Mahakama ya Haki za Binadamu: Hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha ilikuwa sawa, japo kuna haki zao zilikiukwa

Kumbuka hii rufaa ni ya siku nyingi wakiwa gerezani bado, hivyo haingeacha kusomwa eti kwa sababu walishatoka kwa msamaha wa Rais! Maadamu shauri lilikuwa mahakamani, hapakuwa na budi, liisha!!!!
Okey, hili sikulijua asante kwa taarifa pia BBC wamelitolea ufafanuzi.
 
Nilijua TU tangu siku ile walipopewa Msamaha wa Rais. Nilimwambia mwenzangu mmoja kuwa Kuna File limechunguliwa, kinachofanyika Ni kui pre empty Mahakama ya Haki za Binadamu ya Africa! It was expected!
 
Sidhani kama watakuwa na guts za kwenda kudai fidia kwa kuwa tu walikaa mahabusu kwa siku nne "tu" bila kufahamishwa makosa yao. Kama ndo hivyo, nadhani bwana mdogo Nondo siku akipata dhamana tu, akafungue case haraka, reference iwe hukumu hii:)
 
Walionewa na kudhalalishwa, wana stahiki kulipwa fidia tena mara moja bila kupingwa.
walio shiriki kuwaonea malipo yao ahera
 
Ngoja niwasamaraizie vilaza...mahakama haijatengua hukumu iliyotolewa. Hivyo itabaki kwenye kumbukumbu kuwa jamaa ni convicted rapists. Ila katika mchakato wa kuwashtaki kina nguza, kuna haki za msingi walinyimwa hivyo wanaweza omba fidia kwa kunyimwa haki hizo....mpo hapo????
Sasa kama Nguza hakupimwa uwezo wake wa kufanya hilo tendo wala damu zao hazikupimwa hiyo basis ya hukumu ilikuwa nini. Hii inatia shaka kwa hukumu hiyo na inaeafanya watu kufikiria kwamba yaweza kuwa sababu ya serikali (rais) alitoa msamaha!
 
Mahakama imewaachia uhuru ingawa wako nje kwa msamaha wa rais, kwahiyo swala ka kudai fidia ni juu yao watavyoona inafaa:
Acha kupotosha mahakama haijaondoa kosa lao la kulawiti watoto limebaki pale pale kuwa walitenda, ilichosema ni kuwa kuna haki zao zilikiukwa kama zilivyotajwa hivyo wanaweza dai fidia kwa haki hizo kukiukwa.
Ina maana kama wasingekuwa nje kwa msamaha wa raisi wangeendelea kubaki ndani kwa hukumu hii
 
Babu seya Anabid adai fidia serikali imlipe... maana. Jogoo wa babu seya jogoo alikuwa Apandi Mtungi.
 
Acha kupotosha mahakama haijaondoa kosa lao la kulawiti watoto limebaki pale pale kuwa walitenda, ilichosema ni kuwa kuna haki zao zilikiukwa kama zilivyotajwa hivyo wanaweza dai fidia kwa haki hizo kukiukwa.
Ina maana kama wasingekuwa nje kwa msamaha wa raisi wangeendelea kubaki ndani kwa hukumu hii
wangeachiwa maana Jogoo wa babu seya apandi mtungi
 
Nawashangaa sana wanaowaita hawa jamaa ni mafirauni,hivi kwani mkuru anaweza kuwatoa pasipo kisa na taarifa zote?tuweni serious sio kubwabwaja
 
View attachment 723364
Nguza Viking na wanae
Mahakama hii imetoa hukumu leo hii ambapo Nguza na mwanae wamepewa siku 30 kuwasilisha maombi ya kutaka walipwe fidia na serikali iwapo watataka kufanya hivyo baada ya hukumu hiyo ya mahakama kutolewa leo hii.

Serikali pia itakuwa na haki ya kupinga Nguza na mwanawe wasilipwe fidia na serikali ndani ya siku 30 kwa kupinga jambo hilo mahakamani hapo iwapo Nguza na mwanae watawasilisha madai hayo katika mahakama hiyo.

