Mahakama ya Kisutu yawahukumu wezi wa EPA, Maranda na Farijala miaka 22 jela

miaka 5=miaka miwili na nusu!
2013 WAPO BARABARANI, wanaendelea kutafuna senti zao taratibu!

sivyo kama unavyi fikilia wamehukumiwa miaka 21 katika kuhesabu usiku na mchana kwa jumla ya makosa yote sasa watatumikia kifungo cha miaka mitano net bila kupungua kwa maana hiyo imepunguzwa kutoka 21 mpk mitano ndiyo watakayotumikia mkuu
 
sivyo kama unavyi fikilia wamehukumiwa miaka 21 katika kuhesabu usiku na mchana kwa jumla ya makosa yote sasa watatumikia kifungo cha miaka mitano net bila kupungua kwa maana hiyo imepunguzwa kutoka 21 mpk mitano ndiyo watakayotumikia mkuu

mkuu ... miaka 21 ni jumla ya adhabu kwa kujumlisha adhabu ya miaka ya kifungo kwa kila kosa .... sasa wamechukua adhabu yenye kifungo kirefu zaidi na kuifanya iendane kwa pamoja na adhabu za vifungo vya makosa mengine ....pale lupango wanahesabu day and night....! tena ukitumikia lupango kwa nidhamu wana ku grant parole

PJ yupo sahihi
 
Kwa hiyo ndio wameamua kulimaliza muvi la EPA kwa style hii?

mbona wahusika wakuu hatujajua hitimisho lao?
 
Mkuu naungana na wewe kabisa, vifungo vikiambatana yaani kifungu cha juu ndicho huchukuliwa na vikifuatana hii ndiyo balaa ukimaliza kimoja unaanza kingine. Jibu rahisi ni kifungu kirefu cha hao jamaa ndicho watakachotumikia na wakifika jela wanatolewa 1/3 ya kifungo chao. Mf. Mtu amehukumiwa 6yrs, 1/3 ni 2yrs basi atatumikia 4yrs na kisha sentence itahesabika ni full.
Kwa maana hiyo hao jamaa kama ni 3yrs sentence basi watatumikia miaka 2 n.k
Hiyo ni sheria ya Tanzania Prisons Services ili kuwaondolea mentality ya kuwa jela ni sehemu ya adhabu lakini ukienda against laws zao huindoa taratibu hiyo remission.

Tusubiri msamaha wa rais kama wasipotolewa ndo tuamini kuwa watatumikia kifungo hicho.
 
I hope ni habari za kweli

CHADEMA watanasema hao jamaa wameonewa

What a shame kwa Chama kama Chadema , angehukumiwa Chenge na Lowasa pia wangesema wanaonewa na Kikwete

Damned if do damned if you dont!!
Wewe Ndg yangu Maundumula unaona ni haki???????? Wako wapi wezi wa KAGODA????Tena wa fedha nyingi Billion Arobaini, hasa huyO Rostam Aziz ambaye kwa ushahidi wa Manjis huyo ndiye KAGODA. Wengine Mhs Raisi alisema warudishe fedha wasamehewe, uliona wapi mwizi arudishe alicho iba yaani arudishe exhibit eti asamehewe ni sheria ya nchi gani hiyo.Huo ni mchezo wa kuigiza, ndio maana mwendesha mashitaka mkuu wa serikali akasema kuwa mwenye ushahidi wa ufisadi wa KAGODA ampelekee. Yaani huyo jamaa akae tu ofisini alipwe mamilioni ya fedha za mshahara watu wafanye kazi ya kumpelekea ushahidi wa KAGODA, kama vile hajui. Tumechoka na longo longo za hii serikali, tanahitaji katiba mpya tunahitaji mabadiliko , period !!!!!!!!!!!
 
Jopo la mahakimu watatu leo lilitoa hukumu ya jumla ya miaka 21 kwa mfanyabiashara Rajabu Maranda ambaye alikuwa katika tuhuma na nduguye za kula njama , kugushi na kuiba fedha za madeni ya nje (EPA) kiasi cha bilioni 1.8.

Watu hao walikuwa wanakabiliwa na tuhuma nane. Hiyo ni hukumu ya kwanza katika mfululizo wa kesi za EPA.

Hukumu hiyo ya mahakimu watatu Ilvin Mgeta, Saul Kinemela na Focus Bambikye iliyotolewa leo majira ya asubuhi kuelekea mchana huu imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Aidha wameamuriwa wakimaliza kifungo chao warejesha hizo fedha au wafilisiwe.
Hukumu hiyo dhidi ya kada wa CCM Maranda na Nduguye Farijali Hussein inaanza kuweka mwelekeo wa kesi nyingine za EPA.

