Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar

Yombayomba

JF-Expert Member
Aug 23, 2006
818
214
[h=2]Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar[/h] 5 June 2012 192 views One Comment
Mwandishi Manyerere aliyefanya mahojiano haya akiwa na wanauamsho
Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano
*Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe ‘Sovereign State’, ijitawale yenyewe
*Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
*Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele
Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar hivi karibuni ilijikuta matatani, baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi wake. Mwandishi wa gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, aliyeeleza lengo kuu la Jumuiya hiyo ya Kiislamu.

JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?

Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa – mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.
Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao, kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.
Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.

JAMHURI: Je, Polisi walivamia?

Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakataa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini.
Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.
JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?

Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu kati ya mmoja wa watu waliohudhuria pale kwenye viwanja palipokuwa na mdahalo ni Maalim Musa Juma, yeye ni mmoja katika wahadhiri wala si kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, lakini ni mwalimu ambaye anahadhiri, anafundisha. Sasa siku ile yeye alikuwa si mzungumzaji, alikuwa mkaribishaji wa wazungumzaji. Walichokifanya wakati wa majira ya saa moja na kidogo usiku, yumo msikitini mwake anasomesha, alikwenda mtu ana shida naye. Alipomwita, kutoka nje kuwafuata wale watu wakamkamata kwenye kiuno, na wengine watano wamekuja wamemzoa wamemshindilia kwenye gari wakampeleka kituo cha Polisi. Wale vijana waliokuwa pale – wanafunzi na watu ambao wanampenda, na sasa kimekuwa kitu sensitive kwa sheikh kumdharau. Sasa hii dharau iliyofanyika, wananchi hawakukubali kwa hiyo wakaanza kupigiana simu wote kwamba Sheikh wetu kakamatwa, twendeni tukamdai kwanini kakamatwa, na tujue. Kama kumchukulia dhamana tumchukulie.
JAMHURI: Lipi jina sahihi la Jumuiya hii? Ni Uamsho au Muamsho?
Sheikh Farid: Hizi harakati zinazoendelea hapa nchini (Zanzibar) zinafanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ndiyo wanaofanya hizi harakati zote. Isipokuwa katika utaratibu wa mambo ya mihadhara, Jumuiya pekee ina uzoefu mkubwa kwenye mihadhara ni Jumuiya ya Uamsho.

JAMHURI: Taasisi ya kidini kwanini ijikite kwenye siasa?

Sheikh Farid: Hakuna tatizo lolote. Hakuna tatizo kikatiba, hakuna tatizo kidini yetu, hakuna tatizo kimtazamo sahihi wa wanasiasa. Kote hakuna tatizo. Mtazamo sahihi wa wanasiasa. Tumchukue Rais wetu wa hapa Zanzibar, Mheshimiwa Jumbe ameandika kitabu na kuna sura maalumu anaita “Dini na Siasa”. Kaeleza mengi. Kaeleza jinsi watu wengine walivyo katika dini zao, lakini akaelezea ama upande wa Uislamu huwezi kutenganisha dini na siasa. Hilo moja. Basi kama watu wanajua wanasiasa, huyu mwanasiasa anatamka kwenye kinywa chake. Alikuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Alikuwa pia Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na kaeleza wazi kabisa kwenye Uislamu huwezi kutenganisha na siasa.
Ukija kwenye Koran, Uislamu unahesabu kuwa dini ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, ikiwamo sehemu ndogo inayoitwa “siasa”. Siasa kwenye Uislamu au kwenye lugha ya Kiarabu, neno hilo hilo siasa kama lilivyo, maana yake ni “uongozi”, kwa hiyo uongozi ni sehemu ndogo, ni mlango katika maisha ya mwanadamu au katika dini ya Kiislamu. Kwa hiyo sisi kuzungumza siasa ni sahihi kabisa.

JAMHURI: Nyuma ya Uamsho kuna msukumo wa kisiasa?

Sheikh Farid: Uamsho haina uhusiano na CUF. Hili suala limeanza ilipokuja hii rasimu ya Katiba, ilipokuja kama rasimu, Serikali nzima iliikataa, Wazanzibari waliikataa wakaona wamedharauliwa. Iliporudi ikaja na dharau nyingine, badala ya kuletwa kama rasimu ikaletwa kuwa ni sheria sasa…kinguvu. Unaposema sheria maana yake ni nguvu, utake usitake. Ikaletwa kama sheria na ilikuwa iletwe kama rasimu. Hilo tatizo la mwanzo. Tatizo la pili, ndani ya rasimu ile kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe wakati anazindua Tume, hakuna mjadala wa Muungano mle ndani yake, ni kwenda mbele tu kuuboresha, lakini suala la kutazama mustakabali wa Zanzibar je, inafaidika na Muungano? Hilo hakuna. Imeshapita miaka 48 na hawajawahi kuulizwa huko nyuma. Sasa sisi hapa ndipo tulipoona kuna haja ya kuulizwa, na njia ya kufanya hivyo ni kupitia kura ya maoni.

