Magufuli: Ningefukuza nusu ya wote ndani ya siku moja kama wangeniimbia eti wana imani na mtu fulani

Ni kweli, bahati nzuri walionekana wazi wazi kwenye TV hivyo JPJM akae akijua kwamba jamaa hao imani yao bado hipo kwa huyo waliokuwa wanampigia debe openly -.

Dk.Magufuli asijidanganye kwamba watatubu na kurudi kwenye kundi - hao niwa kuondolewa tu kwenye jumuhia wanazo simamia, sana sana wabaki ni wanachama wa kawaida wasipewe wadhifa wowote chamani na Serikalini waachwe wale jeuri yao.

Walimdhalalisha sana Kikwete na Chama tawala, unaweza kufikiri awakuwahi kwenda shule - hawafai kabisa hawa. Na ukitaja kuchunguza ni kitu gani hasa kiliwasukuma kufanya utovu wa nidhamu wa hali ya juu utakuta ni kutaka kupalilia vyeo basi - unafiki tu, sio kwamba walimuona mpambe wao anafaa kuliko wengine.
 
Amejidhihirishia ni jinsi gani alivyo na roho ya kisasi na chuki za kibabe. A leader is an example and an image to his/her society,country and world at large so Kama kidooonchi tu anapanic nakutoka povu kiasi cha kuongea tena kwa slogan yke ya dhati as in kutoka moyoni jmn siasa za maji taka kando tuweke tujuzane je likija kubwa atawez kustahimiliiiii?! Cku zooote busara na Hekima zimekuw ni nguzo kuu kwny mafanikio ya vitu vingi ss km asubh yoote hii tunaanz kuwa na uhaba Wa hzo nguzo mchana ukifika itakuaje?!
 
Mungu katuletea Magufuli ili kutudhihirishia kuwa Jakaya Kikwete ni Mwanasiasa bora zaid


mungu anawajalia ccm kwa viongozi ajabu mungu huyo huyo anawahimiza wakaibe hapana yatakuwa miungu ktk amri kumi wizi na uongo hauruhusiw tayar huyo alieletwa na mungu kishanunua boti sijui kivuko kibovu watakuwa miungu mana wanahimiza kusema uongo.
 
Mwenyekiti mpya wa CCM John Magufuli amemsifu Kikwete kuwa na uvumilivu mkubwa na kusema hana uhakika kama yeye ana uvumilivu wa kiasi hicho.
Amesema kuna mkutano uliofanyika na watu wakawa wanaimba wana imani na mtu fulani robo au nusu wangeondoka siku hiyo hiyo, amewataka wajumbe wa CCM kumuombea kwa Mungu angalau awe na nusu ya uvumilivu wa Kikwete


"Nasema kwa dhati kabisa, Mheshimiwa mwenyekiti mstaafu, kuwa huo moyo wa uvumilivu ulio nao, sidhani kama mimi ninao.

Nakumbuka siku ile wanaimba eti wana imani na mtu fulani, ningekuwa mimi ndio mwenyekiti, robo au nusu wangepotea_.

Nawaomba sana ndugu wajumbe, mniombee nipate angalau nusu ya moyo wa uvumilivu alionao bwana Kikwete."



Huu mchezo hautaki hasira
 
Ndio maana watu wanasema hajui chama chake. Akasome kanuni zinasemaje kuhusu kufukuza mwanachama. Anadhani ukiwa mwenyekiti una mamlaka ya kumfukuza mwanachama ukijisikia kama alivyo rais kwa watendaji wa serikali?
kupotezwa na kufukuzwa uanachama ni vitu viwili tofauti.
 
Wangepotea???? Siku hiyo hiyo robo au nusu wangepotea. Uzito wa sentensi hii upo kwenye neno kupotea.
 
Awe na kumbukumbu, waziri mkuu wake ndio kinara wa kuimbia tuna imani na fulani.

Wazee wa kuhamisha magoli naona sasa mnahamishia goli kwa Waziri Mkuu, Magufuli atawatbua wote Na unafiki wenu.
 
Back
Top Bottom