la ‘kufundisha uzalendo’.
:hungry:
 
Kwa hali ya sasa uzalendo unahitajika haraka sana na tukianzia elim ya msingi hatufiki mapema,cha msingi ni kila mtu,dini,vyombo vya habari na kila tabaka kuhubiri uzalendo kwa mifano halisi kama ukosefu wa ajira wakati nchi yetu nitajiri wa madini,ufisadi kama dowansina,richmond,epa na issue nyingine kama hizo.
 
Mi nionavyo mafisadi wamejitoa mhanga kulifundisha somo la uzalendo kwa wasio nacho. Ila tu wanalivutia pumzi hilo somo, muda si muda watu wataungana ili kuwashughulikia hawa viongozi wa siasa wanaotumikia mafisadi badala ya wananchi walowachagua.
Tanzania siyo kisiwa, na upepo unaovuma duniani dhidhi ya hawa mamumiani, hatuwezi kuukwepa sisi kwa nchi, na wananchi bahati nzuri wamekwisha jua ni nani mwanga wao. Hatabaki salama, baada ya hapo Tz yenye wazalendo ambao hawako radhi kubadilishana neti za mbu kwa mapande ya dhahabu watazaliwa na kuishi kati yetu.
Its a matter of time!
Kutegemea elimu ya darasani, ambako mwalimu amekopwa mshahara wake pamoja na marupurupu yake, na mshahara wenyewe ni wa ku-beep mahitaji yake yakiwemo yale ya msing -chakula na maradhi; tusitegemee sana huko. Turuhusu hali iliyopo ichukuwe mkondo wake tu, ndo mwisho wa ubabaishaji
 
Back
Top Bottom