JAMHURI: Kuna umuhimu wa kuwapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Sheikh Farid: Sisi tunachotaka ni kura ya maoni. Wazanzibari waseme wenyewe. Hakuna mtu amepewa kibali cha kumsemea mtu. Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari. Kila mtu aseme mwenyewe na hiyo ndiyo demokrasia, kwa hiyo sisi kama Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu tunasema iitwe kura ya maoni. Nisiseme mie, mie nitasema kwenye karatasi. Kila Mzanzibari atasema kwenye karatasi. Kura ya maoni ni nyepesi tu.

JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?

Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo. Lakini tunashangazwa vilevile, tumechoma makanisa, sisi ameuliwa imam ndani ya msikiti na Jeshi la Polisi…ameuliwa imam ndani ya msikiti, huko Mwembechai kwenu huko Dar es Salaam ameuliwa Muislamu ndani ya msikiti. Acha kuchoma makanisa. Sisi tunalaani uvunjifu wa amani wa aina yoyote – ikiwa wa ubaguzi wa kidini wa kuchoma makanisa, ikiwa wa kuwahujumu watu, tukubali haya si mafunzo maana hata kwenye nyumba yangu wamekuja wamehujumu ndani, wamepiga mabomu ndani ya nyumba, wamevunja mlango.

JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?

Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?

JAMHURI: Marekani majimbo yale ni nchi – ni Muungano, mbona majimbo hayana mamlaka kamili kama nchi?

Sheikh Farid: Mbona upo muungano tofauti na huo. Kama Umoja wa Ulaya si upo? Upo vipi? Katika Umoja wa Mataifa si kila nchi ina kiti?

JAMHURI: Huo si muungano ni kama jumuiya tu.

Sheikh Farid: Huo ni muungano, si wameungana katika vitu maalumu? Wamarekani wameamua wao vile. Sisi tumeamua hivi. Wao hatuwasemei. Sie tunaamua tunachotaka sie. Na sisi hawezi kutulazimisha mtu tuamue kwa akili za Kimarekani. Wamarekani wataamua wao wenyewe Kimarekani, haki za Kizanzibari zitaamuliwa Kizanzibari-Zanzibari.

JAMHURI: Ungependa Muungano wa uwe wa namna gani?

Sheikh Farid: Mie ninachosema ule mchakato wa Katiba imekuwa sawa na kumchukua ng’ombe na gari ya ng’ombe halafu ng’ombe ukamweka nyuma gari ya ng’ombe ukaweka mbele. Au mashine ukaweka nyuma, gari ukaweka mbele. Sijui itakwenda vipi. Sasa tunashangaa, watu wataalamu wana akili lakini inaonyesha akili zao zimefika mahali wanatuona sisi wapumbavu. Sisi bwana tunasema ilivyo kitu kinachowafungamanisha Wazanzibari na Watanganyika ni Muungano. Ninyi mnataka kujadili Katiba ya Muungano, hili tatizo la Muungano kwanini msilizungumze mwanzo? Hili la kuzungumza mwanzo. Kwanza, lizungumzwe hili kwanza mpaka likae sawasawa halafu ndiyo tuzungumze Katiba.
Sasa unasema mimi na wewe tunataka kufanya biashara njoo tufunge mkataba mimi na wewe. Si tuzungumze tukubaliane kwanza halafu ndiyo tuandike mkataba kwa sababu Katiba ndiyo umefunga kila kitu. Kitu kinachotufungamanisha tukizungumze mwanzo. Wananchi wapewe fursa wazungumze mwanzo. Watu wanapewa fursa hizo wasiokuwa na nchi mwanzo…hii ni nchi. Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.

JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?

Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang’ang’ania hiki tu!

JAMHURI: Muungano ukivunjika, nini hatima ya Wazanzibari wanaoishi/waliowekeza Bara?

Sheikh Farid: Jawabu moja, wewe huwajui Watanzania wanaofanya biashara Kenya? Uganda? Hatima yao ipo vipi? Sasa ninyi inaonyesha kuna watu wana fikra mbovu katika vichwa wanaona maana yake tukiwa hivi (tukitengana) tutakuwa maadui, hata! Udugu lazima utabakia. Tumeoa kule. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar usingizi wake (mkewe) ni wa kule (Bara) au hujui wewe? Hatuwezi kuachana bwana, watu watabakia, mapenzi yapo, undugu upo, ujirani mwema kabisa, waliokuwapo hapa Watanganyika watabakia, Wakristo hapa watabakia, itakuwa kila kitu kina utaratibu. Si maana yake kwamba mmetengana muwadhulumu wale ndugu zenu (walio Bara). Mkiwadhulumu sawa! Sisi kawaida yetu hatuko hivyo.

Kwa hisani ya http://www.kwanzajamii.com/
 
Farid aliehojiwa ndie yule Aliekuwa akiwahamasisha Wafuasi Wake KUFA kwa ahadi ya kwenda PEPONI? Na sasa anaongea Asali..........................Kumbe taratibu unazifahamu?
Halafu kuna Vijana wa Watu mkawadhamini haraka tena..............Ebooo!!
 
