Mahakama ya Haki za Binadamu: Hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha ilikuwa sawa, japo kuna haki zao zilikiukwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,388
seyaz.jpg

Nguza Viking na wanae
Mahakama hii imetoa hukumu leo hii ambapo Nguza na mwanae wamepewa siku 30 kuwasilisha maombi ya kutaka walipwe fidia na serikali iwapo watataka kufanya hivyo baada ya hukumu hiyo ya mahakama kutolewa leo hii.

Serikali pia itakuwa na haki ya kupinga Nguza na mwanawe wasilipwe fidia na serikali ndani ya siku 30 kwa kupinga jambo hilo mahakamani hapo iwapo Nguza na mwanae watawasilisha madai hayo katika mahakama hiyo.

Nguza na mwanae walikuwa wamekata rufaa katika mahakama hii kabla ya wao kutoka kwa msamaha wa Raisi.

Chanzo:Azam tv

------------------
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imesema Mahakama za ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili mwanamuziki Babu Seya na mwanawe Papii Kocha, zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine zilikiuka

"Kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya haki za Seya (Babu Seya) na Johnson (Papii Kocha), mahakama imewaruhusu kuwasilisha hoja na kuainisha ni namna wanaweza kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa ndani ya siku 30,"- Jaji Gerald Niyungeko, Mahakama ya Haki za Binadamu,

"Baadhi ya haki zilizotendwa ni pamoja na kuwaachia watuhumiwa watatu kwenye kesi hiyo pamoja na kubakiza mashitaka manne kati ya 21 yaliyokuwa yakiwakabili," Jaji Gerald Niyungeko, Mahakam ya Haki za Binadamu

“Kwa upande mwingine haki zao zilikiukwa, kwa mfano wakiwa Mahakama ya Kisutu walikaaa mahabusu kwa siku nne bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea,"- Jaji Gerald Niyungeko, Mahakama ya Haki za Binadamu

“Aidha, waleta maombi pia waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia wale watoto ambao upande wa jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa,"- Jaji Gerald Niyungeko

Kwa upande mwingine, Nguza aliomba kupimwa kama ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa au lakini pia alikataliwa,”- Jaji Gerald Niyungeko.


Chanzo: Mtanzania
 
Hawa jamaa ni mafiraun mno....nasikitka n kwa nn waliachiwa huru, walionajisiwa cjui wanajisikiaje ?..... Kantagarasi
 
Wanawasafishaaaa ili wawatumie kwenye kampeni.Hawa ni walawiti na wabakajiiiii
Hii mahakama unaijua?

Au ndo yale yale ya kukariri kuwa mahakama hazitendi haki kwa sababu tu hukumu was not in favor of the oppositions.

Ninavyojua, hii mahakama haihusiani moja kwa moja na serikali ya Tanzania na wala majaji wake hawateuliwi na Rais wa Tanzania
 
Hii mahakama unaijua?

Au ndo yale yale ya kukariri kuwa mahakama hazitendi haki kwa sababu tu hukumu was not in favor of the oppositions.

Ninavyojua, hii mahakama haihusiani moja kwa moja na serikali ya Tanzania na wala majaji wake hawateuliwi na Rais wa Tanzania
Tatizo huelew mifumo ya kisiasa ya Dunia hii,ungekuwa unaelewa japo kdogo mithili ya Punje ya haladali usingekosa kuconnect dots.Kwakuwa umeamua kutokuelewa basi ww endelea hvohvo.
 
Hii mahakama unaijua?

Au ndo yale yale ya kukariri kuwa mahakama hazitendi haki kwa sababu tu hukumu was not in favor of the oppositions.

Ninavyojua, hii mahakama haihusiani moja kwa moja na serikali ya Tanzania na wala majaji wake hawateuliwi na Rais wa Tanzania
Kwani iko mbinguni? Si iko Arusha?
 
Tutawalipa tuu cc n donner country, kama tumetumia 18 kwenye by- Election tushindwe kuwalipa hawa, saiz tuko kwenye laiti traki.
 
Ngoja niwasamaraizie vilaza...mahakama haijatengua hukumu iliyotolewa. Hivyo itabaki kwenye kumbukumbu kuwa jamaa ni convicted rapists. Ila katika mchakato wa kuwashtaki kina nguza, kuna haki za msingi walinyimwa hivyo wanaweza omba fidia kwa kunyimwa haki hizo....mpo hapo????
 
Aisee Dude limeemshwa
Kwa taarifa tuu hili shauri lilifunguliwa wakiwa bado gerezani kwa hiyo hakuna dude lililo amshwa na maamuzi yamekuja wakiwa wameshapata msamaha wa Rais....kwa hiyo hii hukumu haina faida yeyote ile....
Hata hivyo haijawaondolea makosa
 
Mahakama imewaachia uhuru ingawa wako nje kwa msamaha wa rais, kwahiyo swala ka kudai fidia ni juu yao watavyoona inafaa:
 
Hawa watu walitolewa kwa msamaha wa rais au walishinda kesi hadi wadai fidia?

Kumbuka hii rufaa ni ya siku nyingi wakiwa gerezani bado, hivyo haingeacha kusomwa eti kwa sababu walishatoka kwa msamaha wa Rais! Maadamu shauri lilikuwa mahakamani, hapakuwa na budi, liisha!!!!
 
Nina imani mpaka raisi kuwasamehe amepewa taarifa za kutosha.

Taabu ni sisi kajamba nani huku nje, kila kitu tunajua.
 
Back
Top Bottom