Naomba kuuliza, hivi mfano mwanaume wa kikristo ameoa binti wa kiislam na ikaja kutokea wamtofautiana au mirathi, ndoa hapo masuala ya hukumu yatakuwaje kwa mahakama ya Kadhi? Ukizangatia huyu mume ni mkristo, hapo najaribu kujiuliza. Mwenye uelewa wa hili naomba anifahamishe. Maana baadae yasije ya kutokea ya kutokea. Na katika masuala ya uundaji wa mahakama hii, ni vyema mambo haya na yanayofanana na hili yaangaliwe ili yasijeleta mtafaruku huku siku za mbeleni