Shukran Sheikh Farid. Msimamo huo huo, hakuna kurudi nyuma. Mpaka kieleweke.
 
shukran sheikh farid. Msimamo huo huo, hakuna kurudi nyuma. Mpaka kieleweke.

kama walikwpa siku nyingi sasa ni finali. Kwa akili ya jk hili haliwezi kabisa. Jamani urais siyo masiala.k
j uijivuta kama ulivyozoea muungano unakufa kama ccm inavyokufia mikononi. Leadership is about taking quick decisions on time. Jk ulitamani sana kuwa rais sasa umeona mwenyewe hii kazi siyo mchezo! Hata wale wengine wanaotamani wajifunze kama akili yako ya panzi acha utaaibika kama jk.
Uamsho wako serious and focused kuliko rais jk na shein
 
Pole pole tunaelekea kufika. Mimi ni muungano wa nchi moja Tanzania ama muungano ufe. Baada ya mpito huu tuliomo kama hatuungani kama nchi moja maana yake hatutaaminiana hadi huko mbele na katika hali hiyo muungano.

Mimi sina hofu muungano huu wa mabishano ukifa, tena ufe haraka. Maana bado tutashirikiana kwa utulivu mzuri zaidi kupitia shirikisho la Afrika ya Mashariki. Udugu, ujirani na urafiki utaendelea tu na hasa ujirani kwa faida ya nchi mbili hizi na pengine baadaye nchi zote mbili zitatambua walichokuwa nacho, walichokosa na walichopata.
 
mtu wenye hoja amkosewe nu ukweli mtupu ameusema ila kuwa watanganyika wamekosa uzalendo wa taifa lao na kujaribu kutia fitna za udini na propaganda ndani ya magazeti yaooo
 
hoja zilizotolewa na shekh ni nzuri na zinavutia, lakini binafsi sijaelewa kama SMZ wamewachagua wanauamusho kuwa wasemaji wa SMZ? pili, hawa wanauamusho ndio kusema kwamba uwepo wa makanisa Nzanzibar ni sehemu ya kero za muunngano? Je kuna haja ya Bara kuanza kuchoma misikiti ili muungano uwe balanced kama wanavyuotaka kutuaminisha? je hoja za G55 uondoshwaji wa makanisa zannzibar ilikuwa moja ya hoja zao? Nisaidieni
 
Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano:
• Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe ‘Sovereign State', ijitawale yenyewe
• Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
• Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele

Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar hivi karibuni ilijikuta matatani, baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi wake. Mwandishi wa gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, aliyeeleza lengo kuu la Jumuiya hiyo ya Kiislamu.

JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?
Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa – mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.
Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao, kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.
Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.

JAMHURI: Je, Polisi walivamia?
Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakataa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini. Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.

JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?
Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu kati ya mmoja wa watu waliohudhuria pale kwenye viwanja palipokuwa na mdahalo ni Maalim Musa Juma, yeye ni mmoja katika wahadhiri wala si kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, lakini ni mwalimu ambaye anahadhiri, anafundisha. Sasa siku ile yeye alikuwa si mzungumzaji, alikuwa mkaribishaji wa wazungumzaji. Walichokifanya wakati wa majira ya saa moja na kidogo usiku, yumo msikitini mwake anasomesha, alikwenda mtu ana shida naye. Alipomwita, kutoka nje kuwafuata wale watu wakamkamata kwenye kiuno, na wengine watano wamekuja wamemzoa wamemshindilia kwenye gari wakampeleka kituo cha Polisi. Wale vijana waliokuwa pale – wanafunzi na watu ambao wanampenda, na sasa kimekuwa kitu sensitive kwa sheikh kumdharau. Sasa hii dharau iliyofanyika, wananchi hawakukubali kwa hiyo wakaanza kupigiana simu wote kwamba Sheikh wetu kakamatwa, twendeni tukamdai kwanini kakamatwa, na tujue. Kama kumchukulia dhamana tumchukulie.

JAMHURI: Lipi jina sahihi la Jumuiya hii? Ni Uamsho au Muamsho?
Sheikh Farid: Hizi harakati zinazoendelea hapa nchini (Zanzibar) zinafanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ndiyo wanaofanya hizi harakati zote. Isipokuwa katika utaratibu wa mambo ya mihadhara, Jumuiya pekee ina uzoefu mkubwa kwenye mihadhara ni Jumuiya ya Uamsho.