Nguza na mwanae walikuwa wamekata rufaa katika mahakama hii kabla ya wao kutoka kwa msamaha wa Raisi.

Chanzo:Azam tv

------------------
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imesema Mahakama za ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili mwanamuziki Babu Seya na mwanawe Papii Kocha, zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine zilikiuka

"Kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya haki za Seya (Babu Seya) na Johnson (Papii Kocha), mahakama imewaruhusu kuwasilisha hoja na kuainisha ni namna wanaweza kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa ndani ya siku 30,"- Jaji Gerald Niyungeko, Mahakama ya Haki za Binadamu,

"Baadhi ya haki zilizotendwa ni pamoja na kuwaachia watuhumiwa watatu kwenye kesi hiyo pamoja na kubakiza mashitaka manne kati ya 21 yaliyokuwa yakiwakabili," Jaji Gerald Niyungeko, Mahakam ya Haki za Binadamu

“Kwa upande mwingine haki zao zilikiukwa, kwa mfano wakiwa Mahakama ya Kisutu walikaaa mahabusu kwa siku nne bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea,"- Jaji Gerald Niyungeko, Mahakama ya Haki za Binadamu

“Aidha, waleta maombi pia waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia wale watoto ambao upande wa jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa,"- Jaji Gerald Niyungeko

Kwa upande mwingine, Nguza aliomba kupimwa kama ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa au lakini pia alikataliwa,”- Jaji Gerald Niyungeko.


Chanzo: Mtanzania
hawa wabakaji na walawiti hawawezi kuja kuwa na amani tena mioyoni mwao watakufa tu .ivi umeshajiuliza alipo zombe leo?
 
wangeachiwa maana Jogoo wa babu seya apandi mtungi
usichanganye pia, uume unaweza kuigizwa hata kama haujasimama na ikatengeneza jinai tayari. Kinachoangaliwa ni kuingia kwa uume tu bila kujali umesimama au la.
 
Nimeanza kujiuliza. Miezi kadhaa kabla ya msamaha wa Raisi Magufuli kutoa msamaha kwa Babu Seya na mwanae Papii, ndugu yao mmoja alitanabaisha kwamba Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu ilikuwa imeamua kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za kisheria katika kesi yao na kusema kwamba ilikuwa imeamua kwamba waachiwe huru, na kwamba uamuzi wa Mahakama hiyo ulifanyika na kilichokuwa kinasubiriwa ni kusoma hukumu tu.

Hukumu hiyo ingemaanisha kwambaTanzania ingeamuriwa kuwaachia huru Babu Seya na mwanae Papii. Kwa maneno mengine, hata bila msamaha wa Raisi Magufuli, suala la kuachiwa huru kwa Babu Seya na Papii lilikuwa limeshafikiwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Ni wazi Raisi Magufuli alijua juu ya uamuzi huu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu. Na kama ni hivyo, inaonyesha kwamba uamuzi wa kusema anawasamehe kina Babu Seya ulikuwa feki, kwa manufaa ya kisiasa na kupunguza aibu kwa Tanzania kuonyesha kwamba Mahakama zetu mara nyingi zinakuwa na msukumo wa kisiasa katika kuamua mambo na kutowapatia watuhumiwa haki zao. Hatusahau kwamba kina Babu Seya walihukumiwa kipindi cha Kikwete (au Mkapa?)

Kwa hiyo sasa serikali ijiandae kulipa mamilioni ya fedha kwa kina Babu Seya na Papii kwa ukiukwaji mkubwa wa haki zao, na serikali inapaswa, kwa mara nyingine tena, ijifunze kwamba ukiukwaji wa haki za watu kuna wakati utakugeuka tu. Bado tuna kesi nyingi mahakamani zinazokiuka haki za watuhumiwa kwa kiwango kikubwa.
 
Back
Top Bottom