Mahakama Kuu yasitisha uamuzi wa Serikali kuzuia Vituo 6 vya TV vilivyorusha Maandamano ya Azimio

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mahakama Kuu ya Kenya imechukua maamuzi hayo baada ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kutishia kuvifutia leseni na kutoza faini vituo hivyo ikidai vimekiuka kanuni kwa kurusha matangazo hayo mubashara.

Amri ya Mahakama imezuia CA kuendelea kutoa vitisho kwa Citizen TV, NTV, K24, KBC, TV47 na Ebru TV na kuwa vyombo hivyo vipo huru kuendelea na kazi zao kama kawaida.

Shauri hilo lilifikishwa Mahakamani kwa Hati ya Dharura na Taasisi ya Katiba, Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK) na umoja wa waandishi wa habari vikitaka uhuru wa vyombo vya habari.

Mahakama imeeleza kuwa uamuzi wa CA unaweza kuhatarisha maisha ya watu kwa kuwa utasababisha Polisi wachukue hatua badala ya kuimarisha ulinzi wa watu.




======================

High Court Suspends CA Decision To Censure 6 TV Stations For Covering Azimio Protests

The High Court has suspended the decision by the Communications Authority of Kenya (CA) to censure six Television stations for covering Monday’s demonstrations by the opposition Azimio la Umoja One Kenya coalition party.

In a ruling on Friday, the court issued orders barring the Authority from carrying on with the threat to revoke licences of the six broadcasters among them Citizen TV, NTV, K24, KBC, TV47 and Ebru TV.

According to court papers seen by Citizen Digital, a case filed by the Katiba Institute, Law Society of Kenya (LSK) as well as journalist unions raised weighty issues saying the decision by CA could undermine media freedom.

The court also said that CA’s decision may endanger the lives of people since the police would be acting in absence of the fourth estate as the people’s watchdog.

"CA’s decision could have a chilling effect on media freedom, freedom of information, and freedom of expression,” read court documents.

“Besides, the decision endangers life because it would enable the trigger-happy National Police Service to operate in darkness and police demonstrations without media oversight.”

In a Wednesday letter by CA CEO Ezra Chiloba, the Authority had criticised the said TV stations for broadcasting the protests led by Azimio leader Raila Odinga live, claiming they violated the code of coverage.

Chiloba thus threatened “liability under relevant provisions of the law, including revocation of broadcast licence and/or broadcast frequencies.”

Katiba Institute, in a subsequent letter to CA, condemned the decision terming it as a “threat to press freedom.”

“We see your actions as a threat to freedom of expression, information, and of the media and a repetition of the 2013 TV shutdown by you. Your decision endangers life because it would enable the trigger-happy Kenyan National Police Service to operate in darkness,” Katiba Institute said on Thursday.


Source: Citizen Digital & NTV Kenya
 
Wakenya wanajielewa sio kama nyinyi kondoo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Wenye kujielewa wasingekufa kwa njaa, Wala wasingeruhusu kabila mbili tu ziwe na haki ya kutawala kabila nzingine 43, Wala wasingeruhusu kuchoma makanisa kwa sababu za kisiasa, Wala wasingeshindwa kuzuia njaa.

Katika Karne ya sayansi na technologia bado mnachukiana na kuuana kwasababu ya ukabila, bado watu hawana chakula wanakufa kwa njaa, huko kujielewa kwa namna hiyo ni upumbavu mtupu.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Shabbash kule nchi jirani vyama vimeshindwa kushawishi umma kudai mambo yanayostahiki kwa khofu ya polisi, Kenya ni modern kwa East Africa, Ruto hana namna achakarike watu wapate unga, mafuta na mchele kw bei nafuu wakenya waneemeke
 
Shabbash kule nchi jirani vyama vimeshindwa kushawishi umma kudai mambo yanayostahiki kwa khofu ya polisi, Kenya ni modern kwa East Africa, Ruto hana namna achakarike watu wapate unga, mafuta na mchele kw bei nafuu wakenya waneemeke
Mulikuwa wajinga, mukasoma mukawa wajinga zaidi, ndomana wa-Venezuela wakawachagulia RAISI..
 
Back
Top Bottom