JAMHURI: Taasisi ya kidini kwanini ijikite kwenye siasa?
Sheikh Farid: Hakuna tatizo lolote. Hakuna tatizo kikatiba, hakuna tatizo kidini yetu, hakuna tatizo kimtazamo sahihi wa wanasiasa. Kote hakuna tatizo. Mtazamo sahihi wa wanasiasa. Tumchukue Rais wetu wa hapa Zanzibar, Mheshimiwa Jumbe ameandika kitabu na kuna sura maalumu anaita "Dini na Siasa". Kaeleza mengi. Kaeleza jinsi watu wengine walivyo katika dini zao, lakini akaelezea ama upande wa Uislamu huwezi kutenganisha dini na siasa. Hilo moja. Basi kama watu wanajua wanasiasa, huyu mwanasiasa anatamka kwenye kinywa chake. Alikuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Alikuwa pia Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na kaeleza wazi kabisa kwenye Uislamu huwezi kutenganisha na siasa.
Ukija kwenye Koran, Uislamu unahesabu kuwa dini ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, ikiwamo sehemu ndogo inayoitwa "siasa". Siasa kwenye Uislamu au kwenye lugha ya Kiarabu, neno hilo hilo siasa kama lilivyo, maana yake ni "uongozi", kwa hiyo uongozi ni sehemu ndogo, ni mlango katika maisha ya mwanadamu au katika dini ya Kiislamu. Kwa hiyo sisi kuzungumza siasa ni sahihi kabisa.

JAMHURI: Nyuma ya Uamsho kuna msukumo wa kisiasa?
Sheikh Farid: Uamsho haina uhusiano na CUF. Hili suala limeanza ilipokuja hii rasimu ya Katiba, ilipokuja kama rasimu, Serikali nzima iliikataa, Wazanzibari waliikataa wakaona wamedharauliwa. Iliporudi ikaja na dharau nyingine, badala ya kuletwa kama rasimu ikaletwa kuwa ni sheria sasa…kinguvu. Unaposema sheria maana yake ni nguvu, utake usitake. Ikaletwa kama sheria na ilikuwa iletwe kama rasimu. Hilo tatizo la mwanzo. Tatizo la pili, ndani ya rasimu ile kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe wakati anazindua Tume, hakuna mjadala wa Muungano mle ndani yake, ni kwenda mbele tu kuuboresha, lakini suala la kutazama mustakabali wa Zanzibar je, inafaidika na Muungano? Hilo hakuna. Imeshapita miaka 48 na hawajawahi kuulizwa huko nyuma. Sasa sisi hapa ndipo tulipoona kuna haja ya kuulizwa, na njia ya kufanya hivyo ni kupitia kura ya maoni.

JAMHURI: Kuna umuhimu wa kuwapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
Sheikh Farid: Sisi tunachotaka ni kura ya maoni. Wazanzibari waseme wenyewe. Hakuna mtu amepewa kibali cha kumsemea mtu. Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari. Kila mtu aseme mwenyewe na hiyo ndiyo demokrasia, kwa hiyo sisi kama Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu tunasema iitwe kura ya maoni. Nisiseme mie, mie nitasema kwenye karatasi. Kila Mzanzibari atasema kwenye karatasi. Kura ya maoni ni nyepesi tu.

JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?
Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo. Lakini tunashangazwa vilevile, tumechoma makanisa, sisi ameuliwa imam ndani ya msikiti na Jeshi la Polisi…ameuliwa imam ndani ya msikiti, huko Mwembechai kwenu huko Dar es Salaam ameuliwa Muislamu ndani ya msikiti. Acha kuchoma makanisa. Sisi tunalaani uvunjifu wa amani wa aina yoyote – ikiwa wa ubaguzi wa kidini wa kuchoma makanisa, ikiwa wa kuwahujumu watu, tukubali haya si mafunzo maana hata kwenye nyumba yangu wamekuja wamehujumu ndani, wamepiga mabomu ndani ya nyumba, wamevunja mlango.

JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?
Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?

JAMHURI: Marekani majimbo yale ni nchi – ni Muungano, mbona majimbo hayana mamlaka kamili kama nchi?
Sheikh Farid: Mbona upo muungano tofauti na huo. Kama Umoja wa Ulaya si upo? Upo vipi? Katika Umoja wa Mataifa si kila nchi ina kiti?

JAMHURI: Huo si muungano ni kama jumuiya tu.
Sheikh Farid: Huo ni muungano, si wameungana katika vitu maalumu? Wamarekani wameamua wao vile. Sisi tumeamua hivi. Wao hatuwasemei. Sie tunaamua tunachotaka sie. Na sisi hawezi kutulazimisha mtu tuamue kwa akili za Kimarekani. Wamarekani wataamua wao wenyewe Kimarekani, haki za Kizanzibari zitaamuliwa Kizanzibari-Zanzibari.

JAMHURI: Ungependa Muungano wa uwe wa namna gani?
Sheikh Farid: Mie ninachosema ule mchakato wa Katiba imekuwa sawa na kumchukua ng'ombe na gari ya ng'ombe halafu ng'ombe ukamweka nyuma gari ya ng'ombe ukaweka mbele. Au mashine ukaweka nyuma, gari ukaweka mbele. Sijui itakwenda vipi. Sasa tunashangaa, watu wataalamu wana akili lakini inaonyesha akili zao zimefika mahali wanatuona sisi wapumbavu. Sisi bwana tunasema ilivyo kitu kinachowafungamanisha Wazanzibari na Watanganyika ni Muungano. Ninyi mnataka kujadili Katiba ya Muungano, hili tatizo la Muungano kwanini msilizungumze mwanzo? Hili la kuzungumza mwanzo. Kwanza, lizungumzwe hili kwanza mpaka likae sawasawa halafu ndiyo tuzungumze Katiba.
Sasa unasema mimi na wewe tunataka kufanya biashara njoo tufunge mkataba mimi na wewe. Si tuzungumze tukubaliane kwanza halafu ndiyo tuandike mkataba kwa sababu Katiba ndiyo umefunga kila kitu. Kitu kinachotufungamanisha tukizungumze mwanzo. Wananchi wapewe fursa wazungumze mwanzo. Watu wanapewa fursa hizo wasiokuwa na nchi mwanzo…hii ni nchi. Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.

JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?
Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang'ang'ania hiki tu!

JAMHURI: Muungano ukivunjika, nini hatima ya Wazanzibari wanaoishi/waliowekeza Bara?
Sheikh Farid: Jawabu moja, wewe huwajui Watanzania wanaofanya biashara Kenya? Uganda? Hatima yao ipo vipi? Sasa ninyi inaonyesha kuna watu wana fikra mbovu katika vichwa wanaona maana yake tukiwa hivi (tukitengana) tutakuwa maadui, hata! Udugu lazima utabakia. Tumeoa kule. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar usingizi wake (mkewe) ni wa kule (Bara) au hujui wewe? Hatuwezi kuachana bwana, watu watabakia, mapenzi yapo, undugu upo, ujirani mwema kabisa, waliokuwapo hapa Watanganyika watabakia, Wakristo hapa watabakia, itakuwa kila kitu kina utaratibu. Si maana yake kwamba mmetengana muwadhulumu wale ndugu zenu (walio Bara). Mkiwadhulumu sawa! Sisi kawaida yetu hatuko hivyo.

CHANZO:
“Tunataka Zanzibar iwe na mamlaka yake yenyewe“ – Mahojiano ya Jamhuri na Uamsho « Uamsho Zanzibar
 
Hata sie hatuutaki huo muungano.
Bakini za kisiwa chenu.
Mmetunyonya kiasi cha kutosha, sasa twalitua zigo la kinyesi
 
Naona kama hawa jamaa wamejipanga kwa hoja. Ila la kuchoma moto makanisa limewaharibia sana.
 
Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano:
• Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe ‘Sovereign State’, ijitawale yenyewe
• Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
• Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele

Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar hivi karibuni ilijikuta matatani, baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi wake. Mwandishi wa gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, aliyeeleza lengo kuu la Jumuiya hiyo ya Kiislamu.

JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?
Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa – mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.
Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao, kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.
Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.

JAMHURI: Je, Polisi walivamia?
Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakataa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini. Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.

JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?
Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu kati ya mmoja wa watu waliohudhuria pale kwenye viwanja palipokuwa na mdahalo ni Maalim Musa Juma, yeye ni mmoja katika wahadhiri wala si kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, lakini ni mwalimu ambaye anahadhiri, anafundisha. Sasa siku ile yeye alikuwa si mzungumzaji, alikuwa mkaribishaji wa wazungumzaji. Walichokifanya wakati wa majira ya saa moja na kidogo usiku, yumo msikitini mwake anasomesha, alikwenda mtu ana shida naye. Alipomwita, kutoka nje kuwafuata wale watu wakamkamata kwenye kiuno, na wengine watano wamekuja wamemzoa wamemshindilia kwenye gari wakampeleka kituo cha Polisi. Wale vijana waliokuwa pale – wanafunzi na watu ambao wanampenda, na sasa kimekuwa kitu sensitive kwa sheikh kumdharau. Sasa hii dharau iliyofanyika, wananchi hawakukubali kwa hiyo wakaanza kupigiana simu wote kwamba Sheikh wetu kakamatwa, twendeni tukamdai kwanini kakamatwa, na tujue. Kama kumchukulia dhamana tumchukulie.

JAMHURI: Lipi jina sahihi la Jumuiya hii? Ni Uamsho au Muamsho?
Sheikh Farid: Hizi harakati zinazoendelea hapa nchini (Zanzibar) zinafanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ndiyo wanaofanya hizi harakati zote. Isipokuwa katika utaratibu wa mambo ya mihadhara, Jumuiya pekee ina uzoefu mkubwa kwenye mihadhara ni Jumuiya ya Uamsho.

JAMHURI: Taasisi ya kidini kwanini ijikite kwenye siasa?
Sheikh Farid: Hakuna tatizo lolote. Hakuna tatizo kikatiba, hakuna tatizo kidini yetu, hakuna tatizo kimtazamo sahihi wa wanasiasa. Kote hakuna tatizo. Mtazamo sahihi wa wanasiasa. Tumchukue Rais wetu wa hapa Zanzibar, Mheshimiwa Jumbe ameandika kitabu na kuna sura maalumu anaita “Dini na Siasa”. Kaeleza mengi. Kaeleza jinsi watu wengine walivyo katika dini zao, lakini akaelezea ama upande wa Uislamu huwezi kutenganisha dini na siasa. Hilo moja. Basi kama watu wanajua wanasiasa, huyu mwanasiasa anatamka kwenye kinywa chake. Alikuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Alikuwa pia Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na kaeleza wazi kabisa kwenye Uislamu huwezi kutenganisha na siasa.
Ukija kwenye Koran, Uislamu unahesabu kuwa dini ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, ikiwamo sehemu ndogo inayoitwa “siasa”. Siasa kwenye Uislamu au kwenye lugha ya Kiarabu, neno hilo hilo siasa kama lilivyo, maana yake ni “uongozi”, kwa hiyo uongozi ni sehemu ndogo, ni mlango katika maisha ya mwanadamu au katika dini ya Kiislamu. Kwa hiyo sisi kuzungumza siasa ni sahihi kabisa.

JAMHURI: Nyuma ya Uamsho kuna msukumo wa kisiasa?
Sheikh Farid: Uamsho haina uhusiano na CUF. Hili suala limeanza ilipokuja hii rasimu ya Katiba, ilipokuja kama rasimu, Serikali nzima iliikataa, Wazanzibari waliikataa wakaona wamedharauliwa. Iliporudi ikaja na dharau nyingine, badala ya kuletwa kama rasimu ikaletwa kuwa ni sheria sasa…kinguvu. Unaposema sheria maana yake ni nguvu, utake usitake. Ikaletwa kama sheria na ilikuwa iletwe kama rasimu. Hilo tatizo la mwanzo. Tatizo la pili, ndani ya rasimu ile kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe wakati anazindua Tume, hakuna mjadala wa Muungano mle ndani yake, ni kwenda mbele tu kuuboresha, lakini suala la kutazama mustakabali wa Zanzibar je, inafaidika na Muungano? Hilo hakuna. Imeshapita miaka 48 na hawajawahi kuulizwa huko nyuma. Sasa sisi hapa ndipo tulipoona kuna haja ya kuulizwa, na njia ya kufanya hivyo ni kupitia kura ya maoni.

JAMHURI: Kuna umuhimu wa kuwapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
Sheikh Farid: Sisi tunachotaka ni kura ya maoni. Wazanzibari waseme wenyewe. Hakuna mtu amepewa kibali cha kumsemea mtu. Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari. Kila mtu aseme mwenyewe na hiyo ndiyo demokrasia, kwa hiyo sisi kama Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu tunasema iitwe kura ya maoni. Nisiseme mie, mie nitasema kwenye karatasi. Kila Mzanzibari atasema kwenye karatasi. Kura ya maoni ni nyepesi tu.

JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?
Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo. Lakini tunashangazwa vilevile, tumechoma makanisa, sisi ameuliwa imam ndani ya msikiti na Jeshi la Polisi…ameuliwa imam ndani ya msikiti, huko Mwembechai kwenu huko Dar es Salaam ameuliwa Muislamu ndani ya msikiti. Acha kuchoma makanisa. Sisi tunalaani uvunjifu wa amani wa aina yoyote – ikiwa wa ubaguzi wa kidini wa kuchoma makanisa, ikiwa wa kuwahujumu watu, tukubali haya si mafunzo maana hata kwenye nyumba yangu wamekuja wamehujumu ndani, wamepiga mabomu ndani ya nyumba, wamevunja mlango.

JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?
Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?

JAMHURI: Marekani majimbo yale ni nchi – ni Muungano, mbona majimbo hayana mamlaka kamili kama nchi?
Sheikh Farid: Mbona upo muungano tofauti na huo. Kama Umoja wa Ulaya si upo? Upo vipi? Katika Umoja wa Mataifa si kila nchi ina kiti?

JAMHURI: Huo si muungano ni kama jumuiya tu.
Sheikh Farid: Huo ni muungano, si wameungana katika vitu maalumu? Wamarekani wameamua wao vile. Sisi tumeamua hivi. Wao hatuwasemei. Sie tunaamua tunachotaka sie. Na sisi hawezi kutulazimisha mtu tuamue kwa akili za Kimarekani. Wamarekani wataamua wao wenyewe Kimarekani, haki za Kizanzibari zitaamuliwa Kizanzibari-Zanzibari.

JAMHURI: Ungependa Muungano wa uwe wa namna gani?
Sheikh Farid: Mie ninachosema ule mchakato wa Katiba imekuwa sawa na kumchukua ng’ombe na gari ya ng’ombe halafu ng’ombe ukamweka nyuma gari ya ng’ombe ukaweka mbele. Au mashine ukaweka nyuma, gari ukaweka mbele. Sijui itakwenda vipi. Sasa tunashangaa, watu wataalamu wana akili lakini inaonyesha akili zao zimefika mahali wanatuona sisi wapumbavu. Sisi bwana tunasema ilivyo kitu kinachowafungamanisha Wazanzibari na Watanganyika ni Muungano. Ninyi mnataka kujadili Katiba ya Muungano, hili tatizo la Muungano kwanini msilizungumze mwanzo? Hili la kuzungumza mwanzo. Kwanza, lizungumzwe hili kwanza mpaka likae sawasawa halafu ndiyo tuzungumze Katiba.
Sasa unasema mimi na wewe tunataka kufanya biashara njoo tufunge mkataba mimi na wewe. Si tuzungumze tukubaliane kwanza halafu ndiyo tuandike mkataba kwa sababu Katiba ndiyo umefunga kila kitu. Kitu kinachotufungamanisha tukizungumze mwanzo. Wananchi wapewe fursa wazungumze mwanzo. Watu wanapewa fursa hizo wasiokuwa na nchi mwanzo…hii ni nchi. Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.

JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?
Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang’ang’ania hiki tu!

JAMHURI: Muungano ukivunjika, nini hatima ya Wazanzibari wanaoishi/waliowekeza Bara?
Sheikh Farid: Jawabu moja, wewe huwajui Watanzania wanaofanya biashara Kenya? Uganda? Hatima yao ipo vipi? Sasa ninyi inaonyesha kuna watu wana fikra mbovu katika vichwa wanaona maana yake tukiwa hivi (tukitengana) tutakuwa maadui, hata! Udugu lazima utabakia. Tumeoa kule. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar usingizi wake (mkewe) ni wa kule (Bara) au hujui wewe? Hatuwezi kuachana bwana, watu watabakia, mapenzi yapo, undugu upo, ujirani mwema kabisa, waliokuwapo hapa Watanganyika watabakia, Wakristo hapa watabakia, itakuwa kila kitu kina utaratibu. Si maana yake kwamba mmetengana muwadhulumu wale ndugu zenu (walio Bara). Mkiwadhulumu sawa! Sisi kawaida yetu hatuko hivyo.

CHANZO:
“Tunataka Zanzibar iwe na mamlaka yake yenyewe“ – Mahojiano ya Jamhuri na Uamsho « Uamsho Zanzibar

ANGALIZO JUU YA ALIYOYASEMA HUYO SHEIKH FARID:

kwanza kabisa nakilaani hicho kikundi pamoja na Viongozi wao!! na washukuru sana Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni legelege kwa sababu CCM ni legelege na Nyerere alishasema!! "Bila CCM Madhubuti Nchi yetu Itayumba" tunaona kweli NCHI INAYUMBA

Nakuhakikishia hawa watu kipindi cha Waasisi wetu (Nyerere na Karume) wasingethubutu sio tu kuyasema hayo wanayoyaiita maslahi ya Zanzibar bali hata kuanzisha hicho kijikundi. Wangekuwa wamekimbia nchi au wapo kolokoloni wananyea debe!! kwa UHAINI!

Nimrejeshe Sheikh Farid kwenye Historia ya Zanzibar!! Sheikh Farid Zanzibar haikuota kama UYOGA na Wapemba na Waunguja wakawa Juu yake. Kijiografia Visiwa vile vilikuwa ni ardhi moja iliyounganika miaka mamilioni yaliyopita!! Kama elimu dunia tatizo rejea tu darasani.

Mimi najiuliza hawa muamusho wanaijua Zanzibar historia yake au ndiyo ule usemi "Mtoto wa Mjomba analilia URITHI?"

Hebu tujikumbushe Zanzibar Kabla ya Mwarabu ilikuaje?

Bisha mpaka ujilipue lMwarabu alivyofika Zanzibar alikuta wenyeji wa visiwa vile walioishi kwa salama salmini na wengi wao walihamia kule kama wavuvi wakitokea BARA!! Waarabu wanajua!! Waafrika sisi tunajua hivyo!! Sasa basi Waarabu kwa kutumia dini walijinufaisha kiuchumi sana kupitia visiwa hivyo na utamu ulivyozidi wakahamia na Bara eti wakijifanya wanasambaza dini lakini lengo kubwa ni kujinufaisha kiuchumi.

Kwahiyo!! Mwarabu alivyokuja, hakukuta Wabara na Wavisiwani wanagombana na hakuna historia inayoonyesha Waafrika wa Zanzibar na Bara wamewahi kupigana vita!! Hiyo inadhihirisha Wabara na Wavisiwani ni ndugu.

Angalizo!!! Mbara sio lazima atokee Karagwe!! Mbara huyu ni wa Bagamoyo au Pangani. MWARABU alilijua, analijua na atalijua hivyo.!!

Zanzibar Kipindi cha Ukoloni!!!

Lazima tukubali wazungu walituzidi ujanja. kwanza kwa kuijua jiografia ya Dunia na pili kufanikiwa kuchora ramani yake na kugawana vipande vya ardhi watakavyo!! Walifanikiwa kutugawa kwa michoro ya ramani lakini bado tamaduni, ustarabu na muingiliano wa Bara na Visiwani uliendelea kudumu. Na hawa wazungu walielewa hilo na ndiyo maana wakamwachia Mwarabu atawale watu wenye silka moja mpaka maili kumi ndani ya Bara!! Kwa hiyo lengo likawa bado liko palepale!!! KUTOWATENGANISHA HAWA NDUGU WAWILI.

Zanzibar Kipindi cha Kudai UHURU na MAPINDUZI!!

Natamani Manyerere angemuuliza huyu Sheikh kwamba Je, anaamini katika Mapinduzi ya mwaka 1964!!????

Hapo ndipo tungejua huyu Sheikh anadai Zanzibar kwa maslahi ya nani? Lakini nataka nimwambie hivi, MZEE KARUME
pamoja na kuzunguka sana duniani na kujifunza mambo mengi, alifahamu asili yake ni wapi.

Alitambua kwa dhati ya moyo wake kwamba ili Zanzibar ipate UHURU wake halisi hakukuwa na budi kuomba msaada kwa ndugu zao Wabara. Mohamed Babu alilijua, Sheikh Thabit Kombo alilijua na hata Mzee Nasoro Moyo analijua hili nashangaa hataki kueleza ukweli ili watu wengine wajue.!! Msaada wa wanandugu hawa wawili (Bara na Visiwani) Walifanikisha kuvunja tawala dhalimu ya kisultani iliyodumu kwa miaka mamia kadhaa

Wanandugu wenye visiwa vyao mara baada ya MAPINDUZI walijirudi na kuwa pamoja kupitia Muungano na kwa kuchanganya UDONGO WA PANDE ZOTE MBILI!! Nyie UAMUSHO ZOEZI LA KUCHANGANYA UDONGO SI DOGO Hawa Waasisi walijua maana yake!! Msicheze na fikra za hawa wazee na wala msione walikosea!!1

Sasa basi, hawa watu wanatia shaka sana!! Sielewi wanaitaka Zanzibar IPI? Ndiyo hawahawa walikuwa hawayatambui Mapinduzi ya Mwaka 1964, Walivyoona wanakosa kuungwa Mkono wanakuja na Hoja hiyo ya Sovereignty.

Uamusho ni zao la Sultan anayetaka kurudi kwa mlango wa Nyuma!! Siamini na sitaamin kama kweli Yeyote anayeamini juu ya Mapinduzi ya 1964 atapuuza Muungano huu uliokuwepo hata kabla ya kuja kwa Mwarabu!!.

WASISAHAU!!
Kwa mujibu wa Tafiti zilizopo Visiwa hivi miaka 100 ijayo vinaweza visiwepo katika USO WA DUNIA. SASA WAKIWA WANADAI HAYO, WAKUMBUKE NA WAJUKUU NA VITUKUU VYAO VITAKAA WAPI?

MUNGU IBARIKI ZANZIBAR YA WAAFRIKA NA SI YA VIBARAKA KUTOKA KULE @@@@@@????

hihi ndio historia uliyoipata kwa muadhama Pengo?????
 
Dah.. Nimemuelewa vizuri Sheikh.. Ila awe wa kwanza kuelimisha vijana na Wazanzibari wengine ambao hawaifahamu historia na hawana uelewa wa kutosha wa kuchambua mambo,kuwa wawe specific kwenye madai yao na wajue adui yao ni nani kwa maendeleo yao.. Wasikurupuke tu kufanya fujo pasipo na hoja za msingi...
 
Kama Hoja hizo za Shekh zina Mshiko wangetumia taratibu zilizopo kuwasilisha hoja hizo. Lakini walijua na wanajua katika vikao Halali hoja hizo hazitafua Dafu. Ndio maana Wakaingia na Mkwara wa kuhamasisha Watu kwa mapambano na Ikibidi hata Ugaidi utumike (Fuatilia vizuri kanda zao za mihadhara) Chachu inayopatikana ni ya Kigaidi. Ahadi ya PEPO kwa maisha, wanaohamasishwa ni Vijana wadogo tu hakuna tofauti na Talaban.
Walipoitwa na Serekali kuonywa nadhani walivimba Vichwa wakidhani wameogopewa, hivyo wakaongeza Presha kwa Kuandamana na Kuingilia Polisi katika Utendaji wa Kazi zao. Polisi Ikawabidi wachukue hatua za ziada.
Matokeo yake tumewasikia kwa Kauili zao Ma AMIRI faridi na Azani wakidai kuwa Nyumba zao zilishambuliwa na Polisi na milango kuvunjwa. Hii ina maana Baada ya waheshimiwa hao kutoa Amri kwa Wafuasi wao wakizunguke kituo cha Polisi wao waliingia mitini.
Aya zote na Hadith zote Imekosekana hata moja ya kuwaambia kuwa AMIRI ni wa Vitendo anakuwa mstari wa mbele??
Mmeshawahdamini wale vijana wa watu? Ebooo!
 
Naona kama hawa jamaa wamejipanga kwa hoja. Ila la kuchoma moto makanisa limewaharibia sana.

Siku moja baada kuchomwa kanisa, viongozi wa UAMSHO walitoa tamko rasmi na katika tamko hilo walikanisha kabisa kuhusika na uchomaji makanisa.

Hili hapa ni tamko lilotolewa:

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI) للجنة الدعوة الإسلامية

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com

MKUNAZINI ZANZIBAR
Tarehe 27MAY2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.
Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ

SOURCE: Uamsho wakanusha kuhusika na uchomaji wa kanisa |
 
Back
Top Bottom