Inadaiwa ndugu hao wawili walitumia nyaraka feki wakisema wao ni Kiloloma
and Brothers na kwamba wanakibali cha kutwaa fedha za BC Cars Export Limited ya Mumbai, India.
Wakili wao Majura Magafu, alisema kwamba wateja wake wanakata rufaa.

Wakiwa ndani si watahamisha wrights za ownership za mali zao au estate zao, sasa watalipa nini au watalipa vipi wakitoka ndani wakati hawana kitu?????????? Mahakimu wamechemsha!!!!!!!!
 
2. ANDREW J. CHENGE

chenge.gif


Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa “mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria….”[6] Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  • Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  • Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  • Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.
Hii inatisha, NI DHULUMA KWA WATANZANIA, inabidi tuandamane tudai katiba mpya ya kulikomboa taifa letu na huu unyangau na ufisadi hadi kieleweke!!!!!!!!!. CHADEMA KAZA BUTI.ALUTA CONTINUA!!!!!!!!!!!
 
finally justice has been made..they got what they deserve for loong time....unavuna ulichopanda..hapa hapa duniani
na Kwa Mungu bado......
 
Hii nchi use@ge umezhdi vifisadi dagaa ndo vinabanwa yale masangala na mapapa yanapeta. Mimi nataka kusikia Mgonja,Yona na Mramba wametiwa ndani ambao ndo walitajwa kwenye hii kesi hao wengine changa la macho, hakuna kitu.
 
I hope ni habari za kweli

CHADEMA watanasema hao jamaa wameonewa

What a shame kwa Chama kama Chadema , angehukumiwa Chenge na Lowasa pia wangesema wanaonewa na Kikwete

Damned if do damned if you dont!!

Maundumula, acha kelele, kwa nini CHADEMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!! Umeniudhi sana tu, kwa kifupi umeharibu siku yangu.
 
"MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, juzi iliwahukumu kifungo cha miaka mitano jela mfanyabiashara maarufu, Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Mbali na kifungo hicho, washtakiwa wametakiwa kurudisha Sh1.8 bilioni walizochota kwenye akaunti hiyo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na endapo watashindwa kufanya hivyo, mali zao zitakamatwa na kutaifishwa.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka manane, yakiwamo kula njama, kughushi, wizi, kuwakilisha hati za uongo na kujipatia fedha kwa udanganyifu kwenye akaunti hiyo, wakijaribu kuonyesha kuwa, kampuni yao ya Kiloloma & Brothers ilikuwa imepewa idhini kukusanya deni la Kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai, India."

SOURCE: Mahakama ya Kisutu & Mwananchi

Today In Perspective:- Samahani Kwa kuwakumbusha najua wengi mtakwazwa lakini nawaomba mnivumilie nimeshindwa kulimeza hili, vipi hii issue kama sio UMMA WA WATANZANIA KWA PAMOJA KUAMUA KUPAZA SAUTI NA KUSHINIKIZA HATUA ZICHUKULIWE, ingekuwa vipi?? Enzi hizo tuliambiwa aliyeibua jambo hili alikuwa mwongo, mzandiki, umbea na mchonganishi, alikuwa amefoji nyalaka na zilipelekwa polisi ili akamatwe na kushitakiwa. Lakini pia MZEE WA KAYA MH. JK alipokuwa ughaibuni na kuulizwa kuhusu wizi uliokuwa umetokea chumbani mwake miaka kadhaa nyuma, alisema hizo ni kelele za wapinzani hazina ukweli wowote ni sawa na kelele za mlango hazimnyimi usingizi, loo!!! Mambo hayo na TZ yenu.
 
Ninachokiona hapa tatizo ni kutokubali mabadiliko na upinzani maana kila mtu atakaye toa hoja ya kukataa uovu anaonekana mpinzani. wakati umefika kwa watanzania kukubali hoja zenye kufichua uovu na kuleta mabadiliko ya kweli kwa mwananchi na tuache kukumbatia uovu maana wahenga walisema ' kwenye ukweli uongo hujitenga' leo imedhihirika wazi hoja ilikuwa ya kweli na watu wamefungwa, je nani muongo mtoa hoja au aliyepinga?
LAZIMA TUBADILIKE HATA KAMA MABADILIKO YANAUMA KWA KUPOTEZEA WATU ULAJI
 
Waliowekwa ndani ni mbuzi wa kafara tu! Tungeipongeza serikali kwa:
1. Kumkamata mmiliki wa Kagoda agriculture
2. KUwakamata na kuwahoji viongozi waandamizi waliopinga kwa nguvu zote kuwa wizi wa EPA haupo
3. Kueleza zile hela zilirudishwa na nani na ziko wapi!
 
Kesi nyingine zipo mahakamani zinaendelea so no need kulalamika hadi hatima ikifikiwa
 
Hizi zile pesa ni 1.8 b eeeti au zilikuwa kama 200billion???
Okey zingine ndo zilirudishwa kwa jk!
 
Back
Top